Wakunga Hawa Wanafukuza Uwoga Wako Wa Kujifungua: Waamini

Wakunga Hawa Wanafukuza Uwoga Wako Wa Kujifungua: Waamini

Uwoga wa kujifungua ni halisi na wanawake wengi wanapo karibia siku ya kujifungua huwa na hofu hii. Tazama jinsi ya kupunguza uwoga huu!

Uwoga wa kujifungua ni halisi; kukamilika na jina lake la kisayansi na kila kitu. Wataalum wanaufahamu uwoga huu kama tokophobia. Kutoka uwoga wa sindano hadi kwa uwoga wa damu, kuna sababu kadha wa kadha kwa nini wanawake huwa na uwoga wa kujifungua. Katika hali sugu, baadhi ya wanawake huamua kuto pata mimba.

Lakini huyo sio wewe, ama? Tayari una mimba, pamoja na uwoga kuhusu vitu tofauti. Na wataalum wanasema kuwa uwoga huu ni kawaida, lakini hakuna kitu cha kuwa na uwoga kuhusu. Ni halisi kuwa na hofu chache katika safari yako ya mimba- kwani hili ni jambo jipya kwako na ni vigumu kutabiri yatakayo tendeka katika siku za usoni. Maombi yako ni kuwa safari yako ya mimba ya miezi tisa itakuwa salama na kila kitu kitaenda kinavyo paswa. Na mara nyingi, maombi yako hujibiwa. Baadhi ya wakunga wanaeleza ukweli kuhusu baadhi ya mambo yanayo kutia kiwewe zaidi. Endelea kusoma - na upunguze hofu zako.

Sababu 5 za uwoga wa kujifungua, na kwa nini hupaswi kuwa na shaka

ndoto mbaya wakati wa mimba

Kuenda haja kubwa kwenye meza ya kujifungua

Kuenda haja kubwa katika hatua ya pili ya uchungu wa uzazi, kizazi kinapo funguka kabisa, ni kawaida sana - na madaktari wengi hutarajia hili kufanyika. Wakati ambapo mwendo wa tumbo hufanyika, ina maana kuwa mwanamke ana sukuma vyema na watunzaji wa afya huona hili kama jambo chanya.

Kwa nini hupaswi kuwa na shaka: Wanawake wengi hata hawagundui wanapo enda haja kubwa katika uchungu wa uzazi. Lakini ukifanya hivi, mtu mwingine ataishughulikia. Mwuguzi ako kasi kutoa hata bila ya kutaja kwa mama anaye shuhudia uchungu wa uzazi.

Epidural yako haita fanya kazi

Kwa wanawake ambao wangependa kujifungua na usaidizi wa matibabu, wazo la kufanya hivyo bila matibabu linaweza watia kiwewe.

Kwa nini hupaswi kuwa na shaka: Katika hospitali nyingi, wanawake wanaweza pata epidural katika hatua yoyote katika uchungu wa uzazi, hata wanapo panuka sentimita 10. Na hakuna haja ya kuwa na shaka ya kupata epidural ambayo haitafanya kazi. Kulingana na utafiti ulio chapishwa kwenye makala ya Obstretics & Gynecology, karibu asilimia 12 ya epidurals hukosa kufanya kazi kama zinavyo stahili. Lakini kama bado unahisi uchungu ama unahisi kuwa kuna jambo ambalo haliko sawa, mweleze mwuguzi wako kwa kasi.

Huwezi stahimili uchungu huo wote

Ikiwa umesikia hadithi za kugadhabisha kutoka kwa marafiki wako walio shuhudia vitu vya kushtua wakijifungua, na unahisi uwoga wa uchungu wa uzazi, hauko peke yako.

Kwa nini haupaswi kuwa na shaka: Uchungu wa kujifungua ni tofauti na mwingine ambao huenda ukashuhudia, lakini hilo ni jambo nzuri. Uchungu wa uzazi haudumu. Kubanwa huja baada ya wakati mdogo. Huku kuna maana kuwa, katikati ya kubanwa huku, kuna mapumziko ya kukusaidia kuweza kustahimili uchungu huo. Uchungu wa uzazi pia huongezeka kwa kiwango, na kumkubalisha mwanamke kuibua mbinu za kustahimili uchungu unapo pungua. Kwa hivyo wakati unapo jitayarisha kusukuma, utakuwa tayari.

Uponaji wa c-section huwa na uchungu zaidi

Wakunga Hawa Wanafukuza Uwoga Wako Wa Kujifungua: Waamini

Wanawake wengi huwa na uwoga kuwa c-section inaweza kuwa na maana ya uponaji mrefu zaidi ikilinganishwa na kujifungua kwa kawaida. Wanawake wengi huwa na uwoga kuhusu upasuaji. Ama wanahisi kana kwamba wamefeli wanapo pata upasuaji ambao hawakuwa wamepangia.

Kwa nini hupaswi kuwa na shaka: Uponaji huchukua karibu wiki sita kwa kujifungua kupitia kwa uke ama upasuaji. Lakini kulingana na WebMD, kuna uwezekano wa kuwa na uchungu hadi mwaka mmoja kwa upasuaji. Baada ya yote, huu ni upasuaji. Huenda ukavuja damu kwa muda mrefu na ushuhudie uchungu wa tumbo, hasa kwenye kidonda. Lakini wanawake wengi husema kuwa, mambo hayakuwa mabaya baada ya upasuaji kama walivyo tarajia. Na kumtunza mtoto wako kuta toa fikira zako mbali na uchungu huo.

Hautakuwa kama hapo awali huko chini

siri ya kuishi miaka mingi

Baadhi ya wanawake hutumia kipindi chao cha mimba wakifikiria kuhusu kuraruka ama kuwa na episiotomy. Huwa mbaya zaidi wakati ambapo ultrasound yako inaonyesha kuwa mtoto wako ni mkubwa.

Kwa nini hupaswi kuwa na shaka: Mwili wa binadamu huwa na uwezo wa kupanuka. Katika ujauzito, vichocheo vya relaxin na estrogen hutayarisha tishu za pelvisi kwa kunyooka kwa kujifungua. Kwa hivyo, usiwe na shaka: uke na perineum zako zitapona. Hata kwa kasi zaidi ukiongeza kegels na mazoezi ya kuchuchumaa ama squats kwenye ratiba yako ya mazoezi baada ya kujifungua.

Uki raruka, daktari atakushona kwa kutumia uzi chache, na kidonda kinafaa kupona baada ya wiki ama siku kumi.

Chanzo: cosmopolitan

Soma PiaYote Unayo Hitajika Kujua Kuhusu Utunzaji Baada Ya Kujifungua

Written by

Risper Nyakio