Ufunguzi Wa Shule Nchini Kenya Kuahirishwa Hadi Mwaka Ujao Wa 2021

Ufunguzi Wa Shule Nchini Kenya Kuahirishwa Hadi Mwaka Ujao Wa 2021

Baada ya kungoja kwa muda mrefu kupata habari kuhusu kufunguliwa kwa shule Kenya, waziri wa Elimu nchini George Magoha amesema kuwa shule hazitafunguliwa kwa muhula wa tatu. Kufuatia shaka za ongezeko la watu walio athiriwa na ugonjwa wa Covid-19 na kwa usalama wa wanafunzi. Bwana Magoha aliendelea kusema kuwa kalenda ya masomo ya mwaka wa 2020 imetupiliwa mbali. Wanafunzi watarudi shuleni mwaka ujao (2021) na kuwa wangerudia darasa walilokuwa mwaka huu. Kwa wanafunzi walio ngoja kuifanya mitihani yao mikuu ya darasa la nane (KCPE) na kidato cha nne (KCSE), watangoja hadi mwisho wa mwaka wa 2021 ili kufanya mitihani yao.

Ufunguzi Wa Shule Nchini Kenya Kuahirishwa Hadi Mwaka Ujao Wa 2021

Kufunguliwa Kwa Shule Kenya

Waziri wa Elimu pia aliwashauri wa kuu wa shule ambazo walikuwa wamepokea malipo ya muhula wa tatu na wa pili kuwarejeshea wazazi karo hiyo. Akiendelea kuhutubia wana habari, alisema kuwa wanafunzi wanapaswa kubaki nyumbani hadi Januari mwaka ujao. Pendekezo la kwanza lilikuwa kuwaruhusu wanafunzi wa vyuo vikuu kurudi shuleni Septemba. Ili jambo hili kutendeka, chuo kikuu kilihitajika kutimiza masharti yote yaliyo orodheshwa na wizara ya Elimu hasa kuhusu umbali kati ya wanafunzi na usafi. Hadi wakati huu sio vyuo vingi vilivyo timiza masharti haya. Kwa sababu hii, pia wanafunzi wa vyuo vikuu watasalia nyumbani hadi mwaka ujao.

Kumekuwa na mengi yaliyo semwa na kutabiriwa kuhusu ufunguzi wa shule kwa muhula wa tatu wa mwaka. Huku wazazi wengi wakiwa na shaka za watoto wao kurudi shuleni, wengine wamechoka kukaa na watoto wao na wangependa warudi shuleni. Baada ya wazazi kujua kuwa watoto wao watabaki nyumbani mwaka huu wote, wanapaswa kuibua mbinu ambazo zita hakikisha kuwa watoto wao bado wanasoma wangali nyumbani. Kwani mwaka mmoja ni muda mrefu sana kwa wanafunzi kuto soma na huenda wakasahau walicho kisoma hata ingawa watarudia darasa walilo kuwa. Ni vyema pia wazazi kuwa makini sana na watoto wao kwani kuna mengi yanayo tendeka nchini wakati huu. Usalama wa watoto upo mikononi mwao na wanapaswa kuhakikisha kuwa wana walinda wakati wote, kufahamu wanacho fanya wakiwa nyumbani, kujua watu wanao tangamana nao na pia mahali wanako enda na marafiki zao ama hata peke yao.

kufunguliwa kwa shule kenya

Kumeripotiwa visa vingi vya watoto kubakwa, wengine kufanya ngono na watoto wa rika lao na kupata mimba, huku wengine wakihusika katika matendo ya wizi na uporaji. Wazazi wanashauriwa kuna na mijadala wazi na watoto wao na kuhakikisha kuwa na kazi za kufanya nyumbani ili wasiwe na wakati mwingi wa ziada utakao wafanya wajiingize katika matendo mabaya. Ni jukumu la wanao walinda watoto kuhakikisha kuwa wako salama kabla ya kufunguliwa kwa shule Kenya kufanyika.

Soma pia: Jinsi Wazazi Wanavyo Weza Kuwalinda Watoto Wao Katika Kipindi Cha Lockdown

Written by

Risper Nyakio