Vidokezo 9 Vya Siri Vya Kujifungua Kwa Wepesi

Vidokezo 9 Vya Siri Vya Kujifungua Kwa Wepesi

Watch the video and prepare to be surprised...

Tutanapo zungumza kuhusu kujifungua kwa wepesi, kina mama wote hutaka liwe jambo la haraka lisilo kuwa na uchungu mwingi. Kina mama wengine huwa na bahati kwani hupatwa na uchungu wa uzazi kwa dakika chache tu lakini kwa kina mama wapya, kujifungua kwa mara ya kwanza kunaweza kuwa jambo la kuogopesha.  Haisaidii kuwa utasoma hadithi nyingi juu ya uchungu wa uzazi wa muda mrefu na vile huwa na uchungu mwingi. Lakini sio lazima iwe hivyo. Tizama vidokezo hivi jinsi ya kijifungua kwa wepesi.

Vidokezo 9 Vya Siri Vya Kujifungua Kwa Wepesi

Filamu hii inaonyesha mchakato wa uzazi wa wepesi

Tulipata filamu ya dakika tatu iliyohusu kujifungua kwa wepesi huku California, USA.  Huu waweza kuwa wakati wa wepesi mno wa kujifungua kwa kawaida – ilichukua kama sekunde 30 kwa mama kujifungua baada ya kusukuma kwa kwanza.

Mama aliyefahamika kwa jina Monica Diaz alitoa maoni yake kwa mtandoa kwamba hii ilikuwa mara yake ya kwanza kujifungua kwa wepesi ikilinganishwa na mara mbili za hapo awali. Hakupatwa na kupasuka kwa hivyo hakuhitaji kushonwa.

Jinsi ya kujifungua kwa wepesi: Njia 9 za siri za kuharakisha kujifungua mtoto

Kina mama pia mwaweza pata uchungu wa wepesi kama Monica. Hizi ni njia tisa za siri ambazo unaweza kufanya ili kujifungua kwa wepesi.

  1. Dumisha afya bora
mama anaye karibia kujifungua

Tekoa King ni mkunga aliyefuzu na profesa wa maswala ya ukunga kutoka chuo kikuu cha California, San Francisco (UCSF). Kulingana naye, kina mama ambao hudumisha afya bora huwa na wakati mwepesi wa kujifungua.

“Hali nzuri ya afya huongeza ustahimilivu.  Iwapo mwili wako una uwezo wa kustahimili  uchungu wa uzazi  hautahitaji usaidizi wa huduma za kitabibu,”  Tekoa alisema.

Jaribu kutembea kwa wingi, kuogelea ama mazoezi ya ujauzito.  Lakini usisahau kushauriana na mkunga wako au daktari wa maswala ya ukunga kwanza kwani kila mama ni tofauti.

2. Hudhuria darasa la kujifungua

Kuzoea madarasa ya kujifungua kutasaidia kupunguza hofu kwako mama.  Jaribu kutafuta darasa lililoko karibu na unapoishi na umlete bwanako pia.

Chagua darasa lililo na watu wachache na wahudumu waliohitimu wanaolenga nia zako.

3. Amua ni kina nani watakao kuwa wakutegemea

Bwanako bila shaka atakuwa kwa upande wako kabla ya kujifungua hadi wakati baada ya kujaliwa na mtoto akisaidia kwa mahitaji ya baadae. Lakini labda utahitaji msaada wa ziada.

Kulingana na matokeo ya uchunguzi katika jarida la Perinatal Education wanawake wajawazito waliopata usaidizi wa doulas (hudumu aliyehitimu anayewasaidia wanawake wajawazito mpaka wanapojifungua watoto) walikuwa na upungufu wa kuhitaji upasuaji na epidurals.

Wanawake wajawazito waliosaidiwa na doula pia walipatwa na uchungu wa uzazi wa muda mfupi ikilinganishwa na wale hawakuwa naye. Ingawaje, sio lazima kina mama kuhusisha huduma za doula.

