Hapa Ni Umuhimu Wa Kujifungua Kwa Njia Asili

Hapa Ni Umuhimu Wa Kujifungua Kwa Njia Asili

Kuna majibu machache yanayo kuwa mama anapo taja kuwa anataka kujifungua kwa njia asili… matibabu ya uchungu na kujifungua bila ya kuingilia kati. Kujifungua kwa asili ni chaguo ngumu kwa mwanamke yoyote kufanya na kusifiwa kwa kustahimili uchungu mbaya zaidi maishani bila njia zozote za kuingilia kati, wanawake hutatizika na chaguo lao. “Hakuna taji…” huenda ikawa moja wapo ya maneno ya kuvunja moyo huku wanawake wengi wakichaguo kuenda njia ya asili na kujifungua bila kutumia usaidizi ama madawa yoyote. Huenda wasionyeshe uchungu wao, ila sio taji. “Wow, nimesikia vizuri kweli?” Kujifungua kwa sili sio kwa kila mtu na baadhi ya wanawake hawana chaguo katika jambo hili. Ila, wakati ambapo huenda hakuna taji linalo pewa kwa wanawake wanao jifungua bila usaidizi wowote wa kimatibabu, kuna hatari kwa wanawake ambao huwa na usaidizi wakati wa kujifungua.

  • Induction

Induction ni njia mojawapo kuu zinazo kuja kati ya mama na kujifungua kwa asili. Wanawake wengi hawana chaguo lingine katika jambo hili. Mambo kama fetal distress ama utatizika kwa kiinitete na shinikizo la damu na kadhalika yana hitaji inductio kwa usalama wa mama na mtoto. Kuna muda ambapo inductio haihitajiki. Mambo kama vile kukawia sio sababu shwari kufanya mama apate induction. Walakini, siku unayo tarajiwa kujifungua ni kufikiria tu. Watoto wengi huenda wakawa hawako tayari kuja bado katika siku yao wanayo tarajiwa. Iwapo mama na mtoto wote hawako tayari kwa uchungu wa mama na kujifungua, huenda changamoto ama matatizo yaka tokea. Wanawake wengi huenda wakawa wameambiwa kuwa induction inahitajika kufuatia kuwa na mtoto mkubwa, na baadaye kujifungua mtoto mdogo kuliko walivyo tarajia. Inductions huenda zika sababisha matatizo ambayo hayakukusudiwa hapo awali kama matibabu ya uchungu, kutumia forceps ama hata c-section katika kesi zingine. Kujifungua kwa asili huenda bila shaka kukaleta matukio sawa ila katika vipindi vichache zaidi.

Minus the risk during pregnancy

Minus the risk during pregnancy

  • Daktari akivunja maji

Katika kitabu cha ujauzito, maji ya mama huenda yakavunjika wakati mfupi baada ya uchungu wa uzazi kuanza ambako kutaharakisha mchakato huo. Baadhi ya wakati (ama wakati mwingi) mambo hayafuati kitabu. Madaktari watavunja gunia la maji la mama kwa sababu mbili; kuanzisha uchungu wa uzazi ama ili kuharakisha mchakato huu. Wakati daktari huvunja gunia la maji yeye mwenyewe ili kuanzisha uchungu wa mama ama kuuharakisha, huenda hatari zikatokea. Huenda mambo yakatokeo kama ilivyo kusudiwa, ila pia huenda kwa urahisi ikaishia kwa upasuaji wa c-section. Hii ni kwa sababu mara maji yanapo vunja, mwanamke hana wakati mwingi kabla ya kujifungua kabla ya hatari za maambukizi kuwa juu. Madaktari kwa ujumla wanakupatia kipindi cha wakati cha kujifungua baada ya kuvunja maji kabla ya upasuaji wa c-section kufanyika. Wanawake wengi huvunjwa maji yao na madaktari bila ya changamoto zozote, ila iwapo sio kwa mtoto mwenye afya ama mama, mbona usikubalishe dunia ifanye mambo yake na ungoje gunia la maji lijipasue?

doctor breaking water

  • Epidural

Kwa wanawake wengi, epidural ndiyo huwa hiar njema zaidi ya kujifungua. Epidurals hasa ni njema kwa mama ambaye ameshuhudia uchungu wa uzazi kwa muda mrefu na anahitaji kupumzika ili aendelee. Pia, epidural inaweza tuliza mama aliye na wasi wasi mwingi na kusaidia uchungu wa uzazi kuzidi kasi katika visa na mama aliye pumzika. Walakini, njia hii ya kujifungua inakuja na bei yake wakati mwingi. Wasiwasi mwingi zaidi kwa wanawake wengi wanao fikiria kutumia epidural ni uwoga wa upasuaji wa c-section bila shaka. Bila shaka mama wa epidural, baada ya utafiti mwingi, hakuna jibu shwari ya ndiyo ama la iwapo epidural inafuatiwa na c-section. Hata kama uwoga wa c-section unaonekana hauna misingi, kuna hatari ongezeka zinazo anzishwa na epidural ambazo kwa kifupi haziko unapo jifungua kwa njia asili.

