Hisia ya kutapika katika mimba husababishwa na ongezeko la homoni za mimba. Kuhisi kichefu chefu na kutapika huwa miongoni mwa ishara za mapema za mimba. Ni ishara ya kawaida na hakuna jambo la kumtia mama kiwewe isipokuwa pale ambapo ana tapika zaidi. Mama anapo gundua kuwa kutapika kwake kumeongezeka ni vyema kuwasiliana na daktari wake kwa kasi. Kuna vitu ambavyo mama anaweza kufanya akiwa nyumbani ili kukomesha kutapika katika mimba.
Jinsi ya kupunguza hisia za kutapika katika mimba
- Kula chakula kidogo mara kwa mara

Badala ya kula chakula kingi cha kiamsha kinywa, chajio ama chamcha, gawanya chakula hicho kwa viwango. Kula chakula kidogo mara zaidi. Hakikisha unakula chakula chenye afya na ujitenge na kula vitamu tamu. Maji ni muhimu sana kwani unapo tapika, unapoteza maji mwilini. Hakikisha unakunywa maji zaidi ya glasi nane kwa siku.
2. Epuka kiungulia
Kiungulia ni chanzo kikubwa kinacho anzisha kutapika na kichefu chefu. Wanawake wengi hutatizika na kiungulia wanapo kuwa na mimba. Kufuatia mabadiliko yanayo fanyika mwilini katika kipindi hiki hasa ya homoni. Kuna dawa za antiacids ambazo mwanamke anaweza kuchukua. Ila ni vyema kuwasiliana na daktari kwani mimba ni nyeti na kuna dawa ambazo huenda zika ibua matatizo.
3. Kuzingatia lishe

Lishe ambayo mama anakula katika kipindi hiki inachangia pakubwa iwapo ata tatizika na kiungulia ama la. Fanya haya ili kupunguza kiungulia.
- Kula crackers ama vyakula vigumu kabla ya kutoka kitandani asubuhi. Hasa zenye chumvi
- Kunywa maji siku nzima na dakika chache kabla ya kulala. Ongeza matunda kwenye maji yako ili kuyapa ladha na kukuwezesha kunywa maji mengi
- Punguza ulaji wa vyakula vyenye pilipili nyingi
- Kula vyakula vyenye viwango vya juu vya protini kabla ya kulala. Kama vile nyama
- Punguza ulaji wa chakula kilicho kaangwa kwenye ufuta mwingi
- Epuka kula chakula chenye harufu kali
- Hakikisha unapasha chakula joto kabla ya kukila. Epuka kula chakula baridi
Unapo jaribu mbinu zote za kukomesha kutapika katika mimba bila kufanikiwa. Ni vyema kuwasiliana na daktari wako. Atakaye fanya vipimo kuhakikisha kuwa hali yako iko sawa.
Chanzo: healthline
Soma Pia: Dalili Za Mimba Ya Mwezi Mmoja Baada Ya Kufanya Tendo La Ndoa!