Mara 3 Ambapo Ni Sawa Kukoma Kunyonyesha Mtoto

Mara 3 Ambapo Ni Sawa Kukoma Kunyonyesha Mtoto

Kumnyonyesha mtoto ni muhimu sana katika miezi ya kwanza sita ya maisha ya mtoto. Kuna sababu ambazo ni sawa kukoma kunyonyesha mtoto.

Kunyonyesha ni mojawapo ya vitendo asili zaidi kwa mama na mtoto wake mchanga. Shirika la Afya Duniani lina shauri wanawake kunyonyesha watoto bila kuwalisha kitu chochote kingine kwa miezi 6 ya kwanza ya maisha yao. Walakini, kulingana na utafiti ulio fanyika na American Association of Pediatrics (AAP), 2/3 ya wanawake ambao wangependa kuwanyonyesha watoto wao huenda waka shindwa kufikisha wakati unao faa. Sio rahisi inavyo onekana. Je, kuna muda wa wastani wa kukoma kunyonyesha mtoto?

Hapa kuna mwongozo wa kukusaidia kujua wakati bora wa kukoma kunyonyesha kuliko kuendeleza. Ni vyema kujua kuwa hatu shauri kuwacha kunyonyesha. Lengo letu ni kusaidia wamama kushinda hisia za hatia ambazo mama huhisi wakati ambapo analemewa kunyonyesha mtoto kwa sababu za kifizikia na afya ya akili.

Je, kuna umri wa wastani wa kukoma kunyonyesha mtoto? Ni wakati upi sawa kuwacha?

kukoma kunyonyesha mtoto

Kunyonyesha ni lishe inayo shauriwa ya watoto wote. Mashirika kama vile WHO na AAP yana shauri kunyonyesha peke yake kwa umri wa miezi ya kwanza sita ya maisha ya mtoto.

Kumnyonyesha mtoto peke yake kuna husisha kumlisha maziwa ya mama peke yake bila kuongeza maji ama kitu kingine.

WHO ina shauri kuwa nyonyesha watoto kwa muda wa miezi 24 na zaidi. Kipindi kati ya miezi 6 na 24 ni wakati ambapo watoto wana anzishiwa kula vyakula vya watu wazima. Maziwa ya mama ni chanzo cha virutubisho vyote ambavyo ni muhimu kwa mtoto wa miezi sita. Pia, ni muhimu katika kumpa mtoto kinga anayo faa. Na kuboresha utangamano kati ya mama na mtoto.

Kunyonyesha kuna faida nyingi. Hata hivyo, wanawake wengi hutatizika wanapo nyonyesha kwa sababu tofauti. Kwa hivyo, swali unalo paswa kuuliza ni, je, kunyonyesha kunapaswa kuendelea katika nyakati ambazo una filisika kimawazo? Tuna angazia wakati ambao ni sawa kunyonyesha, na wakati ambao ni sawa kuendelea.

Omba msaada kwanza

Baadhi ya wamama huweza kufanya kazi na bado kunyonyesha watoto bila kutatizika. Walakini, kwa wamama wengi, sio rahisi, kama inavyo dhihirishwa na utafiti wa AAP.

Kwa bahati nzuri, tunaishi kwa wakati ambapo lishe ya mtoto haita athiriwa ikiwa mama hawezi nyonyesha. Na maendeleo ya kisayansi yame hakikisha kuwa sehemu zingine za faida za maziwa ya mama yanaweza dhibitishwa kwa kiwango fulani.

Kwa hivyo, ikiwa unaweza, hakikisha kuwa unam nyonyesha mtoto wako kwa angalau miezi sita. Walakini, hakuna wakati fulani unao faa kukoma kumnyonyesha mtoto. Ukipata matatizo ya mtoto kunyonya ama shida zingine, ni vyema kujadili na daktari wako ili akushauri na akusaidie.

Sababu 3 Za Kukoma Kunyonyesha Mtoto

kukoma kunyonyesha mtoto

Baadhi ya wakati, wamama walio na matatizo za kunyonyesha wanaweza saidiwa kutatua matatizo yao kwa kupata msaada wanao taka na kwa wakati unao faa. Lakini kuna wakati ambapo kumkomesha mtoto kunyonya huenda kukawa bora kwa mama na mtoto.

