Africaparent Logo
Africaparent Logo
EnglishSwahili
  • COVID-19
  • Becoming a Mama
  • Ages & Stages
  • Parenting
  • Health
  • Feeding & Nutrition

Kujifungua Njia Ya Kawaida Ama Kupitia Upasuaji: Gani Ni Chungu Zaidi?

4 min read
Kujifungua Njia Ya Kawaida Ama Kupitia Upasuaji: Gani Ni Chungu Zaidi?Kujifungua Njia Ya Kawaida Ama Kupitia Upasuaji: Gani Ni Chungu Zaidi?

Upasuaji wa c-section una kiasi kidogo cha uchungu ikilinganishwa na kujifungua kwa njia asili. Bado sio dhabiti njia ya kujifungua ambayo wanawake wanapendelea.

Watoto huwasili duniani kwa njia mojawapo kati ya upasuaji wa c-section ama njia ya kawaida. Hata kama kuna uamuzi ambao wanandoa watafanya katika kipindi cha ujauzito, lakini njia ya kujifungua sio mojawapo kati ya hizo. Huo ni uamuzi wa daktari kujua kitakacho mfaa mama na mtoto zaidi. Na kwa hivyo wanandoa wengi wanataka kujua kati ya kujifungua kwa njia ya kawaida na upasuaji, gani ni chungu zaidi?

Ni jambo moja tu linalo athiri uamuzi wa daktari katika kipindi hiki, ambalo ni afya ya mwanamke. Na afya ya mwanamke humjuza daktari kuhusu uamuzi wake iwapo atajifungua kwa njia ya kawaida ama kupitia upasuaji wa c-section. Walakini, kuna wakati ambapo mwanamke hujua kuwa anajifungua kupitia c-section kabla ya siku kuwadia. Pale ambapo ana mimba yenye matatizo.

Kuna hali ambazo zinaweza kumlazimisha daktari kubadili kutoka kujifungua kwa kawaida hadi kwa c-section wakati wa kujifungua. Daktari anaweza fanya c-section ikiwa mtoto ni mkubwa na pelvisi ya mtoto ni ndogo, ama kama uchungu wa uzazi unafanyika pole pole sana. Matatizo mengine ambayo yanaweza fanya daktari afanye uamuzi wa kufanya upasuaji ni ikiwa mtoto anapata hewa kidogo sana.

Kujifungua kwa kawaida na upasuaji ni nini?

Kujifungua Njia Ya Kawaida Ama Kupitia Upasuaji: Gani Ni Chungu Zaidi?

  • C-section ni ya kuwasaidia wanawake ambao kujifungua kwao kumekuwa na matatizo. Kuna husisha kufanya upasuaji kwenye kuta ya tumbo ya mwanamke ili kutoa mtoto. C-section huja na hatari zake.
  • Misuli ya uterasi hubana wakati wa kujifungua kwa kawaida. Misuli husukuma mtoto chini kupitia kwa kanali ya kujifungua, kichwa kikitangulia. Mchakato huu huanza kati ya mfupa wa pelvisi na mfupa wa mkia juu ya kizazi. Kizazi chako hupanuka wakati wa uchungu wa uzazi, na kujinyoosha ili kiweze kutoshea kichwa cha mtoto.

Ni ipi chungu zaidi kati ya kujifungua kwa kawaida na upasuaji?

Kujifungua Njia Ya Kawaida Ama Kupitia Upasuaji: Gani Ni Chungu Zaidi?

Mimba ina mengi ya kufanya na fiziolojia. Kwa wanawake wengi, mimba huhusishwa na uchungu, uwoga, wasiwasi. Uchungu huathiri uwezo wa mtu. Pia una sababisha uwoga na wasiwasi. Hisia zako kuhusu uchungu wa uzazi huhusishwa na fizikia, saikolojia, mazingira na sababu zingine zinazo athiri pakubwa uamuzi kuhusu mbinu ya kujifungua.

Je, upasuaji wa c-section huuma? La hasha, alisema Victoria Handa, profesa wa afya ya kike katika hospitali ya matibabu ya John Hopkins. "Ni upasuaji mkuu, kwa hivyo bila shaka mwanamke atahitaji dawa ya uchungu. Kwa hivyo hasikii uchungu ila ameamka."

Handa alizidi kusema kuwa, wakati ambapo epidural hiyo inapaswa kukufanya usihisi uchungu, hakumaanishi kuwa hauta hisi chochote. "Inalingana, lakini wanawake wanaweza hisi shinikizo ama hisia zingine wakati wa mchakato huo."

Pia, upande ambao mtoto ana angalia uta changia pakuu katika kiwango cha uchungu. Kwa kawaida, mtoto anapaswa kuwa ameangalia chini. Lakini ikiwa mtoto ana angalia juu, huenda ika sababisha uchungu wa uzazi kwa mgongo ama uchungu mwingi wa mgongo. Na kufanya mama asukume zaidi ama kwa muda mrefu.

