Jinsi Ya Kukabiliana Na Utasa Kwenye Ndoa

Jinsi Ya Kukabiliana Na Utasa Kwenye Ndoa

Infertility is when you have trouble getting pregnant or staying pregnant. Fertility problems can happen in women and men and can have many causes. That’s why both people are usually tested for infertility if a couple is having trouble getting pregnant.

Utasa  ni wakati ambapo mtu ana shida kupata au kulea mimba. Utasa unaweza kumpata mwanamke au mwanamume na una vyanzo vingi.  Utasa ni jambo la kawaida.

Watu wengine huwa na wakati mgumu kupata ua kulea mimba. Mtu huweza kusemekana kuwa tasa baada ya mwaka mmoja au miwili ya kujaribu kupata mimba bila mafanikio. Ama kama unapoteza mimba mara kwa mara. Kuna matibabu ya aina nyingi za utasa na watu wengi huweza kupata mimba na kujaliwa na mtoto.

Utasa sio shida ya wanawake pekee au shida inayotokana na uzee. Mambo nyingi yaweza kusababisha utasa na inaweza kuathiri watu wa jinsia zote na umri wowote ule. Wakati wanandoa wana shida ya kupata mimba, mmoja wao au wote wana uwezo sawia kuwa ndio wenye tatizo. Hii ndio sababu madaktari huwapima wato iwapo wanandoa wana matatizo ya kupata mimba.

Je, nini chanzo cha utasa?

utasa

Kuna sababu nyingi zinazoweza kusababisha utasa. Kumwona daktari maalumu mwenye ujuzi wa mambo ya utasa inaweza kukusaidia kutatua shida yako ya utasa. Atakutafutia dawa zinazo kufaa. Wakati mwingine hakuna chanzo kinachojulikana cha utasa. Hii hujulikana kama utasa usioeleweka.   Utasa usioeleweka waweza kuvunja moyo sana lakini bado kuna mbinu za matibabu ambazo mtu anaweza kujaribu.

Sababu za utasa kwa wanawake

Sababu mojawapo za utasa kwa wanawake huwa:

 • Chlamydia au kisonono ambayo haikutibiwa
 • Kutoachiliwa kwa mayai kutoka kwa ovari zako
 • Mirija ya fallopia imefungika hivyo basi mbegu haziwezi kupita kufikia yai
 • Mayai ya gredi ya chini
 • Umbo la tumbo la uzazi chako kustawisha yai lililotungishwa
 • Endometriosis
 • Fibroids katika tumbo la uzazi

Sababu za uzaaji wa chini kwa wanaume

Sababu nyingi za utasa kwa wanaume huwa:

 • Chlamydia ua kisonono ambayo haikutibiwa
 • Idadi ndogo ya mbegu( kutokuwa na mbegu nyingi kwenye manii)
 • Mbegu isio na uwezo wa kutembea( wakati ambapo mbegu haiogelei vizuri kufikia yai)
 • Mbegu ambazo bado hazijakomaa vizuri
 • Manii yaliyo mazito sana kwa mbegu kutembea
 • Kutokuwa na mbegu kwenye manii.

Nini kinachoongeza hatari yangu kuwa tasa?

utasa

Kuna mambo ya kiafya na mtindo wa maisha ya mtu binafsi inayochangia ongezeko la hatari ya utasa. Hizi ni kama vile:

 • Kupitisha umri wa miaka 35 kwa wanawake
 • Kuwa na uzani wa kiwango cha juu sana au chini zaidi
 • Kemotherapi au radiation
 • Kuwako katika mazingira yenye sumu kama vile lead na dawa za kuulia wadudu
 • Matumizi mabaya ya dawa au pombe
 • Kuvuta sigara
 • Kutofanyiwa vipimo vilivyopendekezwa vya chlamydia au kisonono
 • Historia ya pelvic inflammatory disease( PID)
 • Ajali kwenye korodani au pumbu
 • Mapumbu yenye joto (kutokana na kuvalia nguo zinazobana au kuogelea ama kuoga na maji moto mara nyingi na hivi karibuni).
 • Mapumbu kuwa mahali yasipofaa

Jinsi ya kukabiliana na utasa

utasa

Utasa ni hali ya kiafya inayogusa nyanja zote za maisha kutoka kwa jinsi unavyojisikia katika maisha yako, uhusiano wako na mpenzio  na jinsi unavyoyaona maisha kwa ujumla. Inaweza pia kuwa changamoto pale inapoleta kutojua na hisia mchanganyiko katika maisha ya wanandoa ya kila siku. Kama umekuwa ukipambana na utasa, mkazo wa mawazo sio jambo geni kwako. Lakini ata kama hali yako inalemaza aje kunazo njia za kukusaidia kupambana na wasiwasi. Hapa kunazo njia 12 za kulenganisha mawazo yako kwa akili na mwili wako ili kukupa utulivu katika maisha yako.

