Ushuhuda Wa Kibinafsi Wa Kujifungua Katika Janga Hili La Corona

Ushuhuda Wa Kibinafsi Wa Kujifungua Katika Janga Hili La Corona

Kuzaliwa kwa mtoto ni kugumu katika pande zote, kiafya na ki fedha. Kuishi katika lockdown katika janga hili ni jambo gumu, kifedha na pia ki sykologia. Hivi sasa, mamia ya maelfu ya wanawake wajawazito wanajitayarisha kufanya  vitu hivi viwili. Kama inavyo tarajiwa, kuna wanawake wajawazito ulimwengu kote ambao huenda waka shuhudia kujifungua wakiwa nyumbani katika janga hili la homa ya corona.

Na hasa, isha anza. Mwanamke alijifungua mtoto wa kike mwenye afya alipokuwa katika kuarantini na akawajulisha wengine kuhusu habari hizi kwa kupitia mitandao ya kijamii. Dakika chache baada ya kujifungua. Mitandao ya kijamii walikuwa na hisia tofauti kwa kisa hiki, huku wengine wakim pongeza kwa kujifungua vyema.

Mama wa hivi sasa kutoka Motta Sant'Anastasia huko Italy, kulingana na mtandao wake wa Twitter.

Wakati ambapo watu wengi hawakujua cha kufanya walipokuwa katika kuarantini katika janga hili la homa ya corona; tunaweza mpongeza mama huyu kwa kujifungua kwenye kiti chake alipokuwa amejitenga.

Kujifungua Nyumbani Katika Janga La Corona Kwenye Kiti! Ni Salama Kweli?

giving birth during pandemic

Mwanamke huyu, BrittyPinon aliwaonyesha watu wakati wa maana kwa kuweka picha yake na mtoto wake muda mchache baada ya kujifungua kwenye kiti.

Watumiaji wa mitandao ya kijamii walikuwa na hisia tofauti kuhusu mama huyu kujifungua katika kuarantini. Huku wengine wakimpongeza, wengine walimshauri kumwita mwanawe Quarantina.

Mtumiaji mwingine wa twitter @another_vic alisema: "Huku ujauzito ukiendelea vyema, kuna usalama zaidi kujifungua ukiwa nyumbani... hasa wakati ambapo mahospitali yana kazi nyingi zaidi kwa sababu ya janga hili."

Kuna uwezekano mkubwa na mmoja wa kujitayarisha iwapo una mimba katika wakati huu. Wakati kabla kuwa na mahospitali ya kujifungua (ama hata kabla ya hospitali kuanzia), wanawake walikuwa wanajifungua wakiwa nyumbani. Manyumba ya kisasa ni salama kujifungua hasa iwapo wamama wanao tarajia wana msaada na kama wamejitayarisha ipasavyo.

Je, Kujifungulia Nyumbani Ni Hiari Njema Ya Kujifungua Katika Janga Hili La Corona?

Giving Birth During The Coronavirus Pandemic

Kuna swali ya mahali pa kujifungulia katika janga hili hatari la corona ambapo hospitali zitakuwa na wagonjwa wengi ambao huenda wakasambaza maradhi haya. Janga hili la corona lina nyoosha kwa kiasi kikubwa mfumo wa utunzaji wa afya nchini. Hospitali nyingi haziko tayari kutibu wanawake walio wagonjwa wanao jifungua. Wataalum wa afya kama vile Chuo Kikuu cha Umerikani cha wataalum wa afya ya kike (ACOG) hawafikirii kuna jambo la kukutia wosia; iwapo hospitali unayo itumia ni nzuri. Ila kukiwa n uwingi wa maradhi haya huwezi kosa kuwa na fikira nyingi.

Hiyo ndiyo sababu kwa nini sio jambo jipya kwa wanawake wajawazito kuwa na mawazo ya kujifungulia nyumbani; hasa wanawake walio na mimba isiyo ya hatari. Ila mama kuwa na upasuaji wa C-section kwa mfano hawana hiari katika jambo hili. Pia, kituo cha American College of Nurse-Midwives (ACNM), kinasema kwamba iwapo uko katika hatari ya chini na hujachukua matayarisho yanayofaa, kujifungulia nyumbani huenda kukawa wazo nzuri mbadala ya kujifungulia kwenye hospitali. Iwapo una wazo la kupatia mtoto wako nyumbani, hapa kuna vitu vichache ambavyo unapaswa kuangalia; na kuweka kwenye mawazo yako. Tuna yaangazia hapa chini:

Mambo ya kutia akilini kuhusu kujifungulia nyumbani katika janga hili la homa ya corona

  • Unapaswa kuwa na mkunga na mwuguzi atakaye angazia mchakato wako wa kujifungua
  • Kuwa na njia za kukusafirisha hadi kwa hospitali iliyo karibu iwapo kutakuwa na jambo la dharura
  • Punguza nambari ya wageni kwenye nyumba yako wakati wa ujauzito wako, hasa yeyote aliye tembea.
  • Hakikisha kuwa anaye kupatia utunzaji wa afya anaendelea kuchukua tahadhari zinazo faa kukuweka salama kutoka kuwa wazi na kuendelea kufanya mambo kama kawaida.

Pia, ni muhimu kuweka akilini kuwa unapaswa kutulia na kuwa na baadhi ya vitu nyumbani, iwapo kutokee jambo lolote.

home birth during coronavirus pandemic

Vitu hivi ni kama vile vifaa vya kuosha ambavyo vina hakikisha nyumba yako ni safi ipasavyo, hasa kwenye pande ambayo utajifungulia. Safisha kila mahali, na iwapo una watoto, hakikisha kuwa wana nawa mikono kwa mazoea baada ya kufika nyumbani kutoka shuleni ama baada ya kucheza iwapo wako nyumbani.

Kama ni vitu ambavyo utahitaji, utahitajika kuongea na daktari wako. Wanapaswa kukupatia ushauri wa kibinafsi ya vitu utakavyo hitaji.

Ungechagua kujifungulia nyumbani ama kujifungua kwenye maji katika janga hili la COVID-19? Je, hizo ni hiari kwako?

WhatToExpect Tuko Kenya

Soma pia: Here's Everything You Need To Know About Coronavirus And Pregnancy

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Ayeesha kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio