Kuvuja damu katika muhula wowote wa mimba huwa ishara hasi. Mwanamke mjamzito ana haja ya kufahamu jinsi ya kukomesha kuvuja damu katika mimba iwapo litamtendekea. Kuna sababu nyingi zinazomfanya mama kuvuja damu katika mimba. Sababu nyeti na zingine nyepesi zisizo vyanzo vya shaka.
Vyanzo vya kuvuja damu katika mimba

Kuvuja damu katika ujauzito husababishwa na vyanzo tofauti. Kuvuja damu katika trimesta ya kwanza sio chanzo cha shaka, hata hivyo, ni vyema kuzungumza na daktari wako kuhakikisha mimba inakua ipasavyo.
Kuvuja damu katika muhula wa kwanza
1.Kuvuja damu kufuatia implantation: Yai lililokomaa linapopatana na mbegu ya kiume, linarutubishwa. Kisha kujipandikiza kwenye ukuta wa uterasi na mama huvuja damu nyepesi.
2. Ujauzito wa ectopic: Yai linaporutubishwa, linapaswa kupandikiza kwenye mji wa mimba. Yai linapopandikiza nje ya mji wa mimba kama vile kwenye mirija ya ovari. Hali dharura inayomweka mama kwenye hatari ya kupoteza maisha yake.
3. Ujauzito wa molar: Hali isiyo kawaida ambapo yai lililorutubishwa hupandikiza kwenye ukuta wa uterasi kisha uvimbe hukua badala ya fetusi ama mtoto.
4. Kupoteza mimba: Kuvuja damu nyepesi kisha kuzidi kuwa matone kunakoandamana na maumivu makali ya tumbo ni ishara ya kuharibika kwa mimba.
Kuvuja damu katika muhula wa pili na wa tatu

1. Placenta abruption: Hali ambapo placenta hutengana na ukuta wa uterasi. Ni hatari kwa mama na fetusi.
2. Placenta previa: Hali ambapo placenta hufunika kizazi chote. Huonekana katika wiki ya 20 ya ujauzito.
3. Uchungu wa uzazi usiokomaa: Kuvuja damu katika muhula wa tatu huenda kukaashiria kuwa mama ameingia katika uchungu wa uzazi kabla ya wakati kufika. Huambatana na maumivu ya tumbo.
4. Kuharibika kwa mimba: Nafasi za mama kupoteza mimba hupunguka anapopitisha muhula wa kwanza. Hata hivyo, kuna mambo ambayo yanaweza kumfanya kupoteza mimba baada ya wiki ya 20 ya ujauzito kama vile ajali ama kuanguka.
5. Maambukizi: Magonjwa ya zinaa kama chlamydia na gonorrhea yanaweza kumfanya mama kuvuja damu anapokuwa na mimba.
6. Kufanya ngono: Kuna baadhi ya wanawake wanaovuja damu wanapofanya tendo la ngono wakiwa na mimba. Kumbuka kutumia mitindo iliyo salama na isiyomshinikiza mama.
Hakuna jambo ambalo mama anaweza kufanya kukomesha kuvuja damu katika mimba. Anapaswa kuwasiliana na daktari wake ama kutembelea kituo cha afya kasi awezavyo.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Vyanzo Na Suluhu La Kukojoa Mara Kwa Mara Katika Ujauzito