Vidokezo Muhimu Kukusaidia Kufahamu Jinsi Ya Kumlisha Mtoto Asiye Penda Kula

Vidokezo Muhimu Kukusaidia Kufahamu Jinsi Ya Kumlisha Mtoto Asiye Penda Kula

Kuto penda chakula ni kawaida kwa watoto, wana jaribu kutafuta kinacho wapendeza na kisicho wapendeza. Ni vyema kwa wazazi kuwa watulivu sana katika kipindi hiki.

Kila mzazi ameshuhudia tatizo hilo katika mara moja ama nyingine. Siku moja mtoto wako atakula vyema lakini wakati unaofuata hata taka kula chochote. Kuto penda chakula ni kawaida kwa watoto, wana jaribu kutafuta kinacho wapendeza na kisicho. Huenda ikawa wakati wa kukukwaza unapo jaribu kufikiria cha kuwa tengenezea na ambacho pia watakula. Hapa kuna mambo machache unaweza fanya kurahisishia kufahamu jinsi ya kumlisha mtoto asiyependa kula.

Jinsi ya kumlisha mtoto asiyependa kula

  1. Sinia ya chakula

kumlisha mtoto asiyependa kula

Tengeneza sinia ndogo ya mtoto wako asiyependa kula iliyo na sampuli tofauti ya vyakula wanavyo penda. Watoto wachanga wanapenda kula vyakula vidogo vidogo. Kuwapa vyakula vya kuchagua kutawasaidia kukumbatia kula vyema zaidi. Watengenezee sinia yenye matunda na mboga wanazo zipenda na wakati mwingine kuviita majina ya kupendeza kutamsaidia mwanao kuwa na uhusiano mwema na chakula.

Sababu nyingine kwa nini watoto hukosa kula ni kwa sababu hawataki kusima na kupata muda wa kula. Kwa hivyo, wape sinia yenye chakula na uwape angalau masaa mawili wamalize. Kwa njia hiyo, wanaweza kula bado wakicheza. Huenda ikawa sio njia bora zaidi ya kula, lakini angalau watakula.

2. Wape vitu vya kuongeza kwenye chakula 

 

Vitu kama vile tomato sauce. Watoto wanapenda kuongezea vitu kwa chakula ama hata siagi ya njugu. Hata kama wata jichafua wanapo fanya hivi, wata weza kukula.

3. Ongeza vitu vya kupaka

Watoto wanapenda kujaribu vitu vipya na kuvipaka. Vitu kama siagi kwenye mkate ili kuwa himiza kula mkate. Badala ya kujichafua, wafunze jinsi ya kutumia kijiko ama kisu cha kupaka.

4. Ongeza vitu juu

Watoto wanao zidi kukua na wanasoma kutengeneza vitu na akili zao. Wanapenda kuongeza vitu juu. Kwa hivyo, wakubalishe kuongeza chochote wanachotaka juu ya chakula.

Kutengeneza njia ya kuwa kubalisha kuongeza vitu wanavyo taka kwa chakula chao kutafanya wawe na hamu zaidi ya kuvila. Kama vile kuongeza maziwa ya bururu, ama vipande vya chokleti ama matunda. Chochote wanacho kipendelea, wakubalishe ilimradi wale.

5. Fanya kiwe kinywaji

Vidokezo Muhimu Kukusaidia Kufahamu Jinsi Ya Kumlisha Mtoto Asiye Penda Kula

Watoto wanapenda kunywa vitu, kwa hivyo kuvisiaga viwe vinywaji ni jambo la busare. Unaweza wasiagia matunda wasio penda kula na kuchanganya na maziwa ya bururu ama maziwa ya kawaida. Mhusishe kwenye utaratibu wa kutengeneza kinywaji hicho na bila shaka wata furahia.

6. Panda

Anzisha shamba ndogo nyuma ya nyumba na wewe na mwanao mnaweza fanya kazi pamoja. Watapendelea wazo la kula vyakula walivyo kuza. Pia, kuwa husisha katika utunzaji wa shamba hilo kuta panua akili zao na kuhakikisha wana kitu cha kufanya.

Kuna mambo mengi ambayo unaweza jaribu ili kumlisha mtoto asiye penda kula na kuhakikisha kuwa anapokula, chakula kina afya. Jaribu baadhi ya vidokezo tulivyo angazia na uangazie kinacho mhimiza mtoto wako kula zaidi.

Soma PiaSababu Kwa Nini Unahitaji Utaratibu Wa Kulala Yako Na Watoto Wako

Written by

Risper Nyakio