Vidokezo Vya Kuishi Bila Ugomvi Na Mama Mkwe Wako

Vidokezo Vya Kuishi Bila Ugomvi Na Mama Mkwe Wako

Uhusiano wako na mama mkwe wako ni spesheli. Kwa sababu hii, tuna angazia vidokezo muhimu vya kuishi kwa amani na mama mkwe wako.

Tumeona sinema nyingi kuhusu mama mkwe aliye na wivu, hasa kama unapenda kutizama video kutoka nchi ya Nigeria. Patience Ozokwor ni mojawapo ya waigizaji wanao sifika kwa talanta yake. Katika sinema nyingi, ameigiza kama mama mkwe mwenye wivu na huenda watu wakamuogopa kwa hilo. Ila, sio mama mkwe wote walio kama Bi. Patience, hasa kama unaishi pamoja na wazazi wa bwanako. Utaishi vipi kwa amani na wazazi wa bwanako bila kugombana mara kwa mara? Jinsi ya kuishi na mama mkwe mwenye wivu na ugomvi.

Jinsi ya kuishi kwa amani na mama mkwe mwenye wivu

Baini Mipaka

Vidokezo Vya Kuishi Bila Ugomvi Na Mama Mkwe Wako

Amua jinsi ambavyo ungependa nyumba yako iwe. Unapo pata picha ya nyumba ambayo ungependa kuwa nayo, hakikisha kuwa kuna mipaka na umjulishe mama mkwe wako. Kuwa na mipaka hii ya afya kutasaidia kuepuka kugombana mara kwa mara.

Puuza mambo mengine

kuishi na mama mkwe

Maneno haya mawili yataisaidia nyumba yako kwa sana. Unapokuwa umekasirika, badala ya kufanya kelele, kaa chini kisha msikizane. Puuza mambo madogo, ila hakikisha kuwa umemwambia ili kuepuka ugomvi hapo usoni. Walakini, kupuuza mambo machache hapa na pale ni vizuri ili familia yote iwe na amani. Pia, viwango vyako vya kukua vita ongezeka.

Kuwa na msimamo dhahiri

Hapana, sio katika GTBank Food and Drink Festival. Kuwa mkarimu, ila kuwa na msimamo pia. Kataa kutumika vibaya ama kupuuzwa. Chukua msimamo kwa heshima. Hakikisha kuwa unamwambia kwa heshima kuhusu vitu ambavyo unapenda na vile ambavyo hupendi. Huku kutakusaidia kuboresha heshima katika uhusiano wenu.

Usi tete

Vidokezo Vya Kuishi Bila Ugomvi Na Mama Mkwe Wako

Wanawake mara kwa mara huteta kuhusu mama mkwe wao kwa karibu kila mtu, hasa kwa mabwana zao. Ila, hili sio jambo la busara. Badala yake, mara nyingi, utapata kuwa bwanako ana muunga mamake mkono. Kwa hivyo, koma kuteta. Badala yake, chukua usukani wa jambo hilo na ujaribu kulitatua ili lisikusumbue.

Punguza matarajio yako

Wakati ambapo ni vyema kuwa na uhusiano wa mama na binti yake na mama mkwe wako, huenda mambo yakawa tofauti mara kwa mara. Matarajio mengi huenda yakafanya uvunjike moyo. Lina moyo wako.

Toa mtu wa kati kati

kuishi na mama mkweMazungumzo bila kuhusisha mtu wa kati kati yatasaidia kutatua matatizo yenu. Mtu wa katikati ataongeza ugomvi, chuki na matatizo yenu. Iwapo una tatizo lolote, mwongeleshe bila kuhusisha mtu mwingine na pia ufanye hivi kwa heshima. Usimwambie bwanako akusaidie kutatua tatizo hilo.

Gawana majukumu

kuishi na mama mkwe

Wanawake wengi huhisi kana kwamba kuna mashindano na mwanamke aliye katika maisha ya mvulana wao. Wao huona kana kwamba anachukua nambari yao maishani mwao. Jambo hili huleta ugomvi na majukumu ambayo mama mkwe hataki kuwacha maishani mwa mtoto wake. Njia bora ya kuepuka matatizo kama haya ni kugawana majukumu. Kuwa na mjadala na mfanye uamuzi jukumu ambalo kila mtu atakuwa anatimiza. Kwa sababu ana umri zaidi, tunge shauri achukue usukani wa kutaja majukumu ambayo angependa kutimiza.

Usimhusishe katika ndoa yako

Wakati mwingi, wamama watachukua upande wa wavulana wao haijalishi tatizo ni lipi. Hakikisha kuwa unamtenga na mambo ya ndoa yako.

Kumbuka kuwa siku moja watoto wako watakuletea mabibi zao pia na utakuwa mama mkwe. Uvumbuzi huo utakuongoza katika matendo na uamuzi wako.

Soma pia: Pushy Mothers With High Expectations Raise Successful Daughters

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio