Watoto Wako Wanapaswa Kujua Tofauti Ya Kuguswa Vizuri Na Vibaya

Watoto Wako Wanapaswa Kujua Tofauti Ya Kuguswa Vizuri Na Vibaya

Mambo tofauti kwa wazazi kuwafunza watoto wao wangali wachanga ili kuhakikisha kuwa wana uwezo wa kujilinda.

Kuguswa vizuri na vibaya kwa watoto ni maneno yanayo tumika kueleza watoto aina tofauti za mguso wa mwili ulio sawa na usio faa. Inawasaidia kuelewa visa tofauti na wanapo paswa kuwaambia watu wanao walinda kuwa hawa hisi wako salama. Maneno haya pia yana wasaidia kujua jinsi wanavyo paswa kuwa na watoto wengine. Kwa watoto, kuguswa vizuri ni aina ya kuguswa kunako mfanya ahisi ako salama. Kuguswa vibaya kunamfanya mtoto ahise kuwa hayuko salama na ana hofu. Hakuna anaye paswa kumgusa sehemu nyeti zake mbali na mzazi anapo msafisha na daktari anapo mkagua. Na wanapo cheza, wanapaswa kukumbuka kuwa ikiwa wanaye cheza naye hafurahii, anapaswa kukoma mchezo huo.

Umuhimu wa kufanya hivi ni nini?

Katika nyakati hizi, udhalilishaji kingono kwa watoto umekuwa kwa ongezeko kubwa, na usalama wa watoto kuwa hatarini. Ni muhimu sana kwa watoto kuelewa tofauti kati ya kuguswa vizuri na vibaya na jinsi ya kujieleza kwa ujasiri na bila uwoga iwapo wanahisi kuwa hawako salama. Ni jambo ambalo wazazi wengi wana wakati mgumu kuongea kuhusu jambo hili. Walakini, kujua kuna nguvu. Ni muhimu kwa kila mzazi kuwa na mjadala huu na watoto wake wangali na umri mdogo.

Mifano ya kuguswa vizuri

Baadhi ya mifano: jamii kujitolea kumkumbatia mtoto, na mtoto wako kukubali; mzazi kubadili diaper ya mtoto ili awe msafi; mtoto kukalia paja la mzazi wake anapo somewa hadithi; daktari kumsugua mtoto kwa utaratibu mahali alipo umia, na kuongea na mtoto wako; watoto kucheza pamoja bila kuumizana.

Mifano ya kuguswa vibaya

Mifano kama vile: iwapo yeyote anagusa sehemu za siri za mtoto wako hafanyi jambo nzuri kwa afya ya mtoto wako; yeyote anaye wagusa na kuwaambia iwe siri yao na wasimjulishe yeyote; iwapo lazima mtoto wako amkumbatie jamii hata kama anamwogopa; watoto wawili wakicheza pamoja, na mmoja wao kuumia wakicheza, mmoja wao anaumia ama hapendelei anapaswa kukoma.

Jinsi ya kuwafunza watoto wako kuhusu jambo hili

kuguswa vizuri na vibaya kwa watoto

  • Anza kuwafunza watoto kutoka umri mchanga: Anza kuongea na watoto wako kuhusu kuguswa vizuri na vibaya mapema uwezavyo ili waelewe kuwa na suala nyeti.
  • Toka kwa imani zako: Huenda wazazi waka kosa uhuru wa kuongea kwa wazi na watoto wao kuhusu mada nyeti, ila, kusoma huanza nyumbani na ni muhimu kwa usalama wa mtoto wako. Weka imani zako kando na uongee na mtoto wako kwa njia rahisi na ambayo ataweza kuielewa.
  • Anza kuwafunza watoto wako kuhusu sehemu zao za siri: Wafunze kuwa sehemu zinazo fichikwa na nguo ni za siri na hakuna mtu anaye kuwa na ruhusa ya kuwagusa, mbali na wazazi wao wanapo waosha ama daktari anapo fanya kipimo cha mwili.
  • Wafunze watoto majina sawa ya sehemu mbali mbali za mwili, hasa sehemu zao za siri: Watoto wengi huenda ikawa wao hutaabika kuongea kuhusu kudhalilishwa kingono kwani hawajui maneno ya kutumia. Kusoma majina sawa ya sehemu nyeti za miili yao kunawasaidia watoto kujua maneno ya kutumia na pia kuongea kuhusu sehemu zao za mwili.
  • Wafunze watoto wao kuwa wao ndiyo walio na usemi kuhusu miili yao: Ni vyema kwa watoto wako kujua kuwa wao ndiyo wakubwa wa miili yao na hawapaswi kumkubalisha mtu yeyote kuwagusa kwa njia isiyo wafurahisha na isiyo faa. Kama vile " Usinirukie hivyo, tafadhali wacha, sipendelei unacho fanya." Na pia wafunze kuheshimu miili ya watu wengine na kukoma wanapo ambiwa wakome.

good touch and bad touch

  • Mwelezee mtoto wako kwa kuhusu njia tatu tofauti za kuguswa. Kuna aina tatu za kuguswa. Hizi ni: Kuguswa kuliko salama- kuguswa huku huwafanya watoto wahisi salama na ni nzuri kwao, na wanahisi kuwa wana pendwa na kuwa wao ni muhimu. Kuguswa kusiko salama. Kuguswa kwa aina hii huumiza hisia na miili yao, kwa mfano wanapo gongwa na kitu, kufinywa ama kusukumwa. Wafunze watoto wako kuwa kuguswa kwa njia hii si sawa. Kuguswa kusiko faa. Aina hii ya kuguswa huenda ikafanya watoto wahisi wako salama ila huwa kwa mtu asiye faa. Mfunze mtoto wako kuwa na ujasiri wa kusema hapana anapo guswa kwa njia isiyo faa.

Watoto wanapaswa kufanya nini mtu anapo wagusa kwa njia isiyo faa?

kuguswa vizuri na vibaya kwa watoto

  • Sema hapana! Mjulishe mtu huyo kuwa hupendelei kuguswa hivyo.
  • Kimbia mbali na mtu anaye kugusa vibaya. Usikae peke yako na mtu huyo tena.
  • Omba usaidizi. Ukiweza piga nduru.
  • Jiamini. Hakuna kitu kibaya ulicho kifanya.

Kumbukumbu: Smart School Junior

Soma pia: Sex After Kids: How To Keep Up The Tempo With Your Partner

Written by

Risper Nyakio