Watoto Wako Wanapaswa Kujua Kuguswa Kunako Faa Na Kusiko Faa

Watoto Wako Wanapaswa Kujua Kuguswa Kunako Faa Na Kusiko Faa

Kuguswa kunako faa na kusiko faa ni maneno yanayo tumika kuwaelezea watoto aina ya mguso wa mwili ulio sawa na usi faa. Ni muhimu sana katika kuwasaidia kuelewa visa ambapo wanaweza eleza mtu wanaye mwamini kuhusu na kuomba usaidizi. Maneno haya yanawasaidia kujua jinsi wanavyo paswa kuwasiliana na watu. Kwa watoto, "mguso mzuri" ni kuguswa na mtu anaye wajali. Unao faa kwa usalama na afya yao na kuwasaidia kuhisi wako salama. Mguso usiofaa ni mtu yeyote anaye wafanya wahisi kuogopa na kuwa hawako salama. Pia mguso wowote katika sehemu nyeti zao, isipokuwa pale ambapo inahitajika kwa afya yao. Kwa watoto wanao cheza pamoja, sharti nzuri ni kuwa, iwapo mtu mwingine hafurahii, unapaswa kuwacha.

Kwa Nini Ni Muhimu?

Katika nyakati hizi na umri, ambapo watu wana wabaka watoto na usalama wa watoto uko hatarini sana, ni muhimu sana kuwajulisha watoto kuhusu kuguswa kunako faa na kusiko faa na jinsi ya kuongea wanapo hisi wana ogopa ama hawako salama. Ni mada ambayo huwa tatiza wazazi wengi na wana hangaika kuizungumzia. Walakini kuna nguvu nyingi katika maarifa. Ni muhimu kuwa na mjadala huu na watoto wako ili wajue wanapokuwa hatarini.

Mifano ya kuguswa kunako faa

Mifano ni kama vile mwanajamii anapo kukumbatia, na mtoto kuitikia mwito huo, mzazi kumbadilisha nepi, kumsafisha mwili, mtoto kukalia paja la mzazi wake na kusoma hadithi pamoja. Daktari anapo shika mtoto kwa upole ili kuangalia jeraha lake, watoto kucheza pamoja bila kuumizana.

Mifano ya kuguswa kusiko faa

Baadhi ya mifano: mtu anapo guza sehemu nyeti za mtoto wako na hahusiki na afya ya mtoto wako. Mtu yeyeyote anapo mgusa mtoto na kumwambia asimwambie mtu yeyote, iwe siri yao. kukumbatiwa na mtu asiye mjua na kuhisi kuwa hayuko salama, watoto kucheza pamoja, mmoja kuumia na mwingine kuendelea kucheka bila kukoma.

Jinsi ya kumfunza mtoto wako kuhusu mambo haya

kuguswa kunako faa na kusiko faa

  • Anza kuwafunza watoto wangali wachanga:  Anza kuongea na watoto wako kuhusu kuguswa vizuri na kuguswa vibaya, mapema iwezekanavyo ili wawe na maarifa haya muhimu.
  • Wacha kuwa na starehe ama uwoga:Huenda baadhi ya wazazi wakawa na uwoga wa kuzungumzia baadhi ya mada nyeti na watoto wao. Ila, masomo huanza nyumbani na ni muhimu sana ili watoto wako wawe salama. Weka kando starehe na uwoga wako kuhusu kuwa na mijadala mbali mbali na mtoto wako. Anza kwa njia rahisi ambayo wataelewa.
  • Anza kwa kuwafunza watoto wako kuhusu sehemu nyeti: Waeleze kuwa sehemu za mwili ambazo tuna funika ni sehemu nyeti na ambazo hakuna mtu anaye paswa kugusa. Waeleze kuwa hata wazazi wana wagusa pale tu wanapo wasafisha na si kwa sababu ingine yoyote.
  • Wafunze watoto majina sahihi ya kuita sehemu zao za mwili, ikiwemo sehemu nyeti zao. Watoto mara nyingi hutatizika kusema wanapo bakwa kwa sababu hawajui maneno ya kutumia. Kuwa na maarifa ya maneno sahihi ya kutumia kunawasaidia watoto kujua majina ya kutumia na jinsi ya kusema wanapo shikwa kwa njia isiyofaa.
  •  Wafunze watoto wako kuwa wao ndiyo wana umiliki wote wa mili yao. Ni vyema kuwafunza watoto wako kuwa wao ndiyo wana usemi kuhusu maisha yao na jinsi mili yao inavyo paswa kuwa.

kuguswa kunako faa na kusiko faa

  • Mweleze mtoto wako kuwa kuna aina tatu ya kuguswa. Hizi ni: kuguswa kuliko samaa- kunako wasaidia watoto kuhisi wako salama na kunako wafaa, na kunako wasaidia watoto wahisi kuwa wanapendwa na wana jaliwa. Kusiko faa/salama. Huku kuna waumiza watoto ama kuwafanya wahisi kuwa hawako salama. Wafunze kuwa aina hii sio sawa na wanapaswa kuongea iwapo wanaguswa kwa njia isiyo faa. Kuguswa kusiko takikana. Huu ni mguso ambao huenda ukawa salama kwa watoto ila wanahisi kuwa hawahitaji katika wakati huo. Wasaidie watoto wako kusema 'hapana' kwa heshima.

Watoto wanapaswa kufanya nini mtu anapo wagusa kwa njia isiyo faa?

kuguswa kunako faa na kusiko faa

  • Waseme hapana! Mwambie mtu huyo kuwa hupendelei na hutaki kuguswa.
  • Ondoka kwa upesi! Kimbia mbali na mtu aliye kugusa kwa njia isiyo faa. Usikae peke yako na mtu kama huyo tena.
  • Omba usaidizi. Unaweza piga nduru.
  • Jiamini. Hauku fanya kitu chochote kisichofaa.

Kumbukumbu: Smart School Junior

Soma pia: Sex After Kids: How To Keep Up The Tempo With Your Partner

Written by

Risper Nyakio