Msimu wa baridi nchini huanza mwezi wa sita, saba hadi Agosti. Kujikinga dhidi ya baridi huwa muhimu katika miezi hii ili kujilinda dhidi ya kupata magonjwa.
Wakenya nchini kote wamekuwa wakiteta kuhusu baridi isiyo isha. Msimu wa baridi huandamana na changamoto zake. Tofauti na hapo awali ambapo utawapata watu wengi nje wakifanya shughuli bila kujali kuhusu hali ya anga. Katika msimu huu, watu wengi huwa ndani, ya manyumba ama maofisi zao. Mavazi wanayoyavalia huwa wamedhibitiwa. Lazima yaye mazito yenye joto, tofauti na siku zingine ambapo wanachagua kuvalia mavazi mepesi.
Je, umenunua sweta na soksi?
Tuna angazia siri za kukabiliana na baridi Nairobi katika msimu huu wa baridi.
Jinsi ya kujikinga dhidi ya baridi na kuhakikisha una joto katika msimu wa baridi
Sio kawaida kutoka nje saa nane mchana na kupata kuwa kunakaa kana kwamba kungali asubuhi. Lakini hii ndiyo imekuwa hali yetu kwa miezi michache sasa. Je, tutakabiliana vipi na hali hii na kuhakikisha kuwa tunapata joto na kujilinda dhidi ya baridi na magonjwa?
- Vali mavazi yenye joto

Huu sio wakati wa kuvalia blausi nyepesi na kaptura. Hakikisha una sweta nzito. Zinalinda dhidi ya kuhisi baridi na kuhifadhi joto mwilini. Ongeza skafu kwa mavazi yako. Inalinda sehemu ya shingo kutopata baridi na kukupa joto zaidi.
2. Tumia kifaa cha joto ama heater
Kifaa hiki kinasaidia nyumba ama ofisi yako kuwa na joto. Usihisi kana kwamba uko ndani ya jokofu.
3. Pasha chakula na vinywaji joto

Kula ama kunywa vinywaji na vyakula baridi hakushauriwi katika msimu huu. Badala yake, hakikisha kuwa wakati wote unakula vyakula na vinywaji moto. Kwa wanaopenda chai, hakikisha unainywa mara kwa mara, itaupa mwili joto zaidi. Kula mara kwa mara, kunaupa mwili joto baada ya chakula kuchakatwa mwilini.
4. Valia soksi
Unapokuwa ndani ya nyumba, valia soksi kukupatia joto. Epuka kuvalia viatu wazi unapokuwa nje.
5. Fanya mazoezi

Unapofanya mazoezi, mwili unatoa joto na kuhimiza damu kuzunguka mwilini ipasavyo. Epuka kukaa mahali pamoja kwa muda mrefu bila kufanya lolote.
Baridi inahusishwa na magonjwa ya mfumo wa kupumua kama vile; homa, kukohoa, asthma na pneumonia. Hakikisha kuwa unajilinda na kuwalinda wapendwa wako.
Je, una vidokezo zaidi kuhusu jinsi ya kuhakikisha unapata joto katika msimu huu wa baridi? Tujuze kwa kuwacha ujumbe mfupi.
Chanzo: Africaparent
Soma Pia: Jinsi ya Kutumia Kondomu ya Kiume