Mama mjamzito hushuhudia mabadiliko mengi katika safari yake ya mimba. Asipopata lishe bora, huenda akawa katika hatari ya kuugua. Kuna vitu ambavyo mama anaweza kuangazia ili kulinda dhidi ya anemia katika mimba.
Anemia ni hali ambapo mama huwa na seli za damu nyekundu chache mwilini. Anapougua kutokana na hali hii, atakuwa na ishara kama vile uchovu wa mara kwa mara, mikono na miguu iliyoganda, kuhisi kizunguzungu na matatizo ya kupumua.
Kuna baadhi ya vitu ambavyo mwanamke anaweza fanya ili kuhakikisha kuwa ana afya bora katika mimba na kujilinda dhidi ya kupata anemia.
Kulinda dhidi ya anemia katika mimba
1.Lishe bora

Lishe bora na yenye afya ni chanzo kizuri cha chuma. Lishe bora husisitizwa kwa mama mwenye mimba. Kula lishe yenye afya kunamlinda dhidi ya hali nyingi tofauti katika ujauzito. Sahani ya mama mjamzito inapaswa kuwa na aina zote za virutubisho. Protini, wanga, fiber, vitamini na maji. Vyanzo bora ni kama vile mayai, maharagwe, samaki, nyama kutoka kwa ndege wa nyumbani, njugu, nafaka, mboga za kijani na matunda kama ndizi na strawberries.
2. Vitamini za prenatal

Vitamini za prenatal huwa na wingi wa madini muhimu katika mimba. Baadhi ya madini haya ni kama vile asidi ya folic na chuma. Ni njia nzuri kwa mjamzito kuhakikisha kuwa anapata madini yote na tosha. Wanawake wanaopanga mimba hushauriwa kuanza kuchukua vitamini za prenatal miezi miwili kabla ya kuanza juhudi za kushika mimba.
3. Virutubisho vya chuma

Mjamzito aliye na viwango vya chini vya chuma anahitajika kuchukua virutubisho vya chuma ama supplements ili kufikisha viwango hitajika kwa chuma vya kila siku. Hata hivyo, virutubisho hivi vinapaswa kushauriwa na daktari na wala sio kununua bila ujuzi wa daktari. Mjamzito anahitaji miligramu 27 za chuma kwa siku. Chukua vitamini C pamoja na virutubisho vya chuma ili kuuwezesha mwili kuweza kuzitumia mwilini.
Fanya hivi ili kuboresha kiwango cha virutubisho vya chuma unavyochukua:
- Ongeza njugu kwenye oats na maziwa ya bururu
- Ongeza mboga za kijani kwenye lishe yako
- Kula matunda yenye vitamini C kama vile ndizi
- Kula kuku, nyama na samaki mara zaidi kwa wiki
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Lishe Katika Mimba: Mambo Unayopaswa Kufanya na Usiyopaswa Kufanya