Kulala Sana Ukiwa Na Mimba Ni Salama Kwa Mama Na Mtoto Ama La?

Kulala Sana Ukiwa Na Mimba Ni Salama Kwa Mama Na Mtoto Ama La?

Kulingana na utafiti, mama mwenye mimba anapaswa kuhakikisha kuwa anapata usingizi tosha kila usiku, angalau masaa 8.

Katika darasa za utunzaji kabla ya kujifungua, wakunga na madaktari wa afya ya kike hujadili mabadiliko katika mfumo wako wa usingizi ukiwa mjamzito. Hii ni kwa sababu wanawake wengi wana kanganywa na mara nyingi kutiwa wasiwasi na kiwango cha uchovu na kulala wanacho shuhudia katika trimesta ya kwanza ya ujauzito. Huenda wanawake wengine wakashangaa kwa nini wana shuhudia usingizi mwingi katika ujauzito. Je, ni salama kulala sana ukiwa na mimba?

Hakuna anaye fahamu kwa nini wanawake wajawazito huhisi kuchoka. Wataalum wengi wa matibabu husema kuwa mabadiliko kwa kasi ya homoni, shinikizo la chini la damu, shukrani kwa mimba na kisukari huenda zikawa changia katika kulala kwingi katika mimba.

Ujauzito unapo fika trimesta ya pili, huenda mwanamke akahisi wingi wa nishati mpya mwilini. Muundo wake wa kulala utarudi kuwa kawaida. Lakini mambo huenda yaka badilika anapo fika katika trimesta ya tatu. Kuchoka kifizikia na kuhisi kulala wakati wote kunaweza rudi. Kuna sababishwa na uchovu na fikira nyingi za kubeba uzito wa mtoto. Yote haya yatafanya iwe vigumu kwa mwanamke kufurahia usingizi wake usiku ambao ni muhimu sana ili kuwa na ujauzito wenye afya.

Sababu Kwa Nini Hupaswi Kuwa Na Shaka Kuhusu Kulala Sana Ukiwa Na Mimba

how to prevent oversleeping

Kulingana na The National Health Research Institute, wanawake wenye mimba wana hitaji masaa mengi ya kulala vyema usiku. Na masaa 8 hadi 10 yana shauriwa. La sivyo, kulala mchana kunaweza simamia. Lakini kutolala vya kutosha kuna weza hatarisha maisha ya mwanamke. Kunaweza sababisha shinikizo la juu la damu, kukosa usingizi, pre-eclampsia na changamoto zingine.

Wanawake wajawazito wanao lala vyema wana nafasi chache za kupata mawazo mengi na kuwa na uwoga wa ujauzito ama kukwazwa kimawazo. Kupata usingizi tosha katika ujauzito kunaweza boresha mhemko wa mwanamke. Wanawake wengi wajawazito hukiri kukasirika ovyo na kuto kuwa makini wasipo pata usingizi tosha.

Kwa hivyo kulala sana ukiwa na mimba sio jambo mbaya.

"Wanawake wanahitaji kupata usingizi mwingi wakiwa wajawazito kuliko walivyo fanya kabla ya kupata mimba," alisema Felicia Jang, mkuu wa wakunga katika hospitali kuu ya Federal Teaching.

Vidokezo vya kuboresha ubora wa usingizi ukiwa na mimba

  1. Lala kwa upande wako wa kulia

Kulala Sana Ukiwa Na Mimba Ni Salama Kwa Mama Na Mtoto Ama La?

Mtindo wa kulala ulio bora kwa wanawake wengi wajawazito ni ifuatavyo: lala kwa upande wako wa kulia, huku ukiwa umekunja magoti yako kidogo. Kulingana na Jang ambaye ni mkunga, wanawake wajawazito wanapaswa kulala na upande wao wa kushoto. Kwa njia hii wana weka shinikizo kidogo kwenye mioyo yao.

2. Panga, uwe na programu na upe usingizi kipau mbele

Madaktari wana shauri kuwa wanawake wajawazito waende kulala mapema ili wapate angalau masaa manane ya kulala. Lengo ni kusaidia mwanamke kupata hadi masaa 7 ya usingizi na kwa kesi hiyo, kulala kwingi kuna shauriwa. Panga usingizi wako. Tengeneza programu ama ratiba halisi ya kulala. Chukua hatua kukusaidia kuhakikisha kuwa unapata kiwango tosha cha usingizi.

3. Fanya mazoezi

Husisha dakika 30, mazoezi mepesi katika ratiba yako ya kila siku. Kufanya mazoezi hakusaidii na mzunguko wa damu tu, lakini yatasaidia kuupa moyo wako nguvu. Kabla ya kuanza mazoezi, wasiliana na daktari ama mkunga wako akuruhusu.

4. Kunywa maji tosha

Kunywa maji mengi masaa mawili kabla ya kwenda kulala. Kula matunda yenye maji mengi pia. Mifano ni kama vile tikiti maji, machungwa, mananasi na papai. Kunywa ugili gili huu masaa machache kabla ya kulala ili usingizi wako usisumbuliwe na kuamka kwenda haja ndogo.

5. Epuka vyakula vinavyo sababisha kiungulia

Wanawake wengi hukumbana na tatizo la kiungulia wakiwa na mimba. Ikiwa wewe ni mmoja wao, chukua hatua kuepuka kukula zaidi. Badilisha lishe yako. Epuka vyakula vilivyo na pilipili nyingi. Kufanya uamuzi mzuri kunaweza boresha ubora wa usingizi wako kwa asilimia 50%.

6. Kuoga na maji moto

Kuoga na maji moto kunaweza kusaidia kupata usingizi ukiwa na mimba. Unaweza ongeza idadi kidogo ya mafuta muhimu ili kuimarisha kipindi chako cha kuoga. Kuoga kuna kusaidia kufungua mishipa ya damu na pia kuboresha mzunguko wako wa damu.

Pia, miundo ya usingizi hubadilika katika kipindi chote cha ujauzito. Wanawake wanapaswa kuchukua hatua kuhakikisha kuwa wanapata masaa 8-10 yanayo shauriwa ya usingizi kila siku. Ili kuboresha ubora wa usingizi katika mimba, unaweza oga na maji moto, kunywa maji mengi na ulale kwa mtindo wenye starehe.

Chanzo: nhlbi.gov

Soma Pia:Mambo Yote Unayo Paswa Kujua Kukosa Maji Tosha Mwilini Ukiwa Na Mimba

 

Written by

Risper Nyakio