Mambo 3 Unayo Hitaji Kujua Kuhusu Wanga Katika Mimba

Mambo 3 Unayo Hitaji Kujua Kuhusu Wanga Katika Mimba

Kudhibiti kiwango cha wanga unacho kula na kukigawanya siku yote kunasaidia kudhibiti viwango vya glukosi ya damu katika mimba.

Hannah May Brown ni mtaalum wa lishe katika Chuo Kikuu cha Newcastle, na anatueleza yote tunayo faa kujua kuhusu kula wanga katika mimba.

1. Usiepuke kula wanga katika mimba

Lishe bora ya mama mjamzito

 

Wanga ni muhimu sana kwa mama na mtoto kwani ni chanzo cha nishati na haupaswi kuepukwa katika mimba. Hakikisha kuwa unazidi kula wanga, ili kuwa makini na aina ya wanga unayo kula na kiwango unacho kula kwa siku.

Wanga ni mojawapo ya vyakula vinavyo tengeneza mazoea yenye afya kwa wanawake wenye mimba. Zinapatia mwili na ubongo nishati inayo hitajika kutenda kazi ifaavyo. Vyakula vingi vyenye afya vyenye wanga ya juu kama vile mkate, ni chanzo kizuri cha virutubisho muhimu kwa wamama wenye mimba, kama vile fibre, iodine na folate.

2. Wanga haipatikani kwa mkate na pasta tu

kula wanga katika mimba

Wanga unapatikana kwa vyakula vingi na vinywaji na sio kwenye aina fulani tu ya nafaka. Vyakula kama maziwa na maziwa ya bururu, matunda, mboga, maharagwe huwa na idadi kubwa ya wanga. Vyakula hivi, ambavyo vina virutubisho vingi na ni nzuri kwa afya vina fahamika kama wanga ya ubora wa juu.

Bila shaka kuna baadhi ya vyakula na vinywaji ambavyo vina wanga isiyo nzuri kwetu. Vyakula hivi huwa vime chakatwa sana na vina nishati nyingi na virutubisho vichache mno. Hivi ni kama vile biskuti, keki, chokleti na soda.

Ushauri ni uchague vyakula vya wanga wa ubora mwingi kama vile nafaka nzima, oats, maziwa ya bururu, na mboga.

3. Idadi ya wanga unayo kula ukiwa na mimba ni muhimu

Ni muhimu kufikiria kuhusu aina ya chakula cha wanga unacho kula. Pia ni muhimu kufikiria kiwango cha chakula na kinywaji hicho unacho kunywa ama kula. Hii ni kwa sababu chakula kilicho na wanga hu mmeng'enywa na kuwa glukosi inayo tumika kwenye mishipa ya damu. Na kufanya viwango vyako vya sukari ya damu kuongezeka.

Kudhibiti kiwango cha wanga unacho kula na kukigawanya siku yote kunasaidia kudhibiti viwango vya glukosi ya damu katika mimba. Viwango vya juu vya sukari kwenye damu inaweza sababisha kisukari na kuwa na athari hasi kwako na mtoto wako.

Athari hizi hasi ni kama vile kujifungua kabla ya wakati, mtoto mwenye uzito mwingi na hatari ya matatizo ya kujifungua. Kwa sababu ya haya, ni muhimu kudhibiti kiwango cha wanga unacho kula katika mimba.

Soma Pia:Kutengeneza ratiba mwafaka ya lishe nyumbani nchini Kenya

Written by

Risper Nyakio