Kukausha maziwa ya mama hufanyika kiasili baada ya mama kumaliza kunyonyesha mtoto. Kuna visa ambapo mama angependa kukausha maziwa yake ama kupunguza kiwango cha maziwa kinachotoka.
Kwa mama ambaye angali ananyonyesha, hashauriwa kujaribu kukausha maziwa, huenda mtoto akakosa kupata maziwa tosha. Kuna baadhi ya mbinu zinazotumika kukausha maziwa ya mama.
Kuepuka kunyonyesha na kukamua maziwa ya mama

Ili kukausha maziwa kwa njia asili, mama hushauriwa kukoma kunyonyesha ama kukamua maziwa. Kwani kiwango cha maziwa huongezeka kadri maziwa yanavyohitajika. Kwa hivyo yasipohitajika, utoaji wake utapungua kisha kukauka.
Kulingana na utafiti, majani ya kabichi yanasaidia kutatua hali ya maziwa ya mama kufura. Pia yameonyeshwa kusaidia kupunguza utoaji wa maziwa ya mama. Hata kama kuna utafiti tofauti unaodokeza kuwa majani haya yanaongeza utoaji wa maziwa kwani mama hahisi uchungu anaponyonyesha.
- Utumiaji wa miti shamba na chai
Kuna baadhi ya miti shamba iliyo na nguvu za kupunguza kiwango cha maziwa ya mama. Vitu kama sage, jasmine na peppermint oil yana uwezo wa kumsaidia mama anayelenga kupunguza kisha kukausha utoaji wa maziwa.
Tembe za kupanga uzazi zilizo na kichocheo cha estrogen zinasaidia kupunguza kiwango cha maziwa ya mama. Utumiaji wa tembe za uzazi wa mpango zimedhibitishwa kupunguza utoaji wa maziwa baada ya siku 7.
Wasiliana na daktari unapo:

- Anza kupata vidonda kwenye maziwa
- Kuona ishara za mastitis
- Kuathiriwa na dawa za kupunguza kiwango cha maziwa kama kuhisi kizunguzungu ama kichefuchefu
- Kusombwa na mawazo
Kukauka kwa maziwa huchukua wakati tofauti kwa kila mwanamke. Mama aliyekuwa akitoa kiwango kingi cha maziwa atachukua muda zaidi kabla ya maziwa yake kukauka, ikilinganishwa na mwanamke aliyekuwa na kiwango cha chini cha maziwa ya mama.
Kutumia dawa kukausha maziwa kuna athari hasi kwa afya ya mama. Kilicho muhimu ni kuzungumza na mtaalum wa afya kuhusu suluhu tofauti za kupunguza utoaji wa maziwa na mbinu bora zaidi kwako.
Chanzo: Healthline
Soma Pia: Fahamu Manufaa Ya Kunywa Maziwa Kabla Ya Kulala