Sababu Za Mtoto Kujigonga Kichwa Kwa Kutumia Mikono

Sababu Za Mtoto Kujigonga Kichwa Kwa Kutumia Mikono

Mara nyingi wamama huwa na shaka nyingi wanapo waona watoto wao wakijigonga vichwa kwa kutumia mikono. Kuna sababu nyingi zinazo sababisha tabia hii.

Huenda likawa ni jambo la kuhuzunisha kuona mtoto wako akijigonga kichwa kwa mkono. Huenda pia likakutia shaka iwapo ni jambo jipya kwako. Huenda likakuwacha na maswali mengi, bila imani na huku ukimwangalia mtoto wako kuona iwapo kuna kitu kimeenda mrama. Na sio kama watoto wanaweza sema ama kukuelezea kinacho wafanya wakose starehe. Baadhi ya wakati, huenda ni yote ambayo mtoto wako anaweza fanya - kujigonga kichwa kwa mkono. Na kukuacha ukishangaa: kwa nini mtoto wangu hukaa akijigonga kichwa kwa mkono?

Mbinu hii ya kujigonga kwa mkono ni kawaida kwa watoto. Sio kwa mtoto wako tu. Kiran Pure, ambaye ni mwana psykolojia wa watoto aliye sajili huko Halifax, aligundua kuwa "Iwapo huenda likakaa jambo la kushtua kwa wazazi, tabia hii ni kawaida sana - karibu robo ya watoto wadogo watajipiga kwenye uso ama kichwa mara kwa mara. Kujigonga kichwa kwa mara nyingi huanza baada ya umri wa miezi sita na kuwa katika kilele kati ya miezi ya 18 - 24," alisema.

Watoto wanapokuwa wakipitia maendeleo ya kasi ya kiakili ndipo tabia hii inapokuwa katika kilele chake. Mara nyingi katika miezi ya 18-24. Na watoto wengi huacha wanapokuwa miaka mitatu ama mapema.

Tabia Ya Kujigonga Kichwa Kwa Mkono: Kwa Nini Mtoto Wako Hushinda Akijigonga Kichwa? Why Does My Baby Keep Hitting His Head With His Hand?

Bila shaka watoto hawaongei. Kwa hivyo, huenda ikawa ni wao wanajaribu kukuongelesha kuhusu jambo fulani. Hapa kuna baadhi ya vitu ambavyo huenda wakawa wanajaribu kusema wanapo gonga vichwa vyao.

  • Mtoto wako anataka kupumzika

Kujipiga ili kujituliza - nani hufanya kitendo kama hiki? Watoto. Wengi wao hufanya hivi ili wajitulize wenyewe. Baadhi ya wataalum wa maendeleo wana amini kuwa kusonga kwa mpigo fulani kunasaidia mtoto kupumzika. Kujigongesha huku kwenye mpigo hufanyika wanapo amka kati kati ya usiku ama wanapo lala.

  • Huenda mtoto wako akawa amefadhaika

Hata kwa watu wazima kukabiliana na mafadhaiko huenda kukawa na hisia nyingi. Unapo mwona mtoto wako akijigonga, huenda ikawa ana jaribu kujituliza. Kwa sababu hajajua jinsi ya kujieleza kwa kutumia maneno bado, kwa hivyo anatumia matendo ya kifizikia. Huenda pia akawa anafanya hivi kama njia ya kujituliza katika nyakati hizi.

  • Mtoto wako anataka uangalifu wako

Makini kidogo huenda ikawa ndiyo mtoto wako anahitaji anapojigonga kichwani. Ni kawaida kwako kumkaribia mtoto wako anapo onekana kuwa anafanya kitu cha kujidhuru. Kwa hivyo mtoto wako huenda akaendelea kujigonga ili umpatie uangalifu anaotaka.

  • Tabia ya kujigonga kichwa kwa mkono: Huenda mtoto wako ana jituliza uchungu

Mtoto wako kujigonga huenda kukawa kwa sababu anataka kujituliza uchungu. Huenda ikawa ana maambukizi ya sikio ama ana mea meno. Kujigonga huku huenda kukawa ni njia ya kutoa akili yake mbali na uchungu wa kumea meno ama maambukizi ya sikio.

  • Bila maana

Wakati mwingine, huenda ikawa mtoto wako anajigonga kwa sababu anaweza. Kwa hivyo anajigonga. Ni kama kuwa na uthibiti wa mwili wake kwa njia fulani, na kunamsisimua na kumburudisha.

Jinsi ya kukabiliana na tabia ya mtoto wako ya mkono kugonja kichwa

baby

Huenda ikawa vigumu kujua njia hasa ya kutuliza watoto wanapo jifanyia madhara. Ili kuhakikisha wako salama, hapa ni vitu vichache vya kufanya.

  • Usaidizi wa kifizikia: Watoto wanapokuwa na tabia ya kujigonga wenyewe, unaweza wakaribia na kuziba pigo hilo kwa kutumia mkono wako. Huenda kukasaidia kumtuliza mtoto wako kwa muda mfupi.
  • Mazingara salama: Iwapo mtoto wako ana tabia ya kugongesha kichwa chake kwenye kitu chochote nyumbani, toa kifaa hicho na ukiweke mbali.
  • Maneno ya kutuliza: Waongeleshe maneno ya kuwatuliza. Wajulishe kuwa wako salama. Unaweza wapatia kitu cha kuwatuliza kama vile vijidolivya kushikilia.

Mbinu ya kudumu zaidi: Cha kufanya

Why Does My Baby Keep Hitting His Head With His Hand

Mbinu ya kudumu zaidi ya kusaidia watoto wanao jigonga wenyewe ni kuanza kuwasaidia kufahamu na kuweka hisia zao kuwa maneno. Kwa mfano, iwapo unahisi kana kwamba umekasirika, waambie kinaga ubaga unacho hisi. Unaweza sema jambo kama. "Naona kuwa umekasirika." Kujua kuwa unazifahamu hisia zao kunasaidia kupunguza tabia za kujidhuru. Pia, kuwafunza jinsi ya kujieleza kwa maneno kutawasaidia kukabiliana na hasira zao katika siku za usoni.

Walakini, iwapo mtoto wako ataendeleza tabia ya mkono kugonga kichwa, huenda ikawa ni ishara ya jambo la ndani zaidi. Baadhi ya wakati, tabia hii huhusishwa na usonji, kwa kimombo ni autism. Watoto walio na usonji na ulemavu wa maendeleo hutumia kujidhuru kama njia ya kujituliza. Unapaswa kuwasiliana na mtaalum.

Soma pia: Baby sweats while sleeping? Here’s what you need to know

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Lydia Ume kisha yakatafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio