Nini Kinacho Fanyika Unapo Koma Kutumia Mbinu Za Kupanga Uzazi

Nini Kinacho Fanyika Unapo Koma Kutumia Mbinu Za Kupanga Uzazi

Mojawapo ya sababu ambazo mwanamke hukoma kupanga uzazi ni ili atunge mimba. Lakini mbinu za kupanga uzazi za homoni kama vile tembe, IUD, patch, pete na sindano hutumia homoni tofauti kudhibiti kupevuka kwa yai. Kwa hivyo, nini kinafanyika mtu anapo koma kudhibiti uzazi? Huchukua muda kabla ya homoni mwilini kurudi kiwango cha kawaida, na wanawake wanao koma kutumia bidhaa za kupanga uzazi hushuhudia ishara tofauti kabla ya viwango vya uzazi kuji sawasisha na kuwa kawaida. Kukoma kutumia mbinu za kupanga uzazi zisizo za homoni kama vile copper IUD, ama cervical caps hakuta sababisha ishara ama mabadiliko haya.

Mbinu unayo tumia ya kudhibiti uzazi ina athiri muda ambao homoni zita toka mwilini. Baadhi ya mbinu hizi hufanya kipindi chako cha hedhi kukoma, kuadhiri uso wako na uzito wa mwili. Kwa baadhi ya wanawake, huenda waka pata mimba punde tu baada ya kukoma kupanga uzazi, huku wengine wakichukua muda mrefu zaidi.

kukoma kupanga uzazi

Ina chukua muda upi homoni za kupanga uzazi kutoka mwilini?

Homoni za kupanga uzazi huchukua muda tofauti kutoka mwilini baada ya kukoma kutumia mbinu tofauti za kupanga uzazi. Ila kwa wanao tumia shoti ya kuzuia uzalishaji, huchukua muda wa kati ya miezi tatu hadi sita kwa mwili kusawasisha homoni.

Je, kuna uwezo wa kutunga mimba punde tu baada ya kukoma kupanga uzazi?

Kuna uwezekano wa mwanamke kutunga mimba punde tu anapo koma kutumia mbinu za kudhibiti uzalishaji. Yote haya yana lingana na mahali kipindi chake kiko. Baada ya kukoma kutumia tembe, pete ama IUD, homoni za kudhibiti uzalishaji zinakoma kufanya kazi.

Ukikoma kutumia mbinu za kudhibiti uzalishaji kwa sababu tofauti na kupata mimba, kama vile kusawasisha uzito wako wa mwili, ni vyema kutumia mbinu zingine za kupanga uzazi kama kutumia kondomu.

Kukoma Kupanga Uzazi Kuna Athiri Kipindi Chako Cha Hedhi Vipi?

Mbinu za kudhibiti uzalishaji za homoni hufanya kazi kwa njia mbili tofauti kuzuia kupata mimba. Kudhibiti ovulation na kufanya uterasi ikose kuegemeza kujishikilia kwa yai kwenye kuta zake. Mwanamke anapo koma kuzitumia, ovulation ina rudi kuwa kawaida. Mwanamke anapo tumia mbinu za kuzuia kupata mimba, kipindi chake cha hedhi kina athiriwa. Ikiwa ana tumia mbinu za homoni, huenda ikachukua miezi michache kabla ya viwango vya homoni mwilini kurudi kawaida. Na vipindi vinapo rudi, huenda vikawa vyepesi sana ama vingi na vinavyo kaa kwa muda mrefu.

 

Ukikawia sana kupata kipindi chako cha hedhi baada ya kukoma kutumia mbinu za uzalishaji, ni vyema kumtembelea daktari ili adhibitishe kinacho endelea mwilini mwako.

Baada ya kukoma kutumia mbinu hizi, mwili wako utashuhudia mabadiliko ukizoea hali hii mpya. Huenda ukagundua kuwa uso wako una upele, acne, kuumwa na tumbo na PMS. Ama hata kuumwa na kichwa, kufura tumbo na ongezeko ama punguko la uzito wa mwili. Wanawake ni tofauti na ishara zitakuwa tofauti kwa kila mmoja.

kukoma kupanga uzazi

Kukoma kutumia mbinu za kudhibiti uzalishaji za homoni kuna weza athiri viwango vya Vitamini D mwilini. Kupunguka kwa viwango vya vitamini D mwilini kunaweza kuwa na kinga ndogo ya mwili, kufilisika kimawazo, kuhisi uchovu na matatizo ya uzito wa mifupa mwilini. Ili kutunga mimba, vitamini D ni muhimu sana. Ni vyema kuanza kuchukua tembe za vitamini D, lakini hakikisha kuwa umewasiliana na daktari wako kwanza.

Vyanzo: WebMD      Healthline

Soma Pia:Orodha Ya Tembe Za Kukusaidia Kupata Mimba

Written by

Risper Nyakio