Kemia Na Utangamano Katika Uhusiano: Nini Muhimu Zaidi?

Kemia Na Utangamano Katika Uhusiano: Nini Muhimu Zaidi?

Kemia na utangamano ni muhimu katika uhusiano na hakuna linalo paswa kupuuzwa.

Kemia katika uhusiano kwa urahisi ni vitu unavyo ona na vinavyo kuvutia kwa mtu unapo muona na kukufanya uhisi kana kwamba ungependa kuwa naye. Kinacho kuvutia kwao, hisia hizo… kuvutiwa kwake mara tu unapo waona mara ya kwanza ama baada ya kumwona mara kadhaa… hiyo ndiyo kemia.

kemia katika uhusiano- wanandoa

Picha shukrani kwa: Shutterstock

Vitu vinavyo wafurahisha watu wanapo onana kwa mara ya kwanza huwa tofauti. Baadhi ya wanawake hufurahishwa na urefu na rangi ya uso ya mwanamme, viatu vyake, mavazi aliyo valia ama hata anavyo nukia. Kwa wanaume, huenda waka furahishwa na jinsi mwanamke anavyo jibeba, anavyo ongea, urembo wake na kadhalika. Ukipatana na mtu ambaye ana kufurahisha na unamfurahisha hiyo ndiyo kemia. Huwa kitu cha juu juu bila kuongea sana na kujua ikiwa mnapenda vitu sawa ama mna maono tofauti kuhusu mambo mbali mbali maishani.

chemistry in relationships

Huenda mkawa na kemia na mtu na mkose utangamano. [Credit – Readers Digest]

Utangamano katika uhusiano unakusaidia kung’amua iwapo mvuto huo kwa mtu fulani una thamani, ikiwa ni kitu ambacho ungependa kidumu ama hakina maana na utakitupilia mbali na uendeleze maisha yako.

Wakati ambapo kemia hukuvuta kwa mtu fulani, utangamano unakusaidia kujua iwapo utakaa nao ama la.

Undani ni muhimu lakini hapa, mambo ya juu yana maana pia. Huwezi ingia katika uhusiano ama ndoa na mtu kwa sababu una dhamini kilicho kwenye akili na mawazo yao; pia huwezi anza uhusiano na mtu kwa sababu imani zenu ni sawa… mvuto huo wa kifizikia ni muhimu na unahitajika. Kumtamani mchumba wako kimapenzi, na kuvutiwa kwao ni jambo muhimu sana. Huwezi puuza jambo moja na kudhamini lingine zaidi.Unapo pata kemia katika uhusiano bila utangamano, usitarajie mengi kutoka kwa uhusiano huo. Na unapo pata utangamano bila kemia, pia kuna kiwango chake cha shaka. Cha muhimu unapo anza uhusiano na mtu ni kusawasisha utangamano na kemia kwani mawili haya ni muhimu sana.

Soma pia: Vitu 6 Muhimu Vya Kumfanyia Bibi Yako

Written by

Risper Nyakio