Kitu cha kwanza ambacho mama anapaswa kuwa makini zaidi nacho baada ya kufahamu kuwa ana mimba ni lishe yake. Huu sio wakati salama kwake kuanza kuvijaribu vyakula vipya. Huenda akawa na mvio kwa vyakula fulani, kula vyakula vilivyo salama. Je, ni salama kula mboga katika ujauzito?
Faida za mboga katika ujauzito

Lishe bora na yenye afya ni muhimu katika ujauzito. Chagua chakula bora, na viwango tosha, visivyo vingi kupindukia ama vidogo sana. Kula vyakula visivyo vyenye afya kuna hatarisha maisha ya mama pamoja na ya mtoto. Mboga huwa na madini na virutubisho muhimu ambavyo vinamfaa mama katika ujauzito. Mboga zinasifika kwa kuwa na wingi wa vitamini C na folic acid.
Chakula ambacho mama anakula anapokuwa na mimba kinasaidia mtoto kuwa na afya hata baada ya kuzaliwa. Mtoto anaye zaliwa na mama anaye tunza afya yake katika ujauzito hatatatizika na afya yake katika maisha ya usoni. Anapo zaliwa, mtoto ana uzani wenye afya, na hana matatizo ya kupungukiwa na damu mwilini. Nafasi zake za kuwa na matatizo ya afya kama kisukari ama uzito wa kupindukia hupunguka kwa asilimia kubwa.
Aina ya mboga zilizo muhimu katika ujauzito

Ina wingi wa vitamini K, C na folate. Inasaidia katika kukabiliana na tatizo la kuvimbiwa ama kifunga choo.




Kuna idadi ya mboga iliyo nyingi zaidi?
Mama anapokuwa na mimba huhisi njaa sana na anapaswa kula mara kwa mara ili kutosheleza mahitaji yake na ya mtoto. Kukula hivi kunapunguza nafasi ya kuhisi kichefu chefu na matatizo yoyote yanayo husiana na mfumo wa kuchakata chakula. Hakuna kiwango kilicho kingi sana cha mboga kwa mama mjamzito. Hata hivyo ni salama kujiepusha na ulaji wa mboga zilizo kwenye pakiti. Tayarisha chakula freshi na safi.
Jitenge na ulaji wa chakula mbichi. Safisha mboga vizuri kabla ya kuzitayarisha. Kiwango cha mboga kinacho shauriwa kwa kila siku ni gramu 500. Jaribu kupika mboga zako kwa njia tofauti ili zivutie zaidi. Kama vile kuoka, ama kuchanganya na mchuzi unaopendelea zaidi. Ni muhimu kula mboga katika ujauzito, kuboresha afya ya mama na mtoto.
Chanzo: WebMD
Soma Pia:Vyakula Muhimu Katika Lishe Ya Mama Mjamzito