Uzazi wa mpango huwa njia ya kulinda dhidi ya kupata mimba isiyotarajiwa. Kuna mbinu nyingi za kupanga uzazi, kutumia tembe ama IUD. Tembe za uzazi wa mpango huwa na homoni zinazodhibiti mimba kukua. Mbinu za uzazi wa mpango hudhibiti mzunguko wa hedhi na kipindi cha hedhi kwa miezi ya kwanza kabla ya mwili kuzoea. Mwanamke huenda akakosa kupata kipindi cha hedhi ama kupata kipindi chepesi kuliko ilivyo kawaida. Kipi kinachosababisha kukosa hedhi baada ya kutumia uzazi wa mpango?
Kukosa hedhi baada ya kutumia uzazi wa mpango
- Kubadili lishe

Kubadili lishe kunaweza kukaathiri hedhi. Kwa mfano kutoka nchi moja hadi nyingine na kubadili vyakula ulivyozoea huenda kukafanya kipindi cha hedhi kupotea kwa muda. Kubadili hedhi na kupoteza uzito wa mwili kwa kasi pia kunaweza kusababisha hedhi kupotea kwa muda.
2. Kufanya mazoezi

Kufanya mazoezi magumu isivyo kawaida kutaathiri utenda kazi wa kawaida mwilini na kufanya kipindi cha hedhi kipotee kwa muda. Ikiwa unaanza kufanya mazoezi, anza kwa mazoezi mepesi hadi mwili wako utakapozoea. Wanariadha waliozoea kufanya mazoezi magumu huenda wakakumbana na tatizo hili hasa wanapofanya mazoezi ya kujitayarisha kuenda mashindano.
3. Kusombwa na mawazo

Kuwa na mawazo mengi huathiri mwili na ubongo na kufanya iwe vigumu kudhibiti vichocheo mwilini. Kugundua chanzo cha mawazo na kukitatua kutasaidia kusawasisha hedhi.
Kupata mimba ukipanga uzazi
Ni nadra kupata mimba unapokuwa ukitumia uzazi wa mpango. Ikiwa una panga uzazi na kugundua kuwa hujapata kipindi cha hedhi kama ilivyo kawaida, wasiliana na mtaalum wa afya. Ili kuangalia iwapo kuna suala la kiafya linalokutatiza ama una mimba.
Jinsi ya kuhakikisha kuwa hedhi ni ya kawaida
Kukosa kipindi cha hedhi ukitumia uzazi wa mpango sio ishara kuwa una mimba. Mbali, vichocheo mwilini havijasawasishwa. Hata hivyo ni muhimu kuzungumza na daktari ili kuhakikisha kuwa vitu vyote viko sawa. Unaweza kuzingatia vitu hivi:
1. Kufanya mazoezi mara kwa mara. Kunasaidia kusawasisha vichocheo mwilini.
2. Kupunguza mawazo mengi. Kwa kufanya mazoezi mepesi ama yoga, kutembea kwa dakika chache ama kukandwa mwili.
3. Kula lishe yenye afya. Inasaidia kudumisha uzito wa mwili wenye afya. Ikiwa unatatizika kula, wasiliana na daktari wako.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Vitu 6 Vinavyosababisha Kuumwa na Tumbo Bila Hedhi