Yote Unayo Hitaji Kujua Kuhusu Barbie Doll Wa Afrika

Yote Unayo Hitaji Kujua Kuhusu Barbie Doll Wa Afrika

Chelsea Ndirangu ni model wa Kenya anaye fahamika kama Afrika Barbie Doll na angependa kuwa kwenye kurasa ya kwanza ya jarida kama vile Vogue.

Huenda ukawa ulisoma kuhusu Barbie Doll wa Afrika katika mojawapo ya kona za mtandao, na kushangaa nani aliye nyuma ya jina hili lisilo la kawaida. Jina lake halali ni Chelsea Ndirangu. Na maswali yako yako karibu kujibiwa. Malaika huyu wa kumodel wa Kenya alikaa kitako na kuanza mjadala na James Kahongeh kutueleza kuhusu maisha yake, alivyo lelewa US, kazi ya ya modelling, jina lake la kipekee na mengineyo.

Barbie Doll Wa Afrika

african barbie doll

Barbie Doll wa Afrika bila shaka ni jina la kibinafsi na sio maarufu na sio jambo jipya tunapo uliza kuhusu jina hili katika mahojiano. Kama unavyoweza kutarajia, wafuasi wake wa mtandaoni walimchagulia jina hili na likabaki kutumika na watu wengi. Chelsea alisema akiendelea kuongea kuhusu jina hili.

"Familia ya mtandao ilinichagulia jina hili, alisema. "Nime ambiwa mara nyingi jinsi sura yangu inavyo kaa kama kijidoli. Jambo hili lina hisi vyema na kana kwamba sio la kawaida. Mwaka ulio pita mwezi wa Julai, nilipunguza urefu wa nywele zangu zikakaa kana kwamba mawimbi. Kila mtu alionekana kupenda mtindo wangu mpya na jinsi ulivyo ambatana na uso wangu. Napenda jina hili; lina toshea kwenye utu wangu wa kimchezo mchezo."

Yote Unayo Hitaji Kujua Kuhusu Barbie Doll Wa Afrika

Barbie Doll wa Afrika anaendelea kuongea kujihusu: alizaliwa Kenya na kulelewa Arlington/Mansfield huko Texas, US. Alianza kuwa model alipokuwa umri wa miaka saba. Kumwuliza kilicho msukuma kwa tasnia hii, alisema: "Nilipokuwa nakua, ningechukua magazini za mamangu na kuanza kutazama kurasa zake, na kufurahishwa na models walio kuwa warembo sana. Kisha ninge waiga kwa kusimama kama wao mbele ya kioo. Ndoto yangu ilikuwa siku moja kuwa kwa kurasa ya kwanza ya jarida. Model ninaye mpenda zaidi ni Naomi Elaine Campbell. Wakati wote nilidhania kuwa ikiwa anaweza, mimi pia ningeweza. Na hivyo ndivyo nilianza kufuata ndoto yangu."

african barbie doll

Cha zaidi, Chelsea anaongea kuhusu kilele cha kazi yake katika mashindano ya modelling yenye jina la "Kuweka Familia na Utangamano" huko Dallas mwanzo wa mwaka huu. Alieleza hiyo kama kazi yake ya kwanza iliyo kuwa na mafanikio. Haijakuwa rahisi kwa Barbie Doll wa Afrika. Ametatizika kujaribu kuwaiga models walio fanikiwa, kabla ya kugundua kuwa anapaswa kuwa alivyo na kuwa modelling ni kuhusu utu wako na mtazamo wako. Kisha umri na unavyo kaa.

Na James anapo uliza ni nchi gani angependa kuwakilisha kama model, jibu lake lilikuwa Kenya. Alisema: "Bila shaka ingekuwa Kenya. Nina bahati kupata mapenzi na kuungwa mkono sana na watu kutoka nyumbani. Marafiki zangu walio Kenya ndio egemezo langu kuu. Wakati ambapo huenda tusionane mara kwa mara, wao ni kama familia kwangu. Kwa hivyo Kenya siku yoyote ile."

Mwishowe, kila mtu anaye fanya kazi anapenda kuangalia mahali ambapo angependa kuwa siku za usoni. Kuwa na ndoto za kufuzu. Na Chelsea sio tofauti. Katika kipindi cha miaka mitatu, ana matumaini kuwa akifanya kazi na uajenti wa modeling ambao anapendelea. Kwa kuongeza, ana matumaini ya kuwa model wa Victoria Secret na kuonekana katika kurasa ya kwanza ya i-D, Vogue na Harper Bazaar. Na pia kuenda Met Gala.

Hitimisho

Katika ndoto zake zote, Barbie Doll wa Kiafrika pia angetaka kuanzia uajenti wa modelling nchini Kenya ndoto zake zinapo timika. Ili kuifanya iwe rahisi kwa watu wachanga ambao wangependa kuwa models.

Soma zaidi: ‘My Physique Wasn’t Right’ – Tonto Dikeh Explains Why She Did Bum Surgery

Chanzo: Nation

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio