Kukosa usingizi kwa mjamzito ni jambo linaloshuhudiwa kwa sana katika safari ya ujauzito. Hasa katika muhula wa mwisho wa mimba, mama mjamzito huwa na vipindi virefu vya kukosa usingizi. Kuna sababu tofauti zinazosababisha hali hii.
Kukosa usingizi kwa mjamzito huchangiwa na:

1. Maumivu ya sehemu za mwili kama mgongo na miguu kufuatia kukua kwa mimba na kulegea kwa ligaments
2. Kuhisi hamu ya kwenda msalani mara kwa mara. Kuamka baada ya kila dakika chache usiku hufanya usingizi kupotea na vigumu kulala tena
3. Mapigo ya mtoto tumboni, huenda yakafanya mama atatizike kulala
4. Baadhi ya wanawake hutatizika kutokana na hali ya kiungulia katika mimba, hii ni sababu nyingine ya mama mjamzito kukosa usingizi
5. Katika trimesta ya tatu, utoaji wa kichocheo cha estrogen mwilini huongezeka na kuathiri uwezo wa mama wa kulala vyema usiku
6. Mimba inavyozidi kukua, ndivyo inavyokuwa vigumu kwa mama kulala kwa upande mmoja. Na kumfanya ahisi maumivu na iwe vigumu kwake kulala
7. Mjamzito anapokula chakula kingi kabla ya kulala, huenda akatatizika kupata usingizi
8. Katika muhula wa tatu na wa mwisho wa ujauzito, mjamzito huenda akawa na mawazo na shaka kuhusu kujifungua kwake na kumfanya akose kupata usingizi
Jinsi ya kuboresha usingizi katika ujauzito

1.Ili kulala vyema zaidi wakati wa ujauzito, mama aliye na mimba anashauriwa kufanya haya:
2. Kufanya mazoezi mepesi. Matembezi huwa magumu japo mimba inavyozidi kukua. Mazoezi husaidia kupunguza maumivu ya mwili na kumwezesha mama kulala vizuri usiku
3. Kutengeneza ratiba ya kulala. Awe na wakati maalum wa kuingia kitandani na kuamka
4. Kutumia mto wa wajawazito na kuuweka katikati ya miguu humsaidia mama kulala vyema zaidi
5. Kuepuka kutumia simu na vifaa vingine vya kielektroniki usiku
6. Kuepuka kunywa vinywaji vilivyo na kaffeini kama soda na kahawa usiku kabla ya kulala
7. Kutokula chakula kingi muda mfupi kabla ya kuingia kitandani
8. Kuhakikisha kuwa chumba cha kulala ni kisafi, kimetulia na hakina mwangaza mwingi usiku
Soma Pia: Mabadiliko Mwilini Mama Anapokuwa Na Mimba Ya Mwezi Mmoja