Unapaswa kuchagua mbinu ipi ya kujifungua?

number of C-sections

Mbinu ya kujifungua huathiriwa na maoni ya mtu binafsi. Maoni haya huwa kufuatia uraibu hapo awali, vyanzo vya habari, ambazo usahihi wake hutofautiana. Mbali na hayo, kwa baadhi ya wanawake, upasuaji wa c-section huonekana kama njia ya kuhepa uchungu wa uzazi. Baadhi yao hufanya uamuzi wa kutumia mbinu hii ya kujifungua.

Hivyo hivyo, masomo mengi yame elezewa sababu nyingi za kuchagua kujifungua kwa njia ya kawaida.

Kulingana na utafiti uliofanyika na Black katika mwaka wa 2005, sababu zinazo wafanya wanawake kuchagua mbinu ya kujifungua kwa kawaida ni kama vile: kupona kwa kasi, uwoga wa dawa za kutuliza uchungu, uraibu chanya hapo awali, kukosa wasiwasi kuhusu jinsi mtoto anavyo endelea.

Kulingana na daktari Allison Bryant, ambaye ni mtaalum wa matibabu ya fetusi, kwa wanawake wengi, kujifungua kupitia kwa uke huhisi kama jambo asili.

Upasuaji wa c-section una kiasi kidogo cha uchungu ikilinganishwa na kujifungua kwa njia asili. Bado sio dhabiti njia ya kujifungua ambayo wanawake wanapendelea. Mbali na hayo, hatimaye uamuzi huwa wa daktari.

Soma Pia:Ulifahamu Kuwa Alama Yako Ya Upasuaji Wa C-section Inaweza Pona?

Got a parenting concern? Read articles or ask away and get instant answers on our app. Download theAsianparent Community on iOS or Android now!

img
Written by

Risper Nyakio

  • Home
  • /
  • Delivery
  • /
  • Kujifungua Njia Ya Kawaida Ama Kupitia Upasuaji: Gani Ni Chungu Zaidi?
Share:
  • Vidokezo Muhimu Vya Kupona Baada Ya Upasuaji Wa C-section

    Vidokezo Muhimu Vya Kupona Baada Ya Upasuaji Wa C-section

  • Mambo 21 Usiyo Paswa Kufanya Baada Ya Upasuaji Wa C-Section

    Mambo 21 Usiyo Paswa Kufanya Baada Ya Upasuaji Wa C-Section

  • Mitindo 5 Ya Ngono Ya Kuepuka Baada Ya Upasuaji Wa C-Section!

    Mitindo 5 Ya Ngono Ya Kuepuka Baada Ya Upasuaji Wa C-Section!

  • Hapa Kuna Manufaa Ya Kujifungua Kwa Njia Asili

    Hapa Kuna Manufaa Ya Kujifungua Kwa Njia Asili

  • Vidokezo Muhimu Vya Kupona Baada Ya Upasuaji Wa C-section

    Vidokezo Muhimu Vya Kupona Baada Ya Upasuaji Wa C-section

  • Mambo 21 Usiyo Paswa Kufanya Baada Ya Upasuaji Wa C-Section

    Mambo 21 Usiyo Paswa Kufanya Baada Ya Upasuaji Wa C-Section

  • Mitindo 5 Ya Ngono Ya Kuepuka Baada Ya Upasuaji Wa C-Section!

    Mitindo 5 Ya Ngono Ya Kuepuka Baada Ya Upasuaji Wa C-Section!

  • Hapa Kuna Manufaa Ya Kujifungua Kwa Njia Asili

    Hapa Kuna Manufaa Ya Kujifungua Kwa Njia Asili

Get advice on your pregnancy and growing baby. Sign up for our newsletter
  • Becoming a Mama
    • Pregnancy
    • Delivery
    • Losing a Baby
  • Ages & Stages
    • Baby
    • Toddler
    • Kids
  • Parenting
    • News
    • Relationship & Sex
    • Parent's Guide
  • Health
    • Allergies & Conditions
    • Vaccinations
    • Diseases-Injuries
  • Feeding & Nutrition
    • Breastfeeding & Formula
    • Latching & Concerns
    • Weaning
  • More
    • TAP Community
    • Advertise With Us
    • Contact Us
    • Become a Contributor


  • Singapore flag Singapore
  • Thailand flag Thailand
  • Indonesia flag Indonesia
  • Philippines flag Philippines
  • Malaysia flag Malaysia
  • Sri-Lanka flag Sri Lanka
  • India flag India
  • Vietnam flag Vietnam
  • Australia flag Australia
  • Japan flag Japan
  • Nigeria flag Nigeria
  • Kenya flag Kenya
© Copyright Africaparent.com 2023 Tickled Media Pte Ltd. All rights reserved
About Us|Team|Privacy Policy|Terms of Use |Sitemap HTML

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it