Mifano mingine ya usaidizi ni kama vile kuchagua daktari wa maswala ya ukunga, hospitali nzuri ama mtu atakaye wasaidia wewe na bwanako kumlea mtoto baadaye.

4. Kazia fikra zako kwa jambo lingine

Kwa kina mama wanaojifungua kwa mara ya kwanza, uzalishaji waweza kuchukua masaa 12 hadi 14.  Kwa hivyo kubanwa kunapoanza jaribu kuwa mtulivu. Iwapo utahisi hofu jaribu kuhesabu kila wakati unahisi kubanwa na pumua kwa nguvu kila wakati unapohisi uchungu. Kazia fikra zako kwa mambo mengine kama kutembea, kuoga au kuoka keki.

Kile ambacho kitakufanya upumzike kitasaidia kujifungua kwa wepesi.

5. Chagua chakula chepesi

kujifungua kwa urahisi

How to give birth easily: eat a light snack before entering labour so you’ll have enough energy to push, mums! | Image Source: Stock Photo

Kula chakula chepesi wakati uchungu wa uzazi unapoanza ukiwa nyumbani itakupa nguvu inayohitajika kina mama kujifungua. Jiepushe na chakula kilicho na mafuta nyingi na kilicho na ugumu kusaga kwani tumbo liliojaa laweza sababisha utapike ama uende choo kubanwa kunapozidi.

Kubana kwa misuli na kupumua kwa wepesi kutakufanya upoteza maji nyingi kina mama. Kwa hivyo kunywa maji nyingi kabla ya uchungu wa uzazi kuanza kutakufanya kujifungua kwa wepesi.

6. Oga kwa maji vuguvugu

Uchungu kutokana na kubanwa  kutafanya mwili kupindana  na baadaye utahisi kuchugachuga. Daktari Marcie Richardson, daktari wa maswala ya ukunga kutoka hospitali ya Harvard Vanguard Medical Associates asema kuwa kuoga na maji vuguvugu kunaweza kupunguza maumivu.

Ili kuhisi kama unakandwa, kielekeze kichwa cha shower kwenye mgongo na kiuno chako.

7. Uliza bwanako akukande

Kulingana na utafiti uliochapishwa kwenye jarida la Experts Reviews of Gynecology na Obstretics, kina mama wajawazito waliokandwa kabla ya kupatwa na uchungu wa uzazi walipata uchungu uliopunguka na wasiwasi mdogo wakilinganishwa na wale hawakupata.

Mwambie mume wako mahali atakapokusugua kama vile mabega na shingo wakati kubanwa kutakapoanza.  Alafu tilia mkazo kwa mgongo wa chini kubanwa kunapozidi.

Kina mama pia msisahau kuwaambia waume wenu ile wakati hautaki kusuguliwa.

8. Usilale chini

Kukaa ukiwa  wima wakati kubanwa kunapoanza kutawezesha mvuto wa graviti kukusaidia baadaye. Hii ni kwa sababu kichwa cha mtoto wako kitatilia mkazo mlango wa tumbo la uzazi wako uufanye ufunguke kidogo.

Jaribu kukaa vingine kama vile kusimama, kupiga magoti, kuchuchuma ambazo hupunguza kuhisi vimbaya  na husaidia kujifungua kwa wepesi.

9. Endelea kupumua kwa kawaida

Kupumua kwa kawaida kutakusaidia kuangazia kubanwa kunapo anza na kukutuliza. Kabla ya uchungu wa uzazi kuanza kuwa na mbinu ya kupumzika akilini. Kwa mfano unaweza anza kwa kupumua kwa undani, kuwaza mahali pazuri ama kusikiza muziki.

Kina mama, ni matarajio yetu kuwa haya makala ya kujifungua kwa wepesi imewasaidia. Iwapo umekuwa na kujifungua kwa wepesi kuwa huru kuongea nasi kwenye nafasi ya maoni hapa chini.

Also Read: Causes of death in childbirth

Written by

Risper Nyakio