Kulala Katika Mimba: Mabadiliko Unayo Paswa Kutarajia Katika Usingizi Wako

Kulala Katika Mimba: Mabadiliko Unayo Paswa Kutarajia Katika Usingizi Wako

Changamoto za kulala katika mimba hulingana na trimesta uliyoko. Tazama mambo ya kufanya ili kuwa na usiku mwema na kufurahia usingizi wako ukiwa na mimba.

Ujauzito baadhi ya wakati huja na mabadiliko katika ubora wa usingizi ambao mwanamke hupata kila siku. Changamoto za kulala katika mimba hulingana na trimesta. Unaweza furahia kulala vyema katika trimesta ya kwanza na unapo fika ya pili upate kuwa ni vigumu sana kulala.

Mwili wako unapo pitia utaratibu wa kukua na kutunza mtoto, utapata kuwa kuna mabadiliko mengi ya kuishi nayo, kama vile matatizo ya kulala katika mimba. Tuna angazia mabadiliko unayo tarajia na jinsi ya kupambana nayo.

Kulala katika mimba: Kwa nini mambo yote ni tofauti?

Uchovu katika hatua hii ya maisha ina sababishwa na homoni na mwili wako unao kua kwa kasi. Homoni za mimba zinaweza kufanya uhisi kuchoka, kutapika, kukasirika ovyo na mwenye hisia nyingi. Kadri ujauzito unavyo endelea kukua, utakuwa mkubwa zaidi, na kufanya iwe vigumu kupata mtindo wa kulala wenye starehe.

Mara nyingi, unapo zoea na kupata njia ya kulala yenye starehe, kwenda msalani mara kwa mara kutakufanya uamke kitandani kwenda msalani na kurudi. Mwendo huu wa kutoka na kurudi uta athiri ubora wa usingizi wako. Kuto pata usingizi tosha kunaweza fanya ujauzito wako uwe mgumu kuliko inavyo paswa kuwa.

Kulala katika mimba: Mabadiliko unayo tarajia katika trimesta ya kwanza

kulala katika mimba

Kulingana na NHS, kila trimesta itakuwa na matatizo binafsi ya kulala. Hii ni kwa sababu ujauzito wako unavyo zidi kukua, mwili wako hufanya mambo tofauti katika kila hatua ili kumpatia mtoto anaye endelea kukua nafasi ya kuishi.

  1. Matatizo ya kulala katika trimesta ya kwanza

Kuhisi usingizi mchana

Kuamka mara nyingi kwenda msalani

Matatizo ya kulala kufuatia fikira nyingi za kifizikia na kihisia zinazo andamana na ujauzito

2. Matatizo ya kulala katika trimesta ya pili

Katika trimesta ya pili, mwanamke anaweza pata usingizi bora kwa sababu mtoto hayuko juu ya kibofu cha mkojo. Mtoto amekua na akasonga juu, kwa hivyo shinikizo na haja ya kwenda msalani mara kwa mara haiko.

Walakini, kuna uwezekano wa kutatizika na kukosa usingizi kwa sababu ya mabadiliko ya homoni na ya kifizikia.

3. Matatizo ya kulala katika trimesta ya tatu

Hiki ndicho kipindi kigumu zaidi inapo fika kwa kulala katika ujauzito. Matatizo ya kulala husababishwa na:

Saizi ya ujauzito

Kukojoa mara kwa mara kwa sababu mtoto ni mkubwa na anasonga mara kwa mara

Kuumwa na miguu, kiungulia na matatizo ya sinus

Je, unapaswa kulala vipi ukiwa na mimba?

Kabla ya kupata mimba, ungelala kwa njia yoyote ile bila kuwa na shaka zozote. Kwa sasa kwani una mimba, kulala kwa njia fulani hakuta kosa starehe tu, mbali huenda kukawa sio salama kwa mtoto wako.

Kwa starehe na afya yake, mtindo bora wa kulala ukiwa na mimba ni kulala kwa upande. AmericanPregnancy.org ina shauri kulala kwa upande wa kushoto ni bora zaidi. Kwani inakubalisha mzunguko wa damu na virutubisho kwenye placenta yako kwa urahisi.

Kulala kwa pande kuna starehe hasa ukikunja miguu kisha uweke mto kati kati. Pia unaweza weka mto chini ya tumbo yako ukiwa kwa mtindo huo wa kulala.

Kulala kwa mgongo ukiwa na mimba

kulala katika mimba

Kulingana na NHS, kulala kwa mgongo wako baada ya wiki 28 ya ujauzito, huenda kuka ongeza nafasi zako za kuwa na stillbirth, ama mtoto kuaga kabla ya kujifungua. Hii ni kwa sababu kulala kwa mgongo ukiwa na mimba, huenda kuka katiza mzunguko wa damu na hewa kwa mtoto wako.

Ukiamka usiku wa maanani ujipate umelala kwa mgongo, pinduka kwa kasi na ulale kwa mgongo.

Kulala kwa tumbo

Kulala kwa tumbo huenda kukawa hakuna starehe hasa ujauzito wako ukiwa umekua sana. Pia sio salama kwako wala kwa mtoto.

Jinsi ya kulala vyema ukiwa na mimba

WebMD ime orodhesha vidokezo vichache ambavyo vinaweza kusaidia kulala vyema ukiwa na mimba kama vile:

  • Kula wanga

Vyakula vilivyo na wingi wa wanga vinaweza boresha kulala vyema ukiw ana mimba. Unapaswa kula mkate, wali, mihogo na vyakula vingine vyenye wanga wenye afya.

  • Kula protini

Protini zinausaidia mwili wako kudhibitisha sukari ya damu yenye afya na inaweza kuepusha kuwa na ndoto mbaya ama kuumwa na kichwa.

  • Mito inaweza saidia

Mito ya ujauzito kufanya kulala kwako kuwe rahisi zaidi. Unapaswa kuweka mito chini ya mgongo na tumbo yako na kati kati ya miguu yako.

  • Kufanya mazoezi

Mazoezi na usingizi mwema yana tangamana. Unapo fanya mazoezi, mwili wako hutoa endorphins ambazo ni homoni za furaha. Endorphins huboresha mhemko wako na usingizi wako hata ukiwa na mimba. Walakini, hakikisha kujadili ratiba yako ya mazoezi na daktari wako ukiwa na mimba.

  • Mbinu za kupumzika

Mbinu za kupumzika kama vile yoga na masi zinaweza kutuliza misuli yako na kukusaida kulala vyema.

Vitu vinavyo athiri usingizi katika mimba.

  • Kunywa maji ukiwa karibu kulala
  • Kunywa kaffeini
  • Lishe dhaifu

Usingizi mwema ni mojawapo ya changamoto ambazo wanawake wajawazito hupata. Kuhakikisha kuwa unapata usingizi tosha, tume orodhesha vidokezo vya kulala katika ujauzito kwa kila trimesta. Ili kukusaidia kujua mambo ya kutarajia na jinsi ya kuwa na usingizi mwema.

Je, una vidokezo zaidi vya jinsi ya kulala vyema ukiwa na mimba? Tujulishe kwa kuwacha ujumbe mfupi.

Vyanzo: American Pregnancy

NHS

WebMD

Soma pia:Vidokezo Muhimu Kwa Mama Mwenye Mimba

Written by

Risper Nyakio