Africaparent Logo
Africaparent Logo
EnglishSwahili
  • COVID-19
  • Becoming a Mama
  • Ages & Stages
  • Parenting
  • Health
  • Feeding & Nutrition

Kukwazwa Kimawazo Ukiwa Na Mimba Na Matibabu Yake

2 min read
Kukwazwa Kimawazo Ukiwa Na Mimba Na Matibabu YakeKukwazwa Kimawazo Ukiwa Na Mimba Na Matibabu Yake

Kulingana na utafiti uliofanyika, kati ya asilimia 14 na 23 za wanawake hushuhudia fikira nyingi wakiwa na mimba.

Neema mwenye miaka 28 alijipata akilia mara kwa mara na kushuhudia mhemko wa hisia, kuhisi uchovu alipokuwa katika trimesta yake ya pili ya mimba. Alipuuza ishara hizi za kukwazwa kimawazo katika mimba na kudhani kuwa zilisababishwa na mabadiliko ya homoni. Kama mama wa mara ya kwanza, Neema alienda kumwona daktari wake aliye gundua mabadiliko katika mhemko wake na hisia zake kwa jumla. Alizidi kupuuza ishara hizi kama kukwazwa kimawazo kwa kila siku na kama kuwa sehemu ya ujauzito.

Alipofika katika trimesta ya tatu, Neema alikuwa na hisia nyeti kwa kila kitu karibu naye na tena hange puuza ishara hizi. Daktari wake alipomwuliza anachofanya kila siku, alihisi kana kwamba anamkemea. Alianza kutatizika na urafiki wake na watu wengine, na kujipata akilia kila wakati.

Kukwazwa kimawazo katika mimba

kukwazwa kimawazo katika mimba

Kulingana na utafiti uliofanyika, kati ya asilimia 14 na 23 za wanawake hushuhudia fikira nyingi wakiwa na mimba. Lakini, imani zisizo za kweli kuhusu mimba, kujifungua na fikira nyingi katika kipindi hiki huifanya iwe vigumu kwa wanawake kupata majibu. Alisema daktari mmoja aliye husika katika utafiti huo.

Chanzo kikubwa ni kuwa, wanafamilia huwashauri wanawake wenye mimba kupuuza ishara hizo na kuwa sio jambo kubwa. Jamii kwa ujumla hufikiria kuwa mimba na kupata mtoto ni kipindi chenye furaha zaidi katika maisha ya mwanamke. Hata kama wanawake hushuhudia hisia nyingi tofauti katika wakati huu.

Habari njema ni kuwa, kuna matibabu ya fikira nyingi katika ujauzito, kulingana na daktari wa saikolojia, Catherine Monk kutoka Chuo Kikuu cha Columbia. Unaweza chukua tembe za antidepressants kama vile (SSRIs) Selective serotonin reuptake inhibitors.

ndoto mbaya wakati wa mimba

Fikira nyingi baada ya kujifungua

Ni vigumu kwa suala hili kutatuliwa mara moja. Kwa hivyo, nafasi kubwa ni kuwa, mwanamke aliye tatizika na fikira nyingi katika mimba atazidi kuhisi hivyo hata baada ya kujifungua. Mara nyingi, huenda mama akakosa kuhisi utangamano kati yake na mtoto wake baada ya kujifungua. Mara nyingi utapata mama akilia bila kikomo baada ya kujifungua na kuhisi uwoga mwingi, na hofu ya kubaki peke yake na mtoto.

Kupata tiba

Kukwazwa kimawazo katika mimba hutendeka, kwa hivyo mama hapaswi kuhisi lawama kwa kukosa kumpenda mtoto wake asilimia 100 kama vile ambavyo watu wange tarajia. Usione aibu kuenda hospitalini kupata tiba, kwani afya yako ya kifikira ni muhimu sana.

Soma Pia: Maisha Baada Ya Mtoto Kuwasili: Mambo Ambayo Hukufahamu!

Got a parenting concern? Read articles or ask away and get instant answers on our app. Download theAsianparent Community on iOS or Android now!

img
Written by

Risper Nyakio

  • Home
  • /
  • Health
  • /
  • Kukwazwa Kimawazo Ukiwa Na Mimba Na Matibabu Yake
Share:
  • Ni Kawaida Kuwa Na Hedhi Ukiwa Na Mimba?

    Ni Kawaida Kuwa Na Hedhi Ukiwa Na Mimba?

  • Kulala Sana Ukiwa Na Mimba Ni Salama Kwa Mama Na Mtoto Ama La?

    Kulala Sana Ukiwa Na Mimba Ni Salama Kwa Mama Na Mtoto Ama La?

  • Kwa Nini Napoteza Uzito Nikiwa Na Mimba?

    Kwa Nini Napoteza Uzito Nikiwa Na Mimba?

  • Sababu 3 Za Kuvuja Damu Katika Mimba

    Sababu 3 Za Kuvuja Damu Katika Mimba

  • Ni Kawaida Kuwa Na Hedhi Ukiwa Na Mimba?

    Ni Kawaida Kuwa Na Hedhi Ukiwa Na Mimba?

  • Kulala Sana Ukiwa Na Mimba Ni Salama Kwa Mama Na Mtoto Ama La?

    Kulala Sana Ukiwa Na Mimba Ni Salama Kwa Mama Na Mtoto Ama La?

  • Kwa Nini Napoteza Uzito Nikiwa Na Mimba?

    Kwa Nini Napoteza Uzito Nikiwa Na Mimba?

  • Sababu 3 Za Kuvuja Damu Katika Mimba

    Sababu 3 Za Kuvuja Damu Katika Mimba

Get advice on your pregnancy and growing baby. Sign up for our newsletter
  • Becoming a Mama
    • Pregnancy
    • Delivery
    • Losing a Baby
  • Ages & Stages
    • Baby
    • Toddler
    • Kids
  • Parenting
    • News
    • Relationship & Sex
    • Parent's Guide
  • Health
    • Allergies & Conditions
    • Vaccinations
    • Diseases-Injuries
  • Feeding & Nutrition
    • Breastfeeding & Formula
    • Latching & Concerns
    • Weaning
  • More
    • TAP Community
    • Advertise With Us
    • Contact Us
    • Become a Contributor


  • Singapore flag Singapore
  • Thailand flag Thailand
  • Indonesia flag Indonesia
  • Philippines flag Philippines
  • Malaysia flag Malaysia
  • Sri-Lanka flag Sri Lanka
  • India flag India
  • Vietnam flag Vietnam
  • Australia flag Australia
  • Japan flag Japan
  • Nigeria flag Nigeria
  • Kenya flag Kenya
© Copyright Africaparent.com 2022 Tickled Media Pte Ltd. All rights reserved
About Us|Team|Privacy Policy|Terms of Use |Sitemap HTML

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it