Kupata na kumlea ni jukumu kubwa na lenye mahitaji mengi. Wazazi wanapaswa kufikiria kwa makini na kujipanga ipasavyo kabla ya kufanya uamuzi wa kupata mtoto. Katika makala haya, tuna angazia maswali muhimu ya kujiuliza katika mchakato wa kujitayarisha kulea mtoto. Kwa walio na wachumba na wasio na wachumba.
Kujibu maswali haya na kuwa na mjadala kuhusu mambo haya kutasaidia kufahamu iwapo nyote wawili mko tayari kumlea mtoto ama la. Mkihisi kuwa kuna mambo mnayo paswa kuangazia na kutimiza kabla ya kulea watoto. Ni vyema kuyafanya kwani kulea huwa na mahitaji mengi sana. Ya kifedha, kihisia na pia wakati. Tazama!
Kujitayarisha kulea mtoto: Nahitaji msaada wa aina gani nikipata mtoto?

Kupata mtoto huwa mojawapo ya baraka nyingi tunazo pokea duniani. Huku wengine waki pata watoto na wachumba wao, kuna wanao fanya uamuzi wa kulea mtoto peke yao, huku wengine wakiwa wazazi wa pekee kufuatia sababu tofauti. Yote ni sawa na hakuna kinacho kufanya kuwa mzazi asiye kamili, kila mzazi ako kamili jinsi alivyo. Hata hivyo, ulezi huja na majukumu tele. Mtoto ana hitaji utunzaji na kuegemezwa na wakati mwingi.
Haijalishi iwapo wewe ni mzazi wa kipekee ama mchumba wako anakusaidia. Watoto wana mahitaji tele. Na utahitaji msaada, kutoka kwa mchumba wako, marafiki na familia. Ulezi ni rahisi unapo pata msaada.
Maswali ya kujiuliza unapo taka kupata mtoto na mchumba wako:

- Mnakubaliana kupata mtoto?
- Mko tayari kifedha na kihisia kuwa wazazi?
- Uhusiano wenu una afya?
- Nyumba yenu ina amani tosha ya kuwaleta watoto humo?
- Mnakubaliana mtakavyo timiza majukumu ya kinyumbani?
Wanandoa wanapaswa kuwa na mjadala kuhusu mambo hayo kabla ya kufanya uamuzi wa kuwa wazazi. Kumbuka kuwa kupata mtoto kuta athiri uhusiano wenu. Hata hivyo, ni muhimu kwenu kuwa karibu zaidi katika kipindi hiki.
Kwa wanao panga kuwalea watoto peke yao bila wachumba, tazama maswali unayo paswa kujiuliza:
- Niko tayari kumlea mtoto peke yangu bila usaidizi?
- Nime jitayarisha vya kutosha kifedha kulea mtoto?
- Nimekua ipasavyo kihisia kum-egemeza mtoto wangu?
- Kupata mtoto bila mchumba kuta athiri kivipi kazi yangu na maono yangu ya usoni?
- Nina kundi la watu ambao wanaweza kunisaidia niki zidiwa?
- Nikipata mchumba mwingine uhusiano na mtoto wangu utaathiriwa?
Sababu tofauti huenda zikamfanya mtu kufanya uamuzi wa kuwa mzazi wa kipekee. Huenda wanandoa pia wakatengana mwanamke anapokuwa na mimba ama baada ya kujifungua. Na hana budi wala kumlea mtoto yule peke yake. Ni jukumu gumu, ila mzazi anapo jikakamua, ana litimiza.
Chanzo : WebMD
Soma Pia: Vidokezo Vya Kuwa Mzazi Bora