  • Dawa zingine

Wakati ambapo epidural ndiyo huenda ikawa inatumika kwa sana (ama angalau inajulikana sana) matibabu ya kutatizika wakati wa uchungu wa uzazi, kuna hiari zingine zilizoko kwa mama walio katika uchungu wa uzazi. Kuna tap ya uti wa mgongo (spinal tap), narcotics, local anaesthetic pudendal block, tranquillizers na nitrous oxide. Tena, matibabu haya yote huwa na nafasi yake katika uchungu wa uzazi ila kuna hatari zinazo husika. Hii sio kusema kuwa vitu haziendi mrama na kujifungua kwa asili kwa sababu bila shaka, jambo hili hutendeka. Walakini, kadri moja anavyo zidi kukaa mbali na kujifungua kwa asili, ndivyo hatari za jambo hukaribika zinavyo zidi.

kujifungua kwa njia asili

Picha: Shutterstock

Upasuaji wa C-Section
Kufuatia sababu za kawaida, wamama wengi hawachagui kujifungua kupitia upasuaji wa C-section. Kwa ujumla, upasuaji huu unafanywa kwa sababu za kimatibabu katika visa vya dharura pale ambapo usalama wa mama ama wa mtoto ama wote wako hatarini. Upasuaji wa C-section huenda ukawa ni matokeo tofauti kabisa na kujifungua kwa njia asili, ila hatari za kuwa na upasuaji wa C-section ili kujifungua huongezeka na kila mbinu inayo tumika. C-sections huwa salama kwa mama na mtoto ila huenda yakawa na matatizo kwani ni upasuaji mkuu. Upasuaji wote mkubwa huja na hatari zake. Pia, watoto wanao zaliwa kufuatia c-section baadhi ya wakati huwa na matatizo ya kupumua. Wakati ambapo mtoto anazaliwa kwa canali ya kujifungua, kubanwa husababisha maji kutoka kwenye mafua na kuimarisha uwezo wake wa kupumua. Mtoto anapo zaliwa kufuatia c-section, anakosa kupitia hatua hii muhimu. Tatizo la mwisho na kujifungua kupitia c-section ni kuwa ujauzito wa usoni na uchungu wa uzazi utakuwa na changamoto. Baadhi ya madaktaru wanashauri usiwe na c-section zaidi ya mbili. Iwapo mama anakusudia kuwa na familia kubwa, huenda akahitaji kuchukua hatua zote muhimu kuhakikisha kuwa ana epuka kujifungua kupitia c-section.

Matukio ya mwisho

Kila mwanamke ni tofauti, kila mwanamke hukabiliana na uchungu wa uzazi vitofauti na kujifungua vitofauti na kila mwanamke ana hadithi tofauti ya kusimulia. Hayo yakiwa yamesemwa, kuna kitu cha kusisimua kuhusu kujifungua bila ya usaidizi wowote. Kujua kuwa mtoto wako alikuja ulimwenguni bila kitu chochote ila mwili wako ni cha kupendeza. Walakini, miezi miwili baada ya kujifungua, haitajalisha iwapo ulitumia matibabu ya uchungu, maji yako yalivunjika, kwa kutumia dawa, ulipata upasuaji wa C-section ama hata kujifungua kwa njia ya asili. Mwishowe, kitu cha muhimu ni kuwa sisi wote tutakuwa na watoto. Wao ni zawadi zetu na sisi wote huwapata haijalishi njia tunayo itumia.

Christy Rasmussen ni mamake preschooler mmoja aliye mzito #na mtoto anayekusudiwa kuwasili Disemba 2. Ana digrii katika Biashara na Sayansi ya Kisiasa/Serikali, ila aligundua kwamba mapenzi yake ya kuandika baada ya kuanza kurasa ya kujifurahisha kuhusu shuhuda za ulezi.

Hapa ni baadhi ya makala yanayo husika na ujauzito:

Soma Pia: The Way We Think About Labour Might Change How We Feel It

Makala haya yalichapishwa tena na idhini ya theAsianparent kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio