Kwa Nini Una Hisi Kujikuna Miguu Katika Ujauzito?

Kwa Nini Una Hisi Kujikuna Miguu Katika Ujauzito?

Ukihisi kujikuna kwa sana, hakikisha kuwa una enda hospitalini ili uweze kufanyiwa vipimo vinavyo faa kudhibitisha iwapo una hali ya OC.

Kuhisi kujikuna kwingi katika ujauzito ni kawaida na sio chanzo cha kuwa na shaka. Ila kujikuna sana huenda kukawa ishara ya tatizo la maini linalo julikana kama Intrahepatic Cholestasis of Pregnancy (ICP) ama hali inayo fahamika kama Obstetric Cholestasis (OC). Makala haya yana angazia kwa undani hali hizi na kujikuna miguu katika ujauzito.

Kujikuna kidogo

mimba ukiwa na uzito mwingi

Kuvalia mavazi mapana huenda kukasaidia katika kujikinga dhidi ya kujikuna, kwani kuna nafasi ndogo ya mavazi yako kugusa ngozi yako na kusababisha kukosa starehe. Huenda pia ukahitaji kujitenga na mavazi ya synthetic, na badala yake uvalie mavazi ya pamba yanayo kubalisha mzunguko wa hewa kwenye ngozi yako. Kuoga kwa maji ya vuguvugu na kujipaka mafuta kuna saidia kupunguza kujikuna.

Baadhi ya wanawake hugundua kuwa, bidhaa zilizo na harufu kali zinaweza kufanya ngozi ikose starehe, kwa hivyo ni vyema kutumia sabuni peke yake na mafuta yasiyo na harufu. Kujikuna kidogo hakuna athari hasi kwako wala kwa mtoto wako, ila huenda kuka ashiria hali sugu zaidi. Ikiwa una shaka, ama una jikuna sana, ni muhimu kuwasiliana na daktari ama mkunga wako.

Hali ya Obstestric Cholestasis ni nini?

kujikuna miguu katika ujauzito

Hii ni hali ya maini inayo athiri mzunguko wa bile mwilini unapo kuwa mjamzito. Chumvi ya bila huzunguka mwilini kwa ujumla kutoka kwa maini hadi kwenye mfumo wa kuchakata chakula na kusaidia na utaratibu wa uchakataji chakula. Hali ya OC ina athiri mzunguko wa bile na kusababisha viwango vyake kuongezeka mwilini. Kama athari yake, una anza kuhisi kujikuna mwili, hata kama kwa baadhi ya wanawake, kujikuna huwa kwenye sehemu ya mikono na miguu peke yake.

Kujikuna kwa aina hii huenda kukaongezeka usiku lakini haku andamani na upele. Ishara zingine ni kama vile mkojo mweusi, kupitisha kinyesi cha gray na jaundice ambapo ngozi hugeuka kuwa ya kinjano na macho meupe.

Mara nyingi, hali hii huhudhuriwa katika trimesta ya kwanza, hata ingawa inaweza anzia mapema. Habari nzuri ni kuwa kwa ujumla, hupungua siku chache baada ya kujifungua.

Jinsi ya kutibu hali ya kujikuna miguu katika ujauzito

Unapo shuhudia kujikuna katika ujauzito, kuna hatua nyingi asili unazo weza kuchukua kupunguza ishara hizi.

  • Kujipaka mafuta yasiyo na harufu
  • Valia mavazi yasiyo kubana
  • Kuvalia mavazi ya fiber asili kama vile pamba

Ukihisi kujikuna kwa sana, hakikisha kuwa una enda hospitalini ili uweze kufanyiwa vipimo vinavyo faa kudhibitisha iwapo una hali ya OC. Hata kama hakuna tiba ya OC, kuna hatua za kupunguza ishara zake ikiwemo kuoga kwa maji ya vuguvugu, ama kuwekelea tembe za barafu kwenye sehemu unayo hisi kujikuna.

Soma Pia: Mwongozo Wa Wiki Ya 33 Ya Ujauzito: Yote Unayo Paswa Kujua

Written by

Risper Nyakio