Jinsi Ya Kujua Iwapo Mtoto Ana Njaa Baada Ya Kumlisha

Jinsi Ya Kujua Iwapo Mtoto Ana Njaa Baada Ya Kumlisha

Huenda ikawa kuangalia wakati kati ya kumlisha mtoto sio jambo la busara kwani saizi ya tumbo ya mtoto haijulikani.

Ni muhimu sana kwa mama kujua iwapo mtoto ana njaa. Kuna njia nyingi ambazo unaweza jua ikiwa mtoto ana njaa na angetaka maziwa ya mama kama vile wanapo:

 • Onyesha ishara za kutafuta chuchu zako, ama kuanza kunyonya wanacho pata
 • Kulia ovyo na kuto tulia
 • Kusongesha kichwa kutoka upande mmoja hadi mwingine
 • Kufungua midomo yao
 • Kutoa ulimi nje ya mdomo
 • Kuwekelea mikono juu ya midomo yao
 • Kufanya midomo kana kwamba wana nyonya

Kujua iwapo mtoto ana njaa: Epuka kufanya haya

Kujua iwapo mtoto ana njaa

 • Usingoje mtoto wako anapo hisi njaa zaidi na kuanza kulia ili umnyonyeshe. Huenda akawa hana starehe ya kula vyema. Kulia kutamchokesha na huenda akalala kabla ya kunyonya vyema.
 • Usiwe na shaka mtoto asipo nyonya baada ya kila masaa mawili ama matatu. Unatafuta ratiba sio mfumo mkali. Unapo angazia ishara tulizo sema, ratiba ya kula itafuata.
 • Usiwe na shaka kuwa mtoto wako ana kosa chakula tosha ama ikiwa unatoa maziwa tosha ya mtoto wako. Kumlisha mara kwa mara kuta ashiria mwili wako kutoa maziwa zaidi. Ikiwa una shaka kuhusu mtoto kushiba, angazia jinsi diaper unazo mbadilisha zilivyo na kuongeza uzito kwake. Ikiwa mtoto wako anaongeza uzito inavyo faa na kubadili diaper mara 5 ama 6 kwa siku, ako sawa.
 • Kumlisha mtoto wako zaidi hata anapo shiba. Kuna ishara nyingi za kawaida kama vile kutokuwa na hamu ya kula ama kupunguza mwendo wa kunyonya ama kuangalia upande mbali na chuchu. Koma kumnyonyesha unapo ona ishara hizi na usimlazimishe kunyonya zaidi.

Je, unapaswa kumlisha mtoto vipi?

Kujua iwapo mtoto ana njaa

Huenda ikawa kuangalia wakati kati ya kumlisha mtoto sio jambo la busara kwani saizi ya tumbo ya mtoto haijulikani. Na huenda mtoto akawa na shibe masaa mengi baada ya kunyonya. Huku mwingine akihitaji kunyonya mara kwa mara.

Njia hasa ya kumlisha mtoto ni kuangazia kuwa hawana njaa. Kwa kuangalia ishara zake za njaa na kumnyonyesha anapo hitaji kunyonya hata inapo maanisha kunyonya mara nyingi kwa lisaa limoja.

Kwa hivyo mama, angazia ishara hizi muhimu kufahamu wakati ambapo mtoto wako anahitaji kula. Usikawie kumnyonyesha mtoto zaidi ya mara moja kwa chini ya lisaa limoja.

Vyanzo: ResearchGate, NCBI, Sciencenews.org

Soma Pia: Ishara Kuwa Mtoto Wako Hapati Maziwa Tosha Ya Mama

Written by

Risper Nyakio