Hapa kuna sababu tatu.

  1. Kufilisika kimawazo ama kuhisi kuhatarisha maisha ya mtoto

Moja kati ya wanawake watano hutatizika na kufilisika kimawazo katika mwaka wa kwanza baada ya kujifungua. Mawazo ya kujiua ni sababu ya pili inayo sababisha vifo baada ya kujifungua na kuwa moja kati ya kila vifo vitano baada ya kujifungua.

Je, una tatizika na mawazo na mhemko usio kupendeza, na kunyonyesha kuna kuwa kugumu zaidi? Kuwa karibu zaidi na mtoto wako unapo mnyonyesha kuna ibua mawazo yasiyo pendeza? Una chukua dawa kufuatia kufilisika kimawazo? Una hisi kuhatarisha maisha ya mtoto wako ama yako unapo nyonyesha?

Ikiwa jibu lako kwa maswali haya ni "ndiyo", usihisi hatia kuhusu kukoma kumnyonyesha mtoto wako. Na katika wakati huo, ni vyema uongee na daktari wako bila kukawia.

2. Watoto zaidi ya mmoja

Ikiwa una mapacha ama zaidi, hongera! Walakini, kuangalia watoto wengi wakati mmoja sio kazi rahisi.

Wanawake wengi huweza kuwa nyonyesha watoto wao bila matatizo yoyote. Walakini, huenda ikawa vigumu kwa wamama wengine kunyonyesha watoto wengi.

Ikiwa inakutatiza kuwalisha watoto wako, ni sawa kutafuta njia mbadala. Una hitaji nguvu ya kuwa tunza watoto wako.

3. Mtindo wa maisha unao chosha

Unapo rudi kazini, huenda ukatamani kukamua maziwa ili mtoto wako aendelee kupata faida zake. Wamama wengi wanaofanya kazi na kuwa nyonyesha watoto huweza kukamua maziwa bila kutatizika.

Walakini, wamama wengine huenda waka tatizika kufanya hivyo ama hata kuwa na maziwa tosha. Pia, baadhi yao huenda waka safiri sana kwa sababu ya kazi yao. Kwa kisa hicho, ili kuwa na maziwa tosha, unahitajika kukamua maziwa mara kwa mara. Na ikiwa una safiri kwa muda mrefu, ni vigumu kuwa na utaratibu wa kukamua maziwa.

Huenda pia ikawa vigumu kuratibisha utaratibu wa kukamua maziwa ya mama. Na wakati huo, huenda wengine wakawa na shida za kuhifadhi maziwa waliyo kamua.

Ikiwa hauna vifaa vya kuhifadhi maziwa vymea ama ikiwa una safiri kwa muda mrefu mara kwa mara, ni sawa kutafuta njia mbadala. Kama unavyo ona, hakuna wakati wa wastani wa kukoma kumnyonyesha mtoto wako. Tafuta wakati wa kumpigia simu ya video mwanao, itapunguza mawazo mengi.

kukoma kunyonyesha mtoto

Sababu za kuto komesha kunyonyesha mwanao

  1. Maradhi ya mastitis. Huku ni kufura kwa matiti kunako kufanya uhisi uchungu unapo nyonyesha mtoto. Unahisi umefura. Wakati ambapo uchungu huo huenda ukakufanya usi nyonyeshe, kumlisha mtoto ni njia bora ya kupunguza uchungu na kufura huko.

2. Jaundice. Watoto wanao nyonyeshwa huenda wakaugua jaundice ikilinganishwa na watoto wanao lishwa formula. Lakini usikome kumnyonyesha mtoto wako.

3. Mtoto haonekani analishwa vyema. Ni vigumu kujua kiasi unacho paswa kumnyonyesha mtoto wako. Kwa hivyo, kuwa na uvumilivu hali ya afya ya mtoto wako ita imarika.

Vyanzo: NHS, UK

Soma PiaJinsi Ya Kuboresha Utoaji Wa Maziwa Ya Mama Kwa Njia Asili

Written by

Risper Nyakio