Jinsi Tunavyo Fikiria Kuhusu Uchungu Wa Uzazi Kunaweza Badili Tunavyo Hisi

Jinsi Tunavyo Fikiria Kuhusu Uchungu Wa Uzazi Kunaweza Badili Tunavyo Hisi

Uchungu wa uzazi huwa tofauti na aina zingine za uchungu kwa sababu huibuka katika mchakato asili ambapo mwili wa mwanamke unafanya unacho paswa kufanya.

Sio jambo geni kwa mwanadada yeyote aliye na mtoto: kujifungua kuna uchungu. Haijalishi namna unayo pata mtoto wako na hakuna njia sawa ama mbaya ambayo mwili wako hupitia mchakato huu. Hata mchakato huu ukiwa wa kupendeza na wa kimiujiza, huwa na uchungu mwingi zaidi, na huenda ikawa swali lako kuu ni jinsi ya kujifungua bila uchungu.

Lakini utafiti mpya umeangalia jinsi na kwa nini uchungu wa uzazi huathiri wanawake vitofauti. Kulinagana na utafiti kutoka kwa chuo kikuu cha La Trobe, kubadili jinsi jamaa inavyo fikiria na kuongea kuhusu kujifungua kunaweza fanya mabadiliko makubwa katika kuboresha jinsi wanawake wanavyo ishuhudia. Mtaalum wa uchungu wa uzazi daktari Laura Whitburn aliongea na wamama wapya katika hospitali mbili huko Melbourne kusikia kuhusu ushuhuda wao wa uchungu wa uzazi.

"Uchungu wa uzazi huwa tofauti na aina zingine za uchungu kwa sababu huibuka katika mchakato asili ambapo mwili wa mwanamke unafanya unacho paswa kufanya, badala ya kitu kuenda mrama," alisema daktari Whitburn. "Hakuna kupinga kuwa kubanwa kwa uchungu wa uzazi huwa na uchungu mwingi. Uchungu huu una fuzu katika lengo la kushika makini ya mama aliye katika uchungu wa uzazi na kumhimiza kutafuta usalama na utunzaji anapo jifungua. Lakini utafiti wangu unaonyesha kuwa sio kila mtu anaye shuhudia aina hii ya uchungu kwa njia sawa".

Njia bora ya kujifungua bila uchungu: "Uchungu wenye lengo"

Jinsi Tunavyo Fikiria Kuhusu Uchungu Wa Uzazi Kunaweza Badili Tunavyo Hisibegi ya kujifungua

Utafiti huo ulishauri kuwa ikiwa wanawake wanaweza kubadili fikira zao kuhusu uchungu wa uzazi uwe "uchungu wenye lengo" na wabaki wakiwa makini katika mchakato huu, wana nafasi zaidi za kutoka na ushuhuda chanya.

"Wanawake wanao ingia katika uchungu wa uzazi na fikira kuwa kuna lengo la uchungu wao, huonekana kuweza kufanya uchungu uwe sehemu ya mchakato huo. Wana nafasi changa za kuhitaji usaidizi kama vile epidural ama c-section." Aliongeza daktari Whitburn.

Pia aliangalia athari ya watunzaji katika kujifungua na walivyo athiri jinsi wanawake walivyo hisi katika uchungu wa uzazi."Inaonekana kuwa sehemu moja ya kubaki makini na ukipigana katika uchungu wa uzazi ni anaye kutunza. Kuwa na mkunga ama mtu wa kuegemeza unaye jua na kuamini, na anaye tuma ujumbe chanya kuhusu mwili wako na unavyo endelea kunaweza saidia kuboresha uwezo wa mwanamke wa kukumbana na uchungu huo," alisema.

Kujaribu kuepuka mbinu za kuingilia kati

Daktari Whitburn alikuwa makini kusema kuwa, walakini, kuna tofauti iliyo bayana kati ya uchungu wa uzazi wa 'kawaida' ulio kwa sababu unafanya kazi ya kusukuma kiumbe kutoka mwilini mwako - na uchungu 'usio wa kawaida' unao husika na changamoto - ambao wakati wote utahitajika kuingiliwa kati.

Kuna shaka inayo kua kuwa, mbinu za kuingilia kati za kimatibabu zina ongeza hatari za kiafya kwa mama na watoto, kuna matumaini makubwa kuwa utafiti huu utasaidia kuwa hamasisha wanawake katika safari yao ya kujifungua.

Katika mwaka wa 2017, asilimia 35 ya wanawake Australia walifanyiwa upasuaji wa C-section, mojawapo ya idadi kubwa zaidi duniani na zaidi ya mara mbili ya kiwango kinacho shauri na Shirika la Afya Duniani. Katika mwaka huo, zaidi ya asilimia 78 ya wanawake wanao jifungua Australia walitumia matibabu ya kupunguza uchungu.

Hakuna njia sawa ya kujifungua

number of C-sections

Pia, ni muhimu sana kusisitiza kuwa hakuna jambo mbaya na aumuzi wowote ule. Hata kama hakuna sababu ya kimatibabu ya kuhitaji upasuaji wa c-section, huenda ukaamua kujifungua kwa mbinu hiyo na ni sawa. kitu cha mwisho ambacho tunge penda kuanza kufanya ni kuambia wanawake watakavyo fanya na miili yao. Utafiti huu unajaribu kuwasaidia mama kuamini kuwa wana uwezo wa kupitia uchungu wa uzazi, na kuwa sio mbaya kama walivyo dhania hapo awali.

Hilo ndilo jibu tulilo pata kutoka kwa wengi kati ya wamama walio husika walio ripoti kuwa, kubadili mawazo kunaweza fanya tofauti kubwa:

"...ulikuwa nayo akilini mwako waati huu wote kuwa kubanwa ni kuzuri. Hata kama kuna uchungu, kulikuwa kuzuri kwani kulisaidia kujua umbali ulio kuwa unafika," mama mmoja alisema.

Je, kuna njia bora ya kujifungua bila uchungu?

Mojawapo ya mambo ya kutia shaka zaidi katika kujifungua ni kuwa uchungu utakuwa wa kupindukia.

Walakini, wamama wengi walisema kuwa, punde tu kichwa cha mtoto wao kilipo toka kutoka kwa uterasi, uchungu huo wote ulipotea haijalishi njia ya kujifungua uliyo tumia!

Ikiwa hauna uhakika mbinu ya kujifungua iliyo sawa kwako (kujifungua ukiwa nyumbani, asili, ama upasuaji wa c-section) ongea na gynaecologist wako kwanza kuhusu mbinu tofauti na itakayo kufaa zaidi.

Soma Pia:Ulifahamu Kuwa Alama Yako Ya Upasuaji Wa C-section Inaweza Pona?

Written by

Risper Nyakio