Sababu kwa nini utakuwa na kipimo hasi cha mimba hata baada ya kukosa kipindi cha hedhi. Kuna sababu chache ambazo huenda zika athiri mambo haya.
Kipimo hasi cha mimba na kukosa kipindi cha hedhi
- Viwango vya chini vya homoni
Ikiwa una jaribu kutunga mimba, huenda bado ukawa mjamzito. Viwango vya chini vya homoni ya HCG(human chorionic gonadotropin) kwenye mkojo huenda ikafanya iwe vigumu kudhibitisha matokeo chanya ya kipimo chako cha mimba.
Kutumia mbinu ya kupanga uzazi yenye homoni ama kuvuja damu kwa mimba, na kunyonyesha huenda kuka athiri matokeo ya kipimo chako. Ikiwa una shaka kuwa huenda ukawa na mimba baada ya kupata matokeo hasi kwenye kipimo chako, ni vyema kungoja siku chache kabla ya kupima tena.

Hata kama ni nadra, mwanamke anapo kuwa na mimba ya aina hii huenda kipimo chake kikaonyesha matokeo hasi. Ukishuhudia ishara hizi na kipimo chako kizidi kuonyesha matokeo hasi, wasiliana na daktari wako.
- Kuhisi kizungu zungu
- Kuvuja damu
- Uchungu mwingi kwenye tumbo ama upande mmoja
- Kichefu chefu na kutapika
Mama anapo nyonyesha, huenda mzunguko wake wa hedhi uka athiriwa. Itachukua muda kurudi kwa utaratibu wa mzunguko wako wa hapo awali. Hii ni kwa sababu kunyonyesha mtoto hutofautiana kila mwezi.

Sababu nyingi zinazo husika na mtindo wako wa maisha huenda zika sababisha kipindi chako cha hedhi kuchelewa. Kama vile mawazo mengi, chakula duni na kunywa kaffeini nyingi huenda kuka athiri mzunguko wako wa hedhi.
Kubadili mitindo yako ya maisha kwa kasi huenda kuka athiri utaratibu wa mzunguko wako wa hedhi. Kama vile kuhusisha mazoezi magumu kwenye ratiba yako ya kila siku, kubadili mazingira yako ama kubadili lishe yako.
Mwanamke anapo kuwa akitatizika na hali za kiafya, huenda kipindi chake cha hedhi kikachelewa. Magonjwa kama vile PCOS (polycystic ovary syndrome). Mwanamke anapo fikisha miaka yake ya ugumba, kipindi chake cha hedhi hukoma. Unapo kaa mwaka mmoja bila kupata vipindi vyako vya hedhi, umeingia katika miaka ya ugumba.
Soma Pia: Ni Kawaida Kuwa Na Hedhi Ukiwa Na Mimba?