Kuwa mzazi ni suala kubwa, kuna mengi yanayo paswa kuangaziwa. Hata kama kuna wakati ambapo mtoto huja kama haja pangiwa. Wakati ambapo wazazi wanaweza kujipanga, ni vyema kuhakikisha kuwa angalau asilimia 50 ya mahitaji yame angaziwa. Tuna angazia jinsi ya kujitayarisha kuwa mzazi.
Ulezi una hisia tofauti, furaha, kuhisi ume fanikiwa, maisha kubadilika, mawazo tele, kukosa usingizi katika siku za kwanza chache. Na kuwa mojawapo ya uamuzi bora zaidi ambao wanandoa wanaweza fanya. Kuona mtoto wao akikua na kujivunia juhudi walizo tia kumlea. Kumlea mtoto kunahitaji mapenzi nyingi, nishati na utulivu.
Watoto hubadilika sana wanapo zidi kukua. Jukumu kuu la mzazi ni kufahamu jinsi ya kumlea mtoto kwa njia ambayo ana hisi furaha, mapenzi, na kwa njia yenye afya.
Je, niko tayari kuwa mzazi?

Hata kama kupata mtoto ni jambo lenye furaha nyingi, lina changamoto tele. Kuwa na mtoto ni sawa na kuwa na mgeni asiye na kitu chochote na anaye kutarajia kumlisha na kumpa kila kitu anacho hitaji. Mahitaji ya mtoto huzidi kuongezeka anavyo zidi kukua.
Mtoto ana hitaji vitu hivi:
Utunzaji - mzazi anapaswa kuwa na uwezo wa kumtunza mtoto. Pamoja na nishati ya kumtunza, kihisia, mahitaji na nguvu za mwili.
Wakati - kumlea mtoto sio kazi ambayo mzazi anaweza wacha wakati wowote. La hasha, unapo amua kuwa mzazi, fahamu kuwa, umeanza kazi ya siku nzima na isiyo na likizo.
Fedha - watoto wana mahitaji mengi, kama vile kununuliwa diapers, chakula, kulipia utunzaji wa afya, chakula na kadhalika. Mzazi pia atapata mahitaji mapya, kutunza afya yake, kununua mavazi mapya ama hata kuanza darasa za kupunguza uzito baada ya kujifungua.
Kabla ya kufanya uamuzi wa kuwa mzazi, hakikisha uko sawa kihisia na kuwa una uwezo wa kumwegemeza mtoto wako kihisia.
Kujitayarisha kuwa mzazi: Maswali muhimu ya kujibu kabla ya kufanya uamuzi huu

- Je, nimekua kihisia kumwegemeza mtoto wangu kihisia?
- Nimejitayarisha vya kutosha kuchukua majukumu ya mahitaji yote ya mtoto wangu?
- Nina uwezo wa kifedha wa kuyaegemeza mahitaji yote ya mtoto wangu?
- Jambo lisilo kusudiwa likitendeka, nina mtu atakaye nisaidia kulea mtoto?
- Kupata mtoto saa hii kuta athiri kazi yangu ama uhusiano wangu?
- Kuna mtu anaye nishinikiza kupata mtoto?
- Mwili wangu uko tayari kupitia safari ya kuwa mjamzito?
- Nitamlea mtoto huyu pamoja na nani?
- Nina familia na marafiki ambao wanaweza kunisaidia jambo lolote hasi liki ibuka katika safari yangu ya ulezi?
- Nina uwezo wa kifedha wa kulipia utunzaji wa kiafya kabla ya kujifungua na baada ya kujifungua?
Ni kweli kuwa, hata kama ungetaka kupata wakati bora zaidi wa kupata mtoto, nafasi ni kuwa wakati huu hautawahi fika. Lakini kuna vitu ambavyo vinaweza kudokezea kuwa uko tayari kuwa mzazi. Ukihisi kuwa uko tayari kifedha na kihisia kupata mtoto, na una watu wa kuegemea, ni wakati sawa kwako.
Chanzo : WebMD
Soma Pia: Changamoto Za Kuwa Mzazi Mmoja Na Jinsi Ya Kuwa Mzazi Mmoja Bora