Sababu Kwa Nini Unapaswa Kumkumbatia Mtoto Wako Zaidi

Sababu Kwa Nini Unapaswa Kumkumbatia Mtoto Wako Zaidi

Kumkumbatia mtoto wako hakusaidia kuboresha uhusiano wenu tu, mbali katika kukuza ubongo wake. Kwa hivyo, hakikisha kuwa unamkumbatia mara kwa mara.

Wanasema kuwa mapenzi ni kiinimacho. Na kila mtu hasa watoto wako, wanahitaji mgusi na kiinimacho cha mapenzi ili kukua kihisia na fizikia. Mapenzi yanayo fanya ubongo wako kukua zaidi huenda ukaonekana kama chembe cha kiinimacho, lakini utafiti mpya umepata kuwa hivi ndivyo ilivyo. Soma linasema kuwa kadri unavyo zidi kuwakumbatia watoto wako, ndivyo ubongo wao unavyo kua. Oxytocin ina jukumu la kusaidia ukuaji huu. Na makala haya yata kuelezea kuhusu mchakato huu na kwa nini unapaswa  kumkumbatia mtoto wako zaidi. Mapenzi kwa kweli yana sisimua!

Je, oxytocin ni nini?

kumkumbatia mtoto wako

Kuna homoni ambayo ubongo hutoa inayo fahamika kama homoni ya mapenzi.

Kwa kisayansi, ina julikana kama oxytocin. Homoni hii ya mapenzi iko kwa kila mtu, wote waume kwa wake. Ina jukumu la kuanza mchakato wa uzalishaji wa watu, kuanza na imani na kuibua hisia za kimapenzi.

Na kwa hivyo kuwa homoni inayo anzisha mzunguko wa maisha ya mtu ambapo tunapata mapenzi, pata mtoto, na kuwalea watoto. Sio jambo la kushangaza kuwa ina saidia kukuza utangamano kati ya wazazi na watoto. Hufanya hivi kwa kuibua hisia za raha na vituo vya tuzo, chanzo cha utangamano wa kijamii kati ya watu walio karibu zaidi nawe.

Cha zaidi ni kuwa, oxytocin ni bora katika kusaidia ukuaji wa akili. Ili kuwa hasa zaidi, ina egemeza kutengenezwa kwa mishipa ya damu kwenye tezi ya pituitary. Tezi hii ina husika na michakato ya kisaikolojia kama vile uzalishaji, fikira nyingi na ukuaji.

watu mashuhuri kenya na mama zao

Kama tulivyo angazia umuhimu na jukumu za oxytocin kwa wanadamu. Kuna njia tatu ambazo ina achiliwa mwilini. Na inapo achiliwa, ina fanya mambo mema kwa watoto na akili zao na kuboresha utangamano kati ya mtoto na mzazi. Hii ni sababu tosha kwa wazazi wengi kutaka kuwaonyesha watoto wao mapenzi mengi ya kifizikia. Lakini, wazazi wanaweza athiri vipi kuwachiliwa kwa homoni hii? Ni rahisi: kwa kuwakumbatia.

Kulingana na Infant Grapevine, oxytocin ina achiliwa kutoka kwa njia tatu tofauti. Ina boresha utoaji wa homoni zingine za raha kama vile serotinin, dopamine, noradrenaline na opioids. Kwa hivyo, inapo boresha, kuna tabia za athari za kisaikolojia zinazo tendeka.

Mapenzi ya kifizikia sio jambo ambalo wazazi wa kiafrika huwa makini nalo. Walakini, kadri unavyo zidi kuingiliana na kuwakumbatia watoto wako, ndivyo oxytocin inavyo tolewa na sio kwa watoto tu, mbali kwa wazazi pia. Pia, tuna pitisha homoni ya mapenzi kupitia kwa muingiliano wetu. Kwa hivyo, hakikisha kuwa unam kumbatia mtoto wako mara kwa mara kama sio kila mara, ili apate faida zote zinazo andamana na kumkumbatia mtoto wako.

Soma Pia:Jinsi Ya Kufunza Watoto Mtindo Wa Maisha Wenye Afya Shuleni Na Nyumbani

Written by

Risper Nyakio