 1. Kubali mawazo yako

Jambo la kwanza kukabiliana na mkazo wa mawazo ni kuelewa kuwa unavyohisi ni kawaida kabisa. Kupitia uchunguzi na utaratibu mwezi baada ya mwingine kunaweza kukupooza, hisia, mwili na pia fedha na kujihisi kama huna uweza juu ya mwili wako.

 1. Jadili maswali na woga wako

Unapo kabiliana na utasa, kunasaidia kuwa na watu karibu nawe wanaoweza kuyajibu maswali yako. Kuwa makini kwa hisia zako na uelewe woga na wasiwasi wako. Kama kuna mshauri wa mambo ya uzazi unaweza penda kuzungumza naye ama kujiunga na kundi lenye watu walio na shida ya utasa katika eneoa lako.

 1. Ongea na mpenzi wako

Jinsi Ya Kukabiliana Na Utasa Kwenye Ndoa

Utasa unaweza kusababisha shida katika ndoa mara nyingi ikileta chuki isiyotajwa, kujihisi kutokuwa kamili, ugumu katika kufanya mapenzi na mvutano katika wanandoa. Isitoshe mwanamke au mwanamume wanaweza itikia hili tatizo kitofauti. Kwa wanaume wakienda mbali kimawazo na wanawake kufadhaika.

4. Jaribu upendo mwororo

Njia nyingine ya kujenga uhusiano baina yako na mchumba wako, ni kujenga mahaba kupitia kufanya mapezi au mbinu zisizo husisha mapenzi. Kwa mfano, unaweza mwandalia mpenzi wako chakula kitamu au kinywaji, mnunulie zawadi ya kupendeza, nunua tiketi za tafrija au michezo ya riadha, kukumbatiana, kushikana mikono, kwenda matembezi na kusuguana mgongo.

5. Pata ufahamu

Jambo moja ambalo huwa chanzo za mkazo wa mawazo ni kutojua juu ya siku za baadaye. Na iwapo umepitia miezi kama sio miaka ya matibabu juu ya utasa, una uhakika umeishi na kutojua kwa wakati mrefu.

Ili kupunguza maswali yako juu ya siku za baadaye, inasaidia kufanya utafiti wa undani juu ya hali yako ya sasa na chaguo ulizo nazo. Kwa mfano kaa kwa ufahamu juu ya hali uliyo nayo na matibabu yake  lakini pia fanya utafiti juu ya hali zingine za utasa na njia mbadala  zilizoko kama vile kumtafuta mtoto  na kama zitafanya kazi kwa familia yako. Hata kama huwezi kutazama mafuta ya kifuwele na kuona siku za mbeleni lakini unaweza jiami na ujuzi na upate amani nyingi akilini mwako.

6. Tafuta njia za kupunguza mkazo wa mawazo.

Njia nzuri ya kujituliza na kuinua roho yako ni kufuatilia na kuzingatia njia ulizo jaribu na kutumia wakati umepita.  Watu wengine kwa mfano, huona kuwa kutembea au kuanza jambo mpya la kufurahisha huwasidia kupunguza wasiwasi. Wengine hupata kuwa kuongea na wanaowapenda, kutafakari, kuomba, kufanya mazoezi, kufanya yoga, au kujiunga na kundi la kukusaidia ama kutafuta maarifa kuhusu shida zao huwasidia kuhisi vizuri.  Wengine pia hupata amani kwa kubadilisha jambo mbaya kuwa nzuri ama kwa kujikumbusha kuchukua siku moja kwa wakati.

Jinsi Ya Kukabiliana Na Utasa Kwenye Ndoa

Wataalam hupendekeza mtu kutafuta na kutumia njia mbili za kukabiliana na mkazo wa mawazo kila siku.  Pia wanapendekeza usiache kutumia hizi njia pindi unapoamka na kujihisi vyema. Majibu kwa shida za utasa huweza kubadilika kutoka siku moja hadi nyingine.

Mwishowe kuna siku ambayo hakuna kitu kitaonekana kufanya kazi na bado utajihisi mwenye machovu na mnyonge. Utawezaje kupitia hivi vipindi? Tazamia kuwa nyakati hizi zitatokea na jaribu kuzipokea zitakavyo kuja. Pia farijika kwa kujua kuwa njia hizi za kupambana na mkazo wa mawazo unazojifunza zitakuweka mahali salama kwa miaka mingi inayokuja na pia zinaweza kukutayarisha kwa uzazi.

 MayoClinic.com

Also read: What Causes Multiple Miscarriages: Tests, Risk Factors And Treatment

Written by

Risper Nyakio