Sababu 6 Kwanini Kujisaidia Mara Ya Kwanza Baada Ya Kujifungua Kuna Uchungu!

Sababu 6 Kwanini Kujisaidia Mara Ya Kwanza Baada Ya Kujifungua Kuna Uchungu!

Wamama wengi walio jifungua wanakubaliana kuwa kujisaidia baada ya kujifungua kuna uchungu! Nini sababu?

Kwa miezi tisa iliyopelekea kwako kujifungua, kina mama watarajiwa hujihimiza wakijua kuwa baada ya safari yao ya ujauzito, lazima watastahimili uchungu na uchovu unaotokana na kumleta mtoto duiani.

Mara tu wanapomaliza kipindi cha uchungu wa uzazi na kujifungua, wao huwezi kupumua heri lakini ngoja kwanza….kuna zaidi. Lazima wakiuke changamoto ingine: kujisaidia baada ya kujifungua kwa mara ya kwanza. Kina mama wengi wanaweza kuitikia kuwa kujisaidia kwa mara ya kwanza baada ya kujifungua kunaweza kuwa uchungu sana, ata zaidi ya uchungu wa uzazi ama kujifungua.

Chanzo ni nini haswa?

Hizi ni sababu sita kwa nini kujisaidia kwa mara ya kwanza baada ya kujifungua huwa kwa uchungu

They have likely been constipated for days

Picha: Shutterstock

  • Kuna uwezekano wamekuwa wamevimbiwa tumbo kwa siku nyingi

Baada ya kujifungua, itachukua muda kwa mwili wako kupona na kurejea mambo yake ya kawaida ikiwemo kimetaboliki na ufupisho wa chakula. Kunywa dawa na kuwa na upungufu wa maji mwilini pia huchangia kuvimbiwa na tumbo baada ya kujifungua.

Kwa kina mama waliojifungua kwa kupitia upasuaji, kuvimbiwa  tumbo kunaweza kuwa shida kubwa, haswa dawa ya kugandishwa inapoisha.

  • Kuna uwezekano walipuuza dawa za kulegeza choo

Umuhimu wa dawa za kulegeza choo baada ya kujifungua huchukuliwa kwa urahisi, lakini zinaweza kusaidia pakubwa wakati wa kujisaidia

  • Wanaweza kuwa waliraruka kwenye uke

Kina mama wengi ambao hujifungua kwa hali ya kawaida, lazima wapitie episiotomy ama kukatwa hilo eneo kati ya uke na mkundu ili kupanua njia ya uzazi. Kuraruka kwa uke na perineum inaweza kufanyika pia wakati wa uchungu wa uzazi.

use stool softeners

  • Wanaweza kuwa na uvimbe

Ata kama hakuweza kuraruka kwenye uke, mama bado anaweza kuwa hajapona na kufura mahali pale

  • Alikoshonwa bado hajapona

Baada ya kuraruka kwa uke ama episiotomy, daktari hushona pale palipo raruka ili kupona. Kupona kunaweza kuchukua siku ama wiki. Ata kwa kina mama waliopitia upasuaji wa C-section, zile nyuzi zinaweza kuwa bado ni laini.

Kina mama waliojifungua majuzi wanawezaje kupunguza uchungu?

how to ease the pain

Jadiliana na daktari wako kuhusu dawa iliyo sawa ili kuhimili ule uchungu. Ibuprofen, malai ya kutuliza, na dawa za kulegeza choo zinaweza kusaidia. Kutilia mkazo palipo na uchungu ni moja wa njia za kumudu uchungu wakati wa kujisaidia.

Unaweza kutumia diaper iliyagandishwa ama maternity pad na utilie mkazo kwenye uke. Jiepushe na jibini ama vyakula vinavyofanya choo kuwa kigumu kama mkate, mchele, pasta na mayai. Badala yake tumia matunda mbichi na mboga: jiepushe na zilizo kwenye mkebe. Chakula chenye mafuta na kilichosagwa pia hakitakikani.

Iwapo uchungu hautaendelea kupunguka kila mara unapojisaidia, shauriana na daktari wako ili kujua chanzo na kukuelekeza  kwa njia inayofaa ili kupona. Ili uweze kusheherekea  miezi yako  ya kwanza baada ya ujauzito.

*Makala haya yalionekana kwa mara ya kwanza katika tovuti ya theAsianparent Philippines kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Vyanzo: Romper, Baby Center, What to Expect, The Huffington Post

SOMA: Everything you need to know about postnatal care

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio