Africaparent Logo
Africaparent Logo
EnglishSwahili
  • COVID-19
  • Becoming a Mama
  • Ages & Stages
  • Parenting
  • Health
  • Feeding & Nutrition

Kujitahini Katika Uhusiano: Je, Unge Penda Kupata Mchumba Kama Wewe?

3 min read
Kujitahini Katika Uhusiano: Je, Unge Penda Kupata Mchumba Kama Wewe?Kujitahini Katika Uhusiano: Je, Unge Penda Kupata Mchumba Kama Wewe?

Lengo la kujitahini katika mapenzi na mahusiano yako ni kulenga kuchukua hatua ya kujiangalia kama mtu na kufanya kazi ili uwe bora zaidi.

Kila mtu huwa na orodha ya mambo muhimu anayo tafuta katika mwenzi wake. Ni rahisi kutaka mwanamme ama mwanamke aliye mkaribu, mwenye mapenzi, anaye mcha Mungu, mwenye hela, mrembo, na kadhalika. Swali ni: una mambo haya muhimu unayo tafuta kwa watu wengine? Kujitahini katika uhusiano ni muhimu, na huenda ukahitajika kuwa mkweli kuhusu mambo unayo yaleta kwenye uhusiano huu.

Kujitahini katika uhusiano: Je, ungependa kuwa na mchumba kama wewe?

kujitahini katika uhusiano

Jiambie ukweli: ungependa kuishi na mtu mwenye tabia sawa na zako, anaye valia na kufikiria kama wewe? Kujitahani katika mahusiano yoyote yale ni kuwa mkweli kwako kuhusu tabia zako, zote nzuri na hasi. Unavyo fikiria na kufanya katika hali zenye tabu. Una tengeneza mazingira yenye mapenzi yanayo kubalisha uhusiano kufuzu? Je, wewe ni aina ya mtu ambaye ungependa kuja nyumbani kwake?

Kujiangalia kwa undani kutakusaidia kujijua na kujifahamu vyema ili ukue na uwe mtu bora zaidi.

Una tabia hizi unazo tamani kwa mwenzi wako?

Ni jambo moja kuombea mwenzi mrefu na mwenye sura ya kupendeza atakaye kupenda hadi uzeeni. Lakini swali ni je, ungekuwa mwanamme wa aina hiyo, ungemchagua binti kama wewe?

Andika orodha ya vitu muhimu unazo tafuta kwa mchumba kisha ulinganisha na tabia zako. Ungependa mchumba anaye valia vizuri, lakini je, mavazi yako yana lingana na ya mtu unaye mtamani? Ungependa mtu aliye tulia na asiye na mambo mengi ilhali unapenda kukasirika na una hasira nyingi mtu anapo kukosea? Una zungumza kuhusu mambo hadi mpate suluhu?

Ikiwa ungependa mtu mkarimu, jiulize mara ya mwisho ulimzawadi mtu.

Je, unakuwaje mtu wa dhamani ya kupendwa?

kujitahini katika uhusiano

Kwa sasa kwani ume gundua tabia zako hasi, hatua inayo fuata ni kutia juhudi kuzirekebisha. Lengo la kujitahini katika mapenzi na mahusiano yako ni kulenga kuchukua hatua ya kujiangalia kama mtu na kufanya kazi ili uwe bora zaidi.

Sasa toa orodha hiyo uliyo tengeneza ya vitu unavyo angalia kwa mwenzi wako na uweke alama kwenye vitu ambavyo una dhibitisha navyo. Kuna nyanja ambazo utahitaji kazi zaidi na hizi ndizo nyanja ambazo unapaswa unahitaji kubadilisha. Kuwa mtu ambaye ungependa kuwa kwa uhusiano naye.

Uta shangaa kupata kuwa unavutia aina ya watu walio kama wewe!

  • Hakuna asiye na doa

Somo muhimu sana katika kujitahini katika mapenzi ni kuwa hakuna mtu aliye sawa. Zoezi hili litakufungua macho kwa ukweli huu. Hili linapaswa kukufunza kuwa haupaswi kutarajia mwenzi asiye na doa, lakini tafuta mtu aliye na tabia na utu sawa na wako.

  • Kujipenda ni muhimu sana: kubali madoa yako

Kubali kuwa una utu hasi na utie juhudi kubadili mambo uwezavyo. Utamvutia mtu unapo kubali madoa yako na kutia juhudi kuwa mtu bora. Usikate moyo katika kujiboresha na kuwa mtu bora. Kumbatia mabadiliko na ufanye kazi hadi utimize viwango vya mtu unaye mtafuta.

Soma Pia: Siri 5 Kuu Za Kudumisha Uhusiano Bora Wa Kimapenzi

Got a parenting concern? Read articles or ask away and get instant answers on our app. Download theAsianparent Community on iOS or Android now!

img
Written by

Risper Nyakio

  • Home
  • /
  • Relationship & Sex
  • /
  • Kujitahini Katika Uhusiano: Je, Unge Penda Kupata Mchumba Kama Wewe?
Share:
  • Malengo 7 Ya Uhusiano Ya Kufanya Mapenzi Yenu Yawe Bora Zaidi

    Malengo 7 Ya Uhusiano Ya Kufanya Mapenzi Yenu Yawe Bora Zaidi

  • Jinsi Ya Kukuza Imani Katika Uhusiano: Njia Za Kujenga Uaminifu

    Jinsi Ya Kukuza Imani Katika Uhusiano: Njia Za Kujenga Uaminifu

  • Mazungumzo 5 Muhimu Sana Katika Uhusiano Yasiyo Paswa Kupuuzwa

    Mazungumzo 5 Muhimu Sana Katika Uhusiano Yasiyo Paswa Kupuuzwa

  • Kufanya Tendo La Ndoa Kila Siku Kuna Manufaa Gani Kwa Afya Yako?

    Kufanya Tendo La Ndoa Kila Siku Kuna Manufaa Gani Kwa Afya Yako?

  • Malengo 7 Ya Uhusiano Ya Kufanya Mapenzi Yenu Yawe Bora Zaidi

    Malengo 7 Ya Uhusiano Ya Kufanya Mapenzi Yenu Yawe Bora Zaidi

  • Jinsi Ya Kukuza Imani Katika Uhusiano: Njia Za Kujenga Uaminifu

    Jinsi Ya Kukuza Imani Katika Uhusiano: Njia Za Kujenga Uaminifu

  • Mazungumzo 5 Muhimu Sana Katika Uhusiano Yasiyo Paswa Kupuuzwa

    Mazungumzo 5 Muhimu Sana Katika Uhusiano Yasiyo Paswa Kupuuzwa

  • Kufanya Tendo La Ndoa Kila Siku Kuna Manufaa Gani Kwa Afya Yako?

    Kufanya Tendo La Ndoa Kila Siku Kuna Manufaa Gani Kwa Afya Yako?

Get advice on your pregnancy and growing baby. Sign up for our newsletter
  • Becoming a Mama
    • Pregnancy
    • Delivery
    • Losing a Baby
  • Ages & Stages
    • Baby
    • Toddler
    • Kids
  • Parenting
    • News
    • Relationship & Sex
    • Parent's Guide
  • Health
    • Allergies & Conditions
    • Vaccinations
    • Diseases-Injuries
  • Feeding & Nutrition
    • Breastfeeding & Formula
    • Latching & Concerns
    • Weaning
  • More
    • TAP Community
    • Advertise With Us
    • Contact Us
    • Become a Contributor


  • Singapore flag Singapore
  • Thailand flag Thailand
  • Indonesia flag Indonesia
  • Philippines flag Philippines
  • Malaysia flag Malaysia
  • Sri-Lanka flag Sri Lanka
  • India flag India
  • Vietnam flag Vietnam
  • Australia flag Australia
  • Japan flag Japan
  • Nigeria flag Nigeria
  • Kenya flag Kenya
© Copyright Africaparent.com 2022 Tickled Media Pte Ltd. All rights reserved
About Us|Team|Privacy Policy|Terms of Use |Sitemap HTML

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it