Jinsi Ya Kufurahia Maisha Yako Ya Ndoa Kama Mwafrika

Jinsi Ya Kufurahia Maisha Yako Ya Ndoa Kama Mwafrika

Ndoa yenye furaha na inayo dumu muda mrefu inahitaji mambo haya ambayo wanandoa wengi hupuuza.

Tunapo angazia wanandoa ambao wamekuwa kwa ndoa zenye furaha kwa miaka mingi, ni kawaida kutamani uhusiano wa aina hiyo. Walakini, tusicho kiona ni juhudi nyingi wanazo tia ili waweze kufurahia walizo maisha yao ya ndoa.

Hata kama kumekuwa na hadithi nyingi za ndoa zilizo vunjika na habari za kuhuzunisha na kuvunja moyo kuhusu ndoa, tuna furahi kusikia hadithi za wanandoa waliokuwa pamoja kwa muda mrefu na ambao bado wana mapenzi tele ya wenzi wao. Kenya, tuna angalia watu mashuhuri kama Nameless na Wahu ambao wote ni waimbaji na wana ndoa ya kutamaniwa. Wamekuwa pamoja kwa zaidi ya mwongo mmoja. Bila shaka ili kufika hapo, walitia bidii na juhudi nyingi katika uhusiano wao ili watangamane vyema.

kufurahia maisha ya ndoa

Uhusiano wao ulianza walipokuwa wangali chuo kikuu na katika wakati ambapo walikuwa wana anza kuimba na bado hawakuwa wametambulika sana. Baada ya kumaliza chuo kikuu kila mtu alihitimu na shahada tofauti na wakaendeleza uhusiano wao. Miaka 13 baadaye, wawili hawa wamebarikiwa na watoto wawili na watu wengi wana tazamia uhusiano na ndoa yao

Tuna angazia vidokezo muhimu vya kukusaidia kufurahia maisha ya ndoa

Vidokezo 5 vya kukusaidia kuboresha na kufurahia maisha yako ya ndoa

Msifu mchumba wako

Kila mtu anapenda kusifiwa na kupongezwa anapo fanya jambo nzuri ama hata kuvalia mavazi ya kupendeza. Hakikisha kuwa wewe sio mchoyo wa sifa hasa kwa mchumba wako. Mpongeze kwa kukumbuka mambo madogo unayo yadhamini. Kwa njia hii, unam himiza kuendelea kufanya matendo hayo.

Tupilia mbali matatizo ya kale

Baadhi ya wakati, huenda ukapata majaribio ya kuibua matatizo ya hapo awali ili kulinganisha alicho fanya hapo awali na anacho kifanya wakati huu. Hili ni jambo ambalo nyote mnapaswa kuepuka ili usimwumize mchumba wako. Hasa ikiwa jambo unalo taka kuibua halikuwa limetatuliwa ipasavyo.

uhusiano unao dumu

Mzawadi mara kwa mara

Kumzawadi mchumba wako ni jambo ambalo halija kumbatiwa ipasavyo katika nchi za Afrika. Unapo mzawadi mchumba wako mara kwa mara, unamdhihirishia kuwa unamjali na kumfikiria kila mara. Pia unapo mnunulia zawadi, hakikisha kuwa unamzawadi kitu anacho kipenda ama kitu ambacho amekuwa akitarajia kuwa nacho. Kwa njia hii atafurahia zaidi na pia ungependa kumpatia kitu ambacho atakitumia na sikukiweka kwenye nyumba bila kutumia.

Usimlinganishe mwenzi wako na wengine

Kuna watu walio na uraibu wa kuwalinganisha wenzi wao na watu wengine ama hata na wapenzi wao wa hapo awali. Kila uhusiano huwa na changamoto na upekee wake. Na hakuna wakati ambapo uhusiano mmoja utakuwa sawa na mwingine. Kwa hivyo epuka kumlinganisha mchumba wako na marafiki ama hata jamaa wako. Unapomlinganisha na wengine, utafanya akose kujiamini ama hata hisia zake kwako zianze kufifia. Badala yake, msaidie kwa mambo anayo kosea ili awe bora.

Jinsi Ya Kufurahia Maisha Yako Ya Ndoa Kama Mwafrika

Sherehekea mambo muhimu

Kusherehekea vitu vinavyo wapendeza kama wanandoa ni kipindi chenu kuwa na wakati pamoja. Ikiwa mchumba wako angependa kusherehekea mwaka mmoja kwenye nyumba mnayo ishi, kuzaliwa kwa mtoto, kufuzu kwenye masomo yake, usipuuze. Hata kama hauna hamu ya kuwa kwenye sherehe hiyo. Mtapata wakati wa kuwa pamoja.

Kwa jumla, kuzungumza na kusikizana ni sababu kuu inayo himiza wanandoa kufurahia maisha ya ndoa na kuwa pamoja kwa muda mrefu. Hakikisha kuwa unazungumza na mwenzi wako kuhusu mambo yoyote yale yanayo kusumbua. Pia ni muhimu kusoma lugha yao ya mapenzi ili ufahamu mambo yanayo wafurahisha.

Soma Pia: Baadhi Ya Wanandoa Nchini Kenya Watakao Kutamanisha Kufunga Ndoa!

Written by

Risper Nyakio