Jinsi Ya Kumlinda Mtoto Wako Mchanga Kutokana Na Virusi Vya Korona

Jinsi Ya Kumlinda Mtoto Wako Mchanga Kutokana Na Virusi Vya Korona

Afya ya mtoto wako inapaswa kupatiwa kipau mbele hasa watoto wanapo rudi shuleni. Gundua jinsi ya kumlinda mtoto wako kutokana na homa ya korona.

Huku dunia yote ikiwa imesimama kufuatia vumo la janga la virusi vya korona, kiasili, wamama wengi wana shaka kuhusu watoto wao kuugua virusi vya COVID-19. Hata kama kwa sasa ime dhibitishwa kuwa virusi hivi ni vyepesi kwa watoto wachanga, kukosa kuwa na chanjo ya virusi hivi kuna tia shaka. Gundua jinsi ya kumlinda mtoto wako kutokana na virusi vya korona.

Je, Nita mlinda vipi mtoto wangu kutokana na virusi vya korona?

jinsi ya kuepuka kupata virusi vya corona

Kwani wanawake wenye mimba wana nafasi zaidi za kuugua virusi vya korona na kusababisha matatizo ya kupumua, matarajio ni kuwa wana nafasi zaidi za kupata maradhi haya. Hii ni kwa sababu unapokuwa na mimba, kinga ya mwili iko chini. Mafua yako punguka na unahitaji hewa zaidi. Walakini, kulingana na utafiti wa hivi majuzi kutoka Uchina, wanawake wenye mimba hawaku ugua virusi hivi kama ilivyo tabiriwa. Habari njema ni kuwa placenta hufanya kazi nzuri katika kumlinda mtoto aliye tumboni mwako.

Huwa jambo tofauti mtoto anapo zaliwa, ukitia akilini kuwa kuna mtoto Umarekani aliye kuwa na vipimo chanya vya virusi vya korona punde tu alipo zaliwa. Hata kama madaktari hawana uhakika, wana fikiria kuwa mtoto aliugua maradhi hayo baada ya kuzaliwa. Hapa chini kuna njia chache za kumlinda mtoto wako kutokana na virusi vya korona:

  • Boresha usafi

kumlinda mtoto kutokana na virusi vya korona

Usafi ni hatua ya kwanza ya kulinda dhidi unayo stahili kuboresha ili kupigana dhidi ya virusi vya homa ya corona. Ili kumlinda mtoto wako, una paswa kuwa makini na watu wanao mkaribia. Hakikisha kuwa hawamgusi na mikono michafu. Kabla ya kumshika, wanawe mikono kwa kutumia maji na sabuni.

Pia, kwani watoto wanapenda kujigusa uso na kuweka vidole mdomoni, osha mikono yake na uso kisha usafishe vyombo na sehemu karibu naye ambazo huenda akagusa. Na kama mama unapaswa kufuata hatua hizi pia.

Tahadhari za vitakasa mikono

Tafadhali tia akilini kuwa vitakasa mikono vya vileo havipaswi kutumika bila usimamizi wa mtu mzima. Pia, vinapaswa kuwa mbali kuepuka kufikia na kuweka mdomoni. Hapa kuna vidokezo vya vitakasa mikono unavyo paswa kukumbuka:

  1. Msimamie mtoto wako anapo tumia vitakasa mikono
  2. Tumia kiwango kidogo cha vitakasa mikono
  3. Sugua mikono yao pamoja hadi ikauke ama uwafunze jinsi ya kusugua mikono hadi kitakasa mikono kikauke
  4. Mkumbushe mtoto wako asiweke mikono yake kwenye mdomo baada ya kupaka kitakasa mikono
  5. Usinunue vitakasa mikono vinavyo nukia ili wasiwe na fikira za kula mikono yao
  6. Weka vitakasa mikono vyote mbali, mahali ambapo watoto hawata fikia
  7. Ikiwa una shuku kuwa mtoto wako amekula kiwango chochote cha kitakasa mikono, wasiliana na daktari kasi
  • Amepata chanjo zote

Njia hakika ya kuwalinda watoto dhidi ya magonjwa ni kuhakikisha kuwa wamepata chanjo zote wanazo faa. Ni kweli kuwa hakuna chanjo ya virusi vya homa ya korona iliyo pitishwa. Lakini kumlinda mtoto wako dhidi ya magonjwa kuna maana kuwa, anapo pata virusi vya korona, mfumo wake wa kinga hauta zidiwa. Na utaweza kupambana dhidi ya virusi hivi.

Na je, mama akipata virusi vya homa ya korona?

Ili kumlinda mtoto kutokana na virusi vya korona, kama mama, unapo ugua maradhi ya korona, hakikisha kuwa unachukua hatua zote badala ya kuwa na wasiwasi. Valia barakoa unapokuwa na mtoto wako na unawe mikono kabla na baada ya kumgusa. Pia, unapo hisi kuchemua ama kukohoa, tumia upande wa ndani wa kiwiko chako. Hakikisha umesafisha kila mahali na vifaa vya kumlisha mtoto wako ili kulinda afya yake.

Vyanzo: Livescience, hopkinsmedicine

Soma Pia:Vidokezo Salama Vya Kuepuka Kuambukizwa Homa Ya Korona

Written by

Risper Nyakio