Unapokuwa na furaha, mimi pia nina furaha. Huu ni usemi ambao karibu kila mzazi amemwambia mtoto wake katika kipindi kimoja ama kingine. Ndiyo sababu kwa nini unafanya yote unayoyafanya ili watoto wako wafuzu maishani wanapokuwa watu wazima. Kwa hivyo sio lawama yako kuwa unatia juhudi zote ili kuwaona watoto wako wakiwa na furaha. Nini muhimu katika kulea watoto wenye furaha? Mbali na michezo ya video na peremende? Inapofika kwa mambo ya kumlea mtoto mwenye furaha, wanasayansi waligundua kuwa jambo la kwanza na lililosawa ni kuwauliza watoto. Waliwauliza watoto kilichowafanya wafurahi.
Kinachomfanya Mtoto Awe Na Furaha Kulingana Na Sayansi

Katika mwaka wa 2009, somo lilifanyika kubaini kinachowafanya watoto wahisi furaha. Bila shaka vitu vya kwanza vilikuwa vya kifedha, hata hivyo, kulikuwa na nambari ya vitu visivyo hitaji pesa. Baada ya watoto kuulizwa wachague kati ya vitu vilivyo orodheshwa, ilikuwa bayana kuwa vitu vilivyoshinda havikuwa vya kifedha. Mahusiano na watu wengine ikilinganishwa na bidhaa za kiteknolojia.
Kulingana na utafiti, vitu ambavyo watoto waliamua kubaki navyo ni kwa sababu vilihusiana na watu wengine. Kwa mfano, watoto walichagua kubaki na rununu kwa sababu ziliwasaidia kuzungumza na watu wengine.
Jinsi ya kulea watoto wenye furaha

Hauwezi lea watoto wenye furaha ikiwa wewe mwenye hauna furaha. Huwezi mwaga kutoka kwa kikombe kisicho na kitu. Lazima wazazi wahakikishe kuwa wanafuraha. Wazazi wenye furaha huwa na watoto wenye furaha. Unapokuwa na furaha, utaweza kuangalia mambo kwa kina, tofauti na unapokuwa na hasira wakati wote. Huenda ukafanya uamuzi kulingana na hisia unazokuwa nazo siku hiyo.
- Wafunze watoto kutengeneza marafiki
Sote tunafahamu kuwa uhusiano ni muhimu, lakini sio wazazi wote wanaochukua muda kuwafunza watoto jinsi ya kutengeneza marafiki na kudumisha urafiki huo. Jambo la kwanza ni kuwafunza watoto kuwa wakarimu na wenye huruma kwa watu walio karibu nao. Mbali na kutengeneza urafiki, watakuwa watu bora zaidi duniani.
- Wafunze kuwa na mtazamo chanya
Ikiwa ungependa kumlea mtoto mwenye furaha, mfunze angali mchanga kutokuwa na mtazamo hasi kuhusu kila kitu. Badala yake, awe na imani kuwa mambo mema yatatendeka.
Mbali na hayo, usimtarajie mtoto wako kufanya kila kitu kwa njia inayofaa. Ila, mhimize afanye kazi hata kama hazifikia viwango vyako, cha maana zaidi ni kuwa anajaribu, mpongeze kwa juhudi zake. Kwa njia hii, atakuwa na motisha ya kufanya kazi zaidi. Hakikisha kuwa mazingira ya watoto wako ni bora kwani yanachangia pakubwa katika kulea watoto wenye furaha.
Soma Pia: Mambo 5 Usiyo Yafahamu Kuhusu Familia Ya Billionea Peter Obi