Vidokezo Vya Kukusaidia Kujua Ikiwa Manii Yana Afya Kwa Kuangalia

Vidokezo Vya Kukusaidia Kujua Ikiwa Manii Yana Afya Kwa Kuangalia

Kujaribu kutunga mimba kunaweza kuwa mojawapo ya wakati wenye changamoto zaidi kwa wanandoa. Kuwa na manii yenye afya kuna imarisha nafasi zako za kupata mimba.

Kujaribu kutunga mimba kunaweza kuwa mojawapo ya wakati wenye changamoto zaidi kwa wanandoa. Ni salama kusema, kuwa na manii yenye afya ama yenye nguvu kuna imarisha nafasi zako za kupata mimba. Lakini baadhi ya wakati, mada hii huenda ikawa ngumu kujadili na bwanako. Linaweza kuwa suala nyeti kuzungumzia ama hata kuanzisha. Kwa hivyo, utawezaje kujua manii yenye afya kwa kuangalia? Tuna vidokezo vichache vya kukusaidia kujua.

Jinsi ya kujua manii yenye afya kwa kuangalia

Vidokezo Vya Kukusaidia Kujua Ikiwa Manii Yana Afya Kwa Kuangalia

Shahawa ya mumeo ina sema mengi kuhusu afya yake ya manii, kiasili. Rangi ya shahawa ndiyo usaidizi wa kibinafsi mwema zaidi wa kudhihirisha afya yake. Kitu cha kwanza unacho paswa kuangalia ni rangi ya manii na itakujulisha mengi kuhusu afya yake:

  • Nyeupe ya mawingu ama grey

Shahawa ya kawaida huwa na rangi nyeupe kana kwamba mawingu, na kana kwamba mafuta. Ikiwa hii ndiyo rangi ya shahawa ya mumeo, vyema! Zingatia mtindo wa maisha wenye afya kama vidokezo tulivyo angazia hapa juu vya viwango vya juu vya manii na ubora wake.

  • Pinki, nyekundu, hudhurungi na machungwa

Hii huenda ikawa ni hematospermia ama damu kwenye shahawa. Katika visa vingine, huenda ikawa kufuatia ngono nyingi ama kujifurahisha kingono, ambayo inapaswa kujitatua kipekee baada ya siku chache. Katika visa sugu, huenda ikawa ni kufuatia shinikizo la damu, maambukizi ya kingono kama herpes, chlamydia na gonorrhoea ama maambukizi ya prostate. Ikiwa una hisi uchungu karibu na sehemu zako za siri, hakikisha unaenda hospitalini bila kukawia.

  • Nyeusi

Mara nyingi, shahawa nyeusi ina sababishwa na damu nzee. Lakini pia huenda ika sababishwa na maumivu kwenye uti wa mgongo. Wasiliana na daktari ikiwa hujafanya hivi bado, huenda ikawa na suala nyeti zaidi.

  • Kijani ama manjano

Rangi hii ya shahawa ina husishwa na mabaki ya mkojo na kuchanganyika na shahawa, inayo sababisha rangi hii isiyo ya kawaida. Lakini katika kesi zingine, huenda ikawa ni tatizo la kimatibabu kama vile maambukizi ya mfumo wa mkojo, maambukizi ya prostate ama maambukizi mengine ya kingono. Ikiwa bwanako anahisi uchungu baada ya kutoa shahawa, ni wakati wa kumwona daktari.

Jinsi ya kujua manii yenye afya: Zoea mitindo yenye afya

 

Manii yenye afya sio kuhusu rutuba ama uwezo wa uzalishaji wa bwanako. Kweli, umri huchangia pakubwa katika jinsi manii yako yalivyo na afya, lakini ulijua kuwa wanaume wanaweza toa manii hadi wafikishe miaka 80? Afya ya manii huanza kupunguka mwanamme anapo sherehekea siku ya kuzaliwa kwake kwa miaka 40 na uwezo wa manii kufikia yai hupunguka kati ya 20-80.

Walakini, kuna baadhi ya mitindo ambayo inaweza himizwa kwa wanaume ili kutoa manii yenye afya.

1.Iweke baridi chini huko

Manii hutolewa tu, katika temprecha baridi- kwa hivyo kunapokuwa msimu wa jua kwenye korodani, unatarajia kuwa na matatizo. Mumeo anapaswa kujitenga na kupasha joto sehemu yake ya siri. Kwa hivyo kukoga kwa maji moto ama vipindi vya sauna vinapaswa kupunguzwa. Tupilia mbali nguo za ndani zinazo bana na uvalie zilizo na nafasi tosha ili manii yaendelee kuchakatwa.

2. Kula vyema

Lishe yenye afya na iliyo sawazishwa na yenye vyakula kutoka vikundi vikuu ni muhimu katika kukupatia nishati siku yote na sio hilo tu. Mbali pia katika kutoa manii yenye afya. Chakula kilicho na folates kama mboga za kijani, viazi na protini huongeza idadi ya manii. Wakati ambapo vitamini D, kwenye nafaka na samaki hu hakikisha kuwa manii yana shepu inayo hitajika na yana uwezo wa kuogelea kwenye yai. Samaki zenye ufuta pia zina omega-3 fatty acids zinazo imarisha nambari na ubora wa manii.

3. Punguza tumbo na ufanye mazoezi

Sio tosha kula vyema tu, unahitaji kumhimiza bwanako kutoka kitini na kwenda kufanya mazoezi. Masomo yana onyesha kuwa wanaume wanao fanya mazoezi wana viwango vya juu ya testosterone inayo pelekea katika kuwa na manii bora. Mazoezi yanaweza saidia na libido pia!

4. Koma kuvuta sigara

Masomo mengi yana onyesha kuwa kuvuta sigara hupunguza kiwango cha manii, kupunguza uwezo wa manii kuogelea hadi kwenye yai na shepu duni ya manii. Pia kuna husishwa na kuharibika kwa mimba. Ikiwa bwanako atakoma kuvuta sigara sasa, utaanza kushuhudia mabadiliko baada ya miezi mitatu- wakati sawa unao chukua seli za manii kukomaa.

5. Pumzika na usiwe na fikira nyingi

Sio muhimu tu kwa mwili kuwa na afya, akili pia inahitaji kuwa sawa. Fikira nyingi hupunguza utendaji kazi wa kingono ama kukomesha utoaji wa manii. Ni muhimu kwa bwanako kupumzika na kupunguza fikira nyingi ili awe na manii yenye afya.

Chanzo: NCBI

Soma Pia:Kula Vyakula Hivi Kuongeza Idadi Ya Manii Yako

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio