Kulingana na The Guardian, uchungu wa kupoteza mtoto haulinganishwi na uchungu mwingine. Na wazazi kushangaa iwapo watahisi wako wazima tena. Mara nyingi uchungu huu huja wazazi wanapogundua kuwa wameishi miaka zaidi ikilinganishwa na watoto wao, na kuwafanya wahisi kuwa hili sio jambo la kawaida.
Wazazi mara nyingi hupitia hatua nyingi za kuomboleza kama vile kushtuka, kutokubali kilichotukia, kutamani watoto wao, kuchanganyikiwa, kuhisi hawana nguvu, kujilaumu, kukasirika, na kukosa matumaini. Ndoa nyingi huanza kuporomoka mtoto anapoaga dunia.
Uchungu wa Kupoteza Mtoto

Kunauwezekano wa kukabiliana na uchungu
La, hakuna uwezekano wa kusahau kilichofanyika. Walakini, wazazi wanaweza kufuata hatua zifuatazo, lakini hili sio ashirio kuwa watasahau uchungu wa kupoteza mtoto.
Una madoa. Hakuna mtu asiye na doa duniani. Lazima ukubali hili ili uweze kuendelea pasipo na lawama.
- Fikiria kuhusu mambo chanya
Wazazi wanaweza kukabiliana na kupoteza mtoto wanapochagua kukumbuka mambo chanya waliyofanya pamoja.

Kuomboleza kunaweza chukua haja ya kufanya mambo mengi. Kuwauliza wanafamilia na marafiki wakusaidie ndiyo njia sawa ya kufuata uchungu unapowazidia.
Wazazi wengi huhisi kana kwamba Mungu amewatupa wanapopoteza watoto wao. Usijilaumu kwa yaliyofanyika.
Mtoto anapoaga, mzazi huhisi kana kwamba amekufa pia. Kupitia hili hubadilisha maisha yako, lakini unaweza jiahidi kuendelea kuishi.
Vyanzo:
The Guardian
Healgrief.org
Soma Pia: Mambo Muhimu Ya Kuangazia Unapojitayarisha Kuwa Mzazi!