Mzunguko wa kawaida wa hedhi kwa wanawake huwa siku 28. Kuna baadhi ya wanawake ambao mizunguko yao huwa kati ya siku 21 hadi 35. Kuingia hedhi mara mbili kwa mwezi hufanyika pale ambapo mzunguko wake hukamilika katika kipindi cha mwezi mmoja. Ikiwa mwanamke ana mzunguko wa siku 25 kisha kupata hedhi yake tarehe 2 ya mwezi. Mzunguko wake utakamilika tarehe 27 kisha kipindi kinachofuata kuanza. Kwa hivyo atakuwa amepata vipindi viwili vya hedhi katika kipindi cha mwezi mmoja.
Sababu za kupata hedhi mara mbili kwa mwezi

Mbali na hilo, kuna sababu ambazo huenda zikamfanya mwanamke kupata hedhi mara mbili kwa mwezi. Kama vile:
- Mabadiliko ya hali ya anga ama kubadili mazingira
- Kuwa na uterine fibroids ama uvimbe katika kizazi
- Kutumia mbinu za uzazi wa mpango
- Kusongwa kimawazo
- Kutokuwa na viwango sawa vya vichocheo mwilini
- Kufanya mazoezi makali kupitiliza
- Maambukizi kwenye kizazi ama maambukizi ya kisanaa
- Kuharibika kwa mimba
- Madhara ya kuvurugika kwa hedhi
- Kutatizika kupata mimba
- Maambukizi kwenye kizazi na mirija ya uzazi kuziba
Manufaa ya kuwa na hedhi ama mzunguko wa kawaida
- Kushika ujauzito kwa kirahisi
- Mama ana nafasi ya kufanya uamuzi wa jinsia ya mtoto atakayopata
- Uhakika wa kutokuwa na baadhi ya maradhi kama vile fibroids ama mirija ya uzazi kuziba
- Kupangia ujauzito kabla ya kupata
Suluhu la kuingia hedhi mara mbili kwa mwezi

Wakati wote unapokuwa na matatizo ya kiafya, ni vyema kutibiwa hospitalini. Utafanyiwa vipimo vya kusaidia kubaini vyanzo vya tatizo lako. Kisha kupatiwa dawa za kurekebisha hali yako.
Kuna baadhi ya mambo ambayo unaweza kufanya kuboresha afya na hali yako. Kama vile:
Kuondoa sumu mwilini. Kuwa na kiwango kingi cha sumu mwilini huathiri mfumo wa ovari mwilini na kuwa vigumu kuzalisha yai. Badala yake, mwanamke huenda akawa na uvimbe kwenye mirija ya uzazi na fuko la uzazi pia.
Kuboresha lishe yako. Lishe huchangia pakubwa katika utendaji kazi mwilini. Kupata madini na vitamini tosha ni muhimu katika kazi zinazo fanyika mwilini na pia kusawasisha kiwango cha vichocheo mwilini.
Kuboresha kinga mwilini. Kupungua kwa kinga mwilini kunamweka mwanamke katika hatari ya kuugua maradhi tofauti. Kupata maambukizi kwenye ovari inakuwa rahisi. Kuwa na kinga bora ni muhimu katika kuulinda mwili dhidi ya maambukizi. Lishe iliyo na mboga na matunda ni muhimu katika kutimiza lengo hili.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Kutumia Siku Ya Kwanza Ya Kipindi Cha Hedhi Kufahamu Umri Wa Mimba