Kukojoa mara kwa mara katika ujauzito ni jambo la kawaida. Kwa baadhi ya wanawake, kukojoa mara kwa mara ni dalili ya ujauzito. Kuhisi haja ya kwenda msalani mara kwa mara baada ya kufahamu hali ya ujauzito, sio jambo la kumfanya mama awe na wasiwasi. Lakini mama anapohisi uchungu anapoenda msalani ama ishara zingine za maambukizi ya kingono, ni muhimu kuwasiliana na daktari wake.
Sababu za mjamzito kukojoa mara kwa mara

Ishara za mimba huwa tofauti kwa wanawake. Wanawake wengi hushuhudia hamu ya kwenda msalani mara kwa mara katika muhula wa kwanza wa mimba. Baadhi ya wanawake huenda wakapata hali ya kuvuja mkojo ama leakage ambapo mkojo wanashindwa kudhibiti utoaji wa mkojo. Jinsi mimba inavyokua, ndivyo inavyosukuma kibofu cha mkojo, mrija wa mkojo na misuli ya pelviki na kuifanya iwe vigumu kwa mama kudhibiti mkojo wake. Mwanamke hugundua kuwa anavuja mkojo anapo:
- Kohoa
- Kuchemua
- Kucheka
- Kutembea
- Kuinua vitu
Kukojoa mara kwa mara katika ujauzito husababishwa na ongezeko la homoni mwilini. Homoni za progesterone na hCG humfanya mama ahisi kwenda msalani mara zaidi.
Kukua kwa fetusi na kusukuma kibofu cha mkojo cha mama humfanya ahisi kutumia choo mara zaidi.
Suluhu

- Mazoezi ya Kegel yanayoipa misuli ya pelviki nguvu yanasaidia kuegemeza kibofu cha mkojo kiweze kudhibiti na kuzuia kuvuja mkojo.
- Kudhibiti unywaji wa viowevu muda mfupi kabla ya kwenda kulala.
- Kupunguza ama kujitenga na unywaji wa kaffeini na bidhaa zake.
- Kukunywa maji tosha kila siku. Kati ya vikombe 8 na 12 ni muhimu katika ujauzito.
Wakati mwingine, huenda kuhisi kukojoa mara kwa mara kukawa ishara ya maambukizi ya mfumo wa mkojo. Ishara zaidi ni:
- Kupitisha mkojo wenye damu
- Mkojo wenye harufu kali
- Uchungu mkali unapopitisha mkojo
- Kushindwa kudhibiti kuvuja mkojo
- Maumivu ya upande wa chini wa tumbo
- Kuhisi kichefuche
Kukojoa mara kwa mara katika ujauzito sio jambo la kutia wasiwasi, ila linapoandamana na ishara za maambukizi ya mfumo wa mkojo, ni muhimu kwenda hospitalini. Hali ya kuvuja mkojo katika mimba hujitatua bila dawa zozote na huisha baada ya kujifungua.
Chanzo: Healthline
Soma Pia: Maambukizi Yanayo Sababisha Mwanake Mwenye Mimba Kuharibika Kwa Mimba