Njia Tofauti Za Kumfanya Mchumba Wako Akuwaze Ukiwa Mbali

Njia Tofauti Za Kumfanya Mchumba Wako Akuwaze Ukiwa Mbali

Kuwa na utangamano wa karibu na mchumba wako ni muhimu sana. Hizi ndizo baadhi ya njia za kumfanya mchumba wako akufikirie.

Vidokezo Vya Kumfanya Mchumba Wako Akufikirie Ukiwa Mbali

Huenda ukawa umejaribu mbinu zote unazo jua ili kumfanya akufikirie na kukupigia simu mara kwa mara, lakini unapungukiwa na mawazo. Unajaribu kufanya mapenzi yenu yakue na umbali wenu lakini haufanikiwi. Leo tunakujuza vidokezo muhimu vya jinsi ya kumfanya mwenzi wako akufikirie mara zote.

kumfanya mchumba akufikirie

  1. Wacha vitu nyuma kimaksudi

Andika maneno ya kimapenzi kisha uwache nyuma kimaksudi. Atakukumbuka na mema yote mliyo fanya pamoja kila mara anapo ona maneno hayo.

2. Valia manukato ya kipekee

Kuwa na harufu ya kipekee yenye kuvutia na mnapo achana, harufu ile itamkumbusha kukuhusu. Kumbuka kuwa harufu ina husishwa na fikira za kilicho tendeka.

3. Valia mavazi ya kuvutia

Wanaume wanafahamika kama viumbe wa kuona. Kwa hivyo hakikisha kuwa unavalia mavazi yanayo vutia ili mchumba wako akukumbuke mnapo achana. Na hata mnapo patana, hata penda mtengane kwani anafurahishwa na ulivyo.

christmas gift ideas

4. Mtunze mpenzi wako

Hakuna asiye penda kutunzwa na zawadi za kupendeza, hasa kutoka kwa mchumba wake. Kuna mwonyesha kuwa anapendwa na anamfikiria kila wakati. Hakikisha unamnunulia vitu anavyo vipenda. Kila mara akiona kitu ulicho mnunulia, atakuwa anakukumbuka. Kwa hivyo tia juhudi kufahamu vitu anavyo vipenda kisha ujikakamue kumnunulia.

Soma piaMambo ya kuvutia ambayo wanandoa wanaweza jaribu kitandani

Written by

Risper Nyakio