Ishara Zinazo Ashiria Kuanza Kumea Meno Katika Watoto

Ishara Zinazo Ashiria Kuanza Kumea Meno Katika Watoto

Kumea meno katika watoto huanza wanapo kuwa miezi kati ya minne na saba, huku wengine wakipata meno baadaye maishani mwao.

Kumea meno katika watoto huanza wanapo kuwa miezi kati ya minne na saba, huku wengine wakipata meno baadaye maishani mwao. Usiwe na shaka ikiwa mtoto wako hatakuwa ameanza kumea meno katika miezi hii. Kumbuka kuwa kila mtoto ni tofauti.

Ishara za kuanza kumea meno katika watoto

kumea meno katika watoto

Ishara maarufu watoto wanapo anza kumea meno ni kama vile:

 • Ufizi ulio fura na laini
 • Kuwa na vurugu na kulia
 • Ongezeko la joto mwilini mwake
 • Kukohoa
 • Kuvuta masikio yao
 • Kuleta mikono yao mdomoni mwao
 • Mabadiliko katika mitindo yao ya kula na kulala
 • Kutaka kula vitu vigumu
 • Kumwaga mate sana na huenda akapata upele usoni

Mtoto anapo anza kumea meno atahisi uchungu, lakini sio lazima awe mgonjwa. Ukigundua kuwa mtoto wako ana harisha, kutapika ama ana upele mwilini, joto jingi, na kukohoa, hakikisha kuwa unampeleka hospitalini kwani hizi sio ishara za kuota meno. Pia, unapo gundua ufizi wake unavuja damu ama kufura usoni.

Dawa ya kuota meno

Huenda dawa za kusugua kwenye ufizi wa mtoto kupunguza uchungu wa kuota meno zikakosa kufanya kazi. Zina oshwa kwa urahisi na kwenye nyuma ya koo ya mtoto na kumfanya atatizike kumeza. Epuka kununua madawa kwenye zahanati kwani huenda yakawa na bidhaa hatari kwa mtoto mwenye umri chini ya miaka miwili. Tumia dawa za kupunguza uchungu kama acetaminophen na ujitenge na ibuprofen.

Jinsi ya kutunza meno yanayo kua ya mtoto

kumea meno katika watoto

Afya nzuri ya mdomo ni muhimu hata kabla aanze kuota meno:

 • Kabla ya meno kuanza kuota, hakikisha unasafisha ufizi wa mwanao kwa kutumia kitambaa kisafi mara moja kwa siku
 • Anapo ota meno, safisha mdomo wake kwa njia sawa mara mbili kwa siku. Hasa baada ya kumaliza kula
 • Baada ya siku ya kusherehekea kuzaliwa kwao ya kwanza, tumia mswaki ulio laini, maji na kiwango kidogo cha dawa ya meno isiyo na flouride.

Mtaalum wa afya ya watoto atamkagua mara kwa mara kuhakikisha kuwa meno yake haya haribiki na kukushauri wakati bora wa kuanza kumpeleka kwa daktari wa meno.

Soma Pia: Vidokezo Vya Kubaki Na Afya Unapo Safiri Barabarani

Written by

Risper Nyakio