Muda baada ya kujifungua kwa mama huwa kipindi kirefu chenye misuko suko mingi. Mtoto anahitaji wakati mwingi na bado anasumbua huku mwili wa mama bado ukitaka muda upone baada ya kujifungua. Ikiwa alijifungua kupitia kwa njia ya upasauji, mwili wake unahitaji muda zaidi kupona kidonda. Mbali na hayo, hawezi kufanya kazi ngumu ama kuinama kwani kidonda kingali kupona. Kucheka, kukohoa na kuchemua ni balaa kwani kidonda huuma kwa sana.
Mchumba wako hata ingawa amekuwa akikuegemeza, hajayapitia yote uliyo yapitia na huenda asielewe unachokipitia. Kujifungua huchukua nishati nyingi ya mama kifizikia na kiakili. Wakati ambapo ungependa akusaidie na kazi zingine, huenda akawa ana endelea na kazi zake za kila siku kama ilivyo kawaida yako. Hana shaka kuhusu uchungu unaoupitia baada ya kujifungua. Ama huenda anakusaidia na mtoto mara kwa mara.

Mama mpya huenda akakasirishwa na vitu vidogo vidogo ama kwa kuona kuwa bwanake hamsaidii. Na kufanya mama ahisi kuwa anamchukia. Hii ni chuki na maarufu katika uhusiano baada ya mtoto. Hii sio kumaanisha kuwa hupendi baba wa watoto wako. Walakini sio mtu unayempenda zaidi katika kipindi hiki. Kwa nini mama huwa na chuki kwa bwana yake baada ya kujifungua?
Kumchukia Bwana Baada Ya Kujifungua
Mara nyingi hisia hii husababishwa na jinsi ambavyo mama anahisi baada ya kujifungua. Mwili wake unapona na mtoto anamhitaji kwa sana. Kuna mabadiliko mengi yaliyofanyika mwilini mwake ikilinganishwa na hapo awali kabla ya kupata mimba. Pia, umeanza maisha mapya ya kuwa mama. Kufahamu haya yote humzidia mama, pia, sio mambo yanayo isha baada ya siku mbili, ni maisha yake mapya, wazo hili huenda likamfanya mama kumchukia bwana yake baada ya kujifungua.
Maisha ya wanandoa ya kimapenzi yata athiriwa. Ni suala maarufu kati ya wanandoa wanapopata watoto na linalotibika.
Kwanini mama anamchukia bwanake
Baada ya kupata mtoto, mama bado anajaribu kung'amua njia yake katika maisha mapya ya kuwa mama. Uchungu wa kifizikia baada ya kujifungua na mawazo mengi yanayomfanya kuchoka. Kumtunza mtoto wiki za kwanza chache baada ya kujifungua huchukua nishati nyingi.
Jinsi ya kutatua suala hili
Kubadili mawazo yako ndiyo hatua ya kwanza. Kwa kuelewa kuwa utashuhudia mhemko wa hisia ambazo hazihusiki na mchumba wako. Mchumba anapaswa kuwa na uvumilivu zaidi mama anapo pona na kumsaidia vyovyote vile awezavyo.
Hakikisha kuwa unalala vya kutosha, hata kama ni vigumu ukiwa na mtoto mchanga. Jaribu uwezavyo. Kunywa maji tosha, kula vyema na ujipe muda wa mapumziko mara kwa mara.
Kudumisha uhusiano baada ya kujifungua

Zungumza
Ongea na mchumba wako kuhusu unavyo hisi ili aweze kukuelewa. Baada ya kukasirika, mweleze kinacho endelea kisha kwa pamoja mtafute suluhu.
Panga kuhusu chuki
Kumchukia bwanako baada ya kujifungua huwa maarufu, kwa hivyo ni vyema kwa mama kufahamu hivi kabla na kuzungumza na bwanake. Ikiwezekana, zungumza na wataalum wa ndoa.
Mama anaweza kuzungumza na wataalum wa ushauri anapo anza kuwa na mawazo hasi kujihusu na kuhusu mtoto.
Chanzo: Healthline
Soma Pia:Sababu Na Matibabu Ya Kukosa Hamu Ya Tendo La Ndoa