Jinsi Ya Kukomesha Kuvuja Damu Katika Mimba Na Kujitunza!

Jinsi Ya Kukomesha Kuvuja Damu Katika Mimba Na Kujitunza!

Mwanamke ana stahili kujitunza zaidi anapokuwa mjamzito. Kwani yote anayo yafanya yana athiri afya yake na ya mtoto anaye kua tumboni mwake. 

Kuvuja damu katika mimba ya mapema ni tatizo linalo wakumba wanawake wengi wenye mimba. Kulingana na utafiti ulio fanyika, kila mwanamke mmoja kati ya wanawake wanne huvuja damu katika mimba. Na karibia 1/3 ya wanawake wanao shuhudia tatizo hili hushuhudia kuharibika kwa mimba. Kuharibika kwa mimba ni tatizo lisilo weza kurekebishwa. Ni kawaida kwa mama kujiuliza kuhusu jinsi ya kukomesha kuvuja damu katika mimba.

Kuvuja damu katika trimesta ya kwanza sio tatizo kubwa, ila ni vyema kwenda kwenye kituo cha afya kufanyiwa vipimo. Kuhakikisha kuwa hakuna jambo linalo kusumbua. Hata hivyo, kuvuja damu katika trimesta ya pili ya mimba ni jambo la kutia wasiwasi. Lina dhihirisha kuwepo kwa tatizo sugu.

Tembelea kituo cha afya unapo kumbwa na haya:

kukomesha kuvuja damu katika mimba

  • Kuvuja damu sana na kujaza pedi zaidi ya moja kwa lisaa limoja
  • Maumivu mengi kwenye tumbo
  • Kuhisi kizungu zungu
  • Kutoa harufu mbaya kutoka kwa uke
  • Kuvuja damu katika trimesta ya pili ya mimba

kukomesha kuvuja damu katika mimba

Hatua ya kwanza ya kukomesha kuvuja damu ukiwa mjamzito ni kufanyiwa vipimo ili kufahamu chanzo cha tatizo hilo. Vipimo kama vile cha uke, kipimo cha damu ama kufanyiwa ultrasound.

Huenda kuvuja damu kukawa kutoa matone ya damu na kukadumu kwa siku moja ama siku mbili. Wanawake hujifungua watoto wenye afya hata baada ya kukumbana na tatizo hili.

Baadhi ya wakati, huenda kuvuja damu kukazidi na kusababisha kuharibika kwa mimba. Unapaswa kwenda kwenye kituo cha afya, kwani hakuna njia ya kurekebisha tatizo hili.

Mwanamke ana hitaji matibabu zaidi baada ya kupoteza mima na seli zingine kubaki kwenye uterasi yake.

Kujitunza unapo vuja damu katika mimba

kukomesha kuvuja damu katika mimba

Mwanamke ana stahili kujitunza zaidi anapokuwa mjamzito. Kwani yote anayo yafanya yana athiri afya yake na ya mtoto anaye kua tumboni mwake.

  • Hakikisha kuwa unapumzika vya kutosha
  • Tumia pedi unapo vuja damu
  • Epuka kufanya ngono hadi utakapo wacha kuvuja damu
  • Wasiliana na daktari wako unapo shuhudia ishara zingine

Ni muhimu kufahamu jinsi ya kukomesha kuvuja damu katika mimba na kujitunza. Hakikisha kuwa unakula lishe bora, kupata usingizi unao tosha na kuwasiliana na daktari wako mara kwa mara.

Soma pia: Mbinu 3 Kuu Za Kuzuia Kutunga Mimba (Jinsi Ya Kuzuia Mimba)

Written by

Risper Nyakio