Kukosa usingizi kwa watu wazee husababishwa na sababu tofauti. Kadri tunavyozidi kuzeeka, ndivyo mwili unavyozidi kubadilika na viwango vya homoni mwilini kubadilika pia. Kiwango cha homoni ya ukuaji ama kwa kimombo growth hormone hupungua mwilini na usingizi kupungua. Kichocheo cha melatonin kinachoathiri uwezo wa kuamka na kulala hupungua na uwezo wa kulala unono kuathirika.
Hata hivyo, ni muhimu kukumbuka kuwa tatizo la kukosa usingizi ama kutatizika kulala huwakumba watu walio katika umri wowote maishani. Baadhi ya dalili za kutatizika na usingizi ni kama vile:
- Kutumia tembe za kupata usingizi
- Kutatizika kuwa makini kazini
- Kulala ofisini ama darasani
- Kuamka na uchovu mwingi asubuhi
- Kutatizika kupata usingizi baada ya kuamka katikati ya usiku
- Kulala sana mchana
Baadhi ya mambo yanayochangia kukosa usingizi kwa watu wazee

Kukosa usingizi usiku husababishwa na sababu tofauti. Baadhi ya sababu hizi ni kama vile kuwa na sononi ama depression, kusongwa na mawazo, mazingira ya kulala kubadilika, shughuli zake za mchana, kuchukua vinywaji vinavyopoteza usingizi kama kafeini. Pia, kuna dawa za kiafya zinazofanya iwe vigumu kupata usingizi usiku.
Maswali yafuatayo yanaweza kusaidia kufahamu chanzo cha kukosa usingizi kwako.
- Je, kuna dawa zozote unazotumia ambazo huenda zinakufanya kukosa usingizi?
- Je, una matatizo ya kiafya ambayo huenda yakawa yanachangia ukosefu wa usingizi?
- Je, kuna tukio la kimaisha ambalo limefanyika linalokuathiri?
- Je, una mawazo mengi yanayokutatiza kulala?
- Je, una songwa kimawazo?
Sababu za kukosa usingizi kwa watu wazee
- Kukosa utaratibu mzuri wa kulala
- Mazingira yasiyo mazuri ya kulala
- Matumizi ya dawa za kiafya
- Kukosa muda hasa wa kulala
- Kunywa pombe viwango vya kupindukia
- Kunywa pombe kabla ya kulala
- Kutazama runinga kitandani
- Kutumia simu wakati unaopaswa kuwa ukilala
- Maumivu ya kimwili
Jinsi ya kuboresha uwezo wa kulala vyema usiku

Kwa watu wenye umri zaidi, wanapaswa kuota jua kwa muda zaidi. Angalau masaa mawili ya mwanga kila siku
- Hakikisha kuwa unafanya mazoezi kwa angalau dakika 30 kila siku. Mazoezi husaidia na utoaji wa homoni za endorphins zinazosaidia kupunguza mawazo na kukusaidia kulala vyema zaidi
- Epuka unywaji wa kafeini na pombe muda mfupi kabla ya kulala. Vinywaji hivi huwa bora unapovichukua asubuhi ama mchana
- Zungumza na daktari wako iwapo unachukua dawa zozote za kiafya kufahamu athari hasi zake na iwapo zinachangia katika ukosefu wa usingizi
- Hakikisha kuwa mazingira ya chumba chako cha kulala yanaboresha kupata usingizi kirahisi. Kama vile kutokuwa na muziki wa juu chumbani, kutumia blanketi safi. Epuka matumizi ya runinga na simu chumbani cha kulala
- Mbali na hayo, ni vyema kuepuka kula chakula kingi dakika chache kabla ya kulala. Ili kuupa mwili muda tosha wa kuchakata chakula hicho.
Chanzo: WebMD
Soma Pia:Tatizo la Kukosa Usingizi Linasababishwa Na Nini Hasa?