Kulingana na wataalum wa afya ya watoto wachanga, mtoto anapaswa kulishwa maziwa ya mama kwa miezi ya kwanza sita. Na baada ya kuanzishwa chakula katika miezi sita, mama anastahili kumlisha mtoto mchanga maziwa hadi anapo fikisha mwaka mmoja.
Hata hivyo, sio wanawake wote wanao weza kuwanyonyesha watoto wao kwa sababu mbali mbali.

Baadhi ya wanawake wasio weza kunyonyesha
- Mama anaye hitajika kazini muda mfupi baada ya kujifungua
- Mama aliye na virusi vya ukimwi ata shauriwa kuto mnyonyesha mtoto wake ili kupunguza hatari ya kumwambukiza mtoto na virusi hivyo.
- Mwanamke anaye tatizika kutoa maziwa tosha kumtosheleza mtoto huenda akashauriwa kumpa mtoto formula.
- Mwanamke anaye kwazwa kimawazo huenda akatatizika kutoa maziwa tosha ya kumnyonyesha mtoto
Manufaa ya kumnyonyesha mtoto
- Maziwa ya mama yana virutubisho ambayo mtoto mchanga ana hitaji
- Ni rahisi kwa mtoto mchanga kuchakata maziwa ya mama
- Yana kinga mwili zinazo mlinda mtoto kutokana na maambukizi
- Kukuza mfumo wa kinga wa mtoto na kumlinda dhidi ya magonjwa kama kisukari na asthma
Manufaa ya kunyonyesha kwa mama
- Kumsaidia kupunguza uzito baada ya kujifungua
- Kumlinda dhidi ya saratani ya ovari na ya matiti
- Kuboresha utangamano kati ya mama na mtoto
Kumlisha mtoto mchanga

Mtoto mchanga hula mara nane hadi kumi na mbili kwa siku, katika siku za kwanza baada ya kuzaliwa. Mama anashauriwa kumnyonyesha kwa dakika 10-15 titi moja kabla ya kumbadilisha.
Mtoto hulishwa anapo hitaji, kuna ishara zinazo onyesha kuwa mtoto ana njaa na anastahili kulishwa. Anapo anza kulia, kutoa sauti kana kwamba ana nyonya na anapo jaribu kuingiza vidole vyake kwenye mdomo. Kufungua mdomo, kutafuta chuchu ya mama na kutoa ulimi nje.
Mtoto anapo lala kwa zaidi ya masaa manne, mama anastahili kumwamsha ili amlishe. Katika wakati huu, ni mapema kuwa na ratiba ya kumlisha mtoto. Ila anavyo zidi kukua, mama atahitaji kudhibitisha ratiba ya kumnyonyesha mtoto wake.
Mtoto anaye pata lishe tosha hubadilishwa nepi zilizo jaa mara sita hadi nane kwa siku. Kulala vyema zaidi usiku na kuonekana ana ongeza uzito wa mwili.
Soma Pia: Mlishe Mtoto Wako Vyakula Hivi Ili Kuhimiza Kurefuka